Mzungu kutoka Uingereza anasema: Rais Kikwete ni mmojawapo ya viongozi wa Kiafrika, ni kiongozi wa amani katika muda huu, anayeongoza nchi inayosadikiwa kuwa ni tajiri sana duniani hususani katika suala la rasilimali za asili,lakini anaongoza duniani kwa kuwa ombaomba, makampuni ya kigeni yameshajua kuwa Tanzania ni nchi huru sana tena rahisi, ambapo mtu yeyote anaweza kwenda na kuchukua vyote kadiri anavyoweza bila kuulizwa, Sipati picha akili za viongozi wa Tanzania zikoje hasa Kikwete Rais wa nchi anayeabudu wazungu. Kwa kipindi cha miaka nane (8) niliyofanya kazi nchini Tanzania nikiwa mfanyakazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP), niligundua namna viongozi wan chi ile wasivyo na uwezo na ni wala rushwa. Uongozi wan chi ile umejaa rushwa, hata mawaziri wake walioomba na kupokea rushwa katika Kampuni ya BAE System katika sakata la rada hawajawahi kuchukuliwa hatua pamoja na ushahidi wa wazi uliopatikana. Walipa kodi wa uingereza wanapaswa kuacha kabisa kufadhili safari zake nyingi za nje……. Kikwete hakupaswa kwenda Davos kuomba, alipaswa kuona aibu kuiambia dunia kuwa Tanzania ni nchi masikini, watu wake wanaishi katika uchumi usioweza kutengeneza hata ziada ndogo (hand to mouth economy), hata ukilinganisha uchumi wa nchi ndogo kama Palestina, Haiti, Lebanon Rwanda hata Somalia, uchumi wao pengine una nguvu zaidi kuliko wa Tanzania. Tunapaswa kuishangaa nchi yeyote duniani inayokaribisha na kuendekeza utani wa aina hii kwa kigezo cha kutoa misaada kwa Tanzania. Kikwete anapaswa azuiliwe kusafiri nje ya nchi, "no fly zone" ili awe makini………………"