Kikwete, Rais anayeangushwa na watendaji wabovu...

Kikwete, Rais anayeangushwa na watendaji wabovu...

Chilisosi

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2008
Posts
3,050
Reaction score
748
Hivi karibuni kwenye vyombo vya habari tumekuwa tukisoma vituko ambavyo kwa kweli naviita ni vya kijinga au kitoto kuhusu waziri wa viwanda na biashara Abdalah Kigoda na sakata la TBS, shirika ambalo ni nyeti sana.

Ni huyu huyu Kigoda alieuza nyumba zetu za serikali wakati wa serikali ya mkapa.

Mie najiuliza hivi ni kwa nini Kigoda anafanya mambo haya bila kuwa na aiubu wala kuogopa lolote?

Mie ni mwanachama wa ccm kwa zaidi ya miaka 20 sasa lakini nakatishwa tamaa na vitendo vya mawaziri wabovu kama hawa.

Inakuwaje huyu kigoda alazimishe kampuni iliyofungiwa kwa utendaji mbovu ipewe tenda ya ukaguzi wa magari wakati TBS wenyewe wamesema haifai? NINI MAANA YA VIWANGO?

Kuna mawaziri wanaopiga kazi vizri sana kama mwakyembe na magufuli lakini Kigoda naona ni kama kituko tu na sijui kwa nini kikwete alimpa nafasi hii nyeti. sasa kulikuwa na maana gani ya kumuondoa Chami? basi chami alionewa.

Kwa nini kigoda anawafanya watanzania wapumbavu?

Umepewa rushwa kiasi gani mpaka uwadharau watendaji wote wa TBS?

Sisi wafanyakazi wa TBS hatutakubali, na tunakuambia kuwa tutaumbua madudu yote yaliyofanywa na hiyo kampuni ya WTM unayolazimishwa ipewe tenda wakati bado hata hela walizokuwa wakifanya ukaguzi kwa miaka mitano iliyopita hawajazifikisha hapa TBS.

Leo unaandikwa magazetini lakini ujue iko siku nguvu ya umma itakuhukumu.

YANA MWISHO HAYA
 
UNaumiza kichwa tu, wenzako tumepiga kelele tumechoka tumeamua kukaa pembeni tunasubiri kuangalia muvi
 
pole sana kwa kuwa ndani ya sisim kwa miaka 20 unafaaa kupigwa viboko
 
kagoda bado anamawazo yale ya kipindi cha mkapa. aliuza mashirika ya umma na hakukuwa na wakumgusa. kipindi cha JK ni mtoto wamjini yatamkuta kama yalivyowatokewa wenzake na wala hatahangaika kumbeba. mwacheni aendelee na ujinga wake.
 
Hivi karibuni kwenye vyombo vya habari tumekuwa tukisoma vituko ambavyo kwa kweli naviita ni vya kijinga au kitoto kuhusu waziri wa viwanda na biashara Abdalah Kigoda na sakata la TBS, shirika ambalo ni nyeti sana.
Ni huyu huyu Kigoda alieuza nyumba zetu za serikali wakati wa serikali ya mkapa.
Mie najiuliza hivi ni kwa nini Kigoda anafanya mambo haya bila kuwa na aiubu wala kuogopa lolote?
Mie ni mwanachama wa ccm kwa zaidi ya miaka 20 sasa lakini nakatishwa tamaa na vitendo vya mawaziri wabovu kama hawa.
Inakuwaje huyu kigoda alazimishe kampuni iliyofungiwa kwa utendaji mbovu ipewe tenda ya ukaguzi wa magari wakati TBS wenyewe wamesema haifai? NINI MAANA YA VIWANGO?
Kuna mawaziri wanaopiga kazi vizri sana kama mwakyembe na magufuli lakini Kigoda naona ni kama kituko tu na sijui kwa nini kikwete alimpa nafasi hii nyeti. sasa kulikuwa na maana gani ya kumuondoa Chami? basi chami alionewa.
Kwa nini kigoda anawafanya watanzania wapumbavu?
Umepewa rushwa kiasi gani mpaka uwadharau watendaji wote wa TBS?
Sisi wafanyakazi wa TBS hatutakubali, na tunakuambia kuwa tutaumbua madudu yote yaliyofanywa na hiyo kampuni ya WTM unayolazimishwa ipewe tenda wakati bado hata hela walizokuwa wakifanya ukaguzi kwa miaka mitano iliyopita hawajazifikisha hapa TBS.
Leo unaandikwa magazetini lakini ujue iko siku nguvu ya umma itakuhukumu.
YANA MWISHO HAYA

Haangushwi, si kamteua mwenyewe kajiangusha mwenyewe, ni dhaifu huyu. Namuheshimu kwa vile ni rais basi.
 
Haangushwi, si kamteua mwenyewe kajiangusha mwenyewe, ni dhaifu huyu. Namuheshimu kwa vile ni rais basi.
Hapo unakuwa umekosea.
Hawa mawaziri wabovu wengi ndio wanaomuharibia jina Rais wetu.
Mbona mwakyembe akifanya mazuri hamumsifii Kikwete lakini kigoda akifanya madudu mnamsema Kikwete
 
Hata kama KIGODA hafai hiyo haikidhi matakwa yako kwamba CHAMI angabaki japo alikutwa na makosa.

Wakati wa uuzaji wa nyumba waziri wa Ujenzi hakuwa KIGODA alikuwa magufuli. Au ulikuwa na maana nyingine?
 
Hapo unakuwa umekosea.
Hawa mawaziri wabovu wengi ndio wanaomuharibia jina Rais wetu.
Mbona mwakyembe akifanya mazuri hamumsifii Kikwete lakini kigoda akifanya madudu mnamsema Kikwete

Pana utamu hapo kwenye red !!!!!!!!!!!
 
Haangushwi, si kamteua mwenyewe kajiangusha mwenyewe, ni dhaifu huyu. Namuheshimu kwa vile ni rais basi.

Matumizi ya sigara ni hatari kwa afya yako.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Inasikitisha kuona kwamba watendaji wengi katika ngazi mbalimbali serikalini wamekosa maadili mema ya kazi mpaka pale mtu fulani mwenye madaraka na uchungu na matokeo mabaya ya watendaji hawa anapoamua kukemea maovu yao ili angalau warudi katika kufanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi.

Katika uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho vya uraia kwa raia na wageni hapa nchini, Februari 6,2013, Mheshimiwa rais Dr.Jakaya Kikwete, alitahadharisha na kusisitiza kwa mamlaka husika kuwa makini katika kutoa vitambulisho hivyo na kutovitoa kama njugu kama zinavyotolewa pasipoti za kusafiria.

Hii inaonyesha wazi kabisa kuwa Mheshimiwa rais Dr.Kikwete anajua jinsi watendaji wake wanavyomwangusha katika utendaji wa kazi. Aliyoyasema Mheshimiwa Dr.Kikwete ndiyo yanayotokea pale wizara ya mambo ya ndani! Bila woga tena nje na ndani ya wizara, biashara ya kupata na kufuatilia pasipoti inafanyika bila woga wowote ule! Kupeana pesa ndani ya bahasha na kuuziana fomu za maombi ya kupata pasipoti si kitu cha kushangaza na wala si kigeni kufanywa na watendaji kwa waomba pasipoti!

Ada ya pasipoti kubwa ni shilingi elfu hamsini za kitanzania (50,000/-) na inatakiwa ilipwe benki na mwombaji katika akaunti husika imeonyeshwa katika tangazo lililoandikwa gazetini siku za nyuma kwa maandishi madogo na kipande chake kidogo kukatwa na kisha kubandikwa ubaoni pale ofisi za uhamiaji wizara ya mambo ya ndani. Lakini ili kupata pasipoti hiyo, waombaji wamekuwa wakihonga shilingi laki moja na nusu mpaka laki mbili (150,000-200,000/-) ili waweze kupata pasipoti hizo. Wakati mwingine husingizia kuwa malighafi za kutengenzea pasipoti zimekwisha mpaka zitakapoletwa toka nje au kuna kazi maalumu kwa ajili ya wanajeshi wanaotakiwa kwenda nje!

Baada ya Mheshimiwa Rais Dr.Kikwete kukemea utoaji wa pasipoti kama njugu, sasa hivi baadhi ya watendaji katika wizara ya uhamiaji pale wizara ya mambo ya ndani wanasisitiza mwombaji awe na viambatanisho vyote vinavyotakiwa katika kupata pasipoti kama vile cheti cha kuzaliwa (Birth Certificate), barua ya maombi ya pasipoti, barua ya mtendaji na hati ya kiapo (Affidavit).

Nasisitiza kusema Mheshimiwa Rais Dr.Kikwete anawapenda watu wake kwa kukemea maovu, lakini baadhi ya watendaji walio katika idara mbalimbali ikiwemo idara ya uhamiaji ambayo ni nyeti sana katika usalama wa nchi, wanamwangusha.

Kama mwombaji hana cheti cha kuzaliwa (Birth Certificate), barua ya maombi ya pasipoti, barua ya mtendaji na hati ya kiapo (Affidavit), hivyo vyote vinaweza kupatikana pale nje tu ya wizara ya mambo ya ndani. Kuna ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wa wizara ya uhamiaji na watendaji wa RITA katika kutoa na kupata vyeti vya kuzaliwa vya chapuchapu kwa kutoa rushwa ya kati ya shilingi elfu hamsini na elfu sabini (50,000-70,000/-). Ada halali ya kupata cheti cha kuzaliwa ni shilingi elfu kumi (10,000/-). Biashara hufanyika kwa njia ya simu za mkononi kwa kutumiana majina ya waombaji wasio na vyeti vya kuzaliwa au kwa mtu wa upande mmoja kwenda katika ofisi husika.

Nje ya ofisi za wizara ya mambo ya ndani kuna maduka yanauza vifaa vya kuandikia na kuchapa (Stationary), hapo ndipo kunapotengenezwa na kuchapwa barua za maombi ya pasipoti, hati za viapo (Affidavit) na barua za watendaji. Inachoshangaza haya yote yanafanyika nje ya makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani! Mihuri ya watendaji wa kata wa Dar ES salaam nzima inapatikana hapo!

Watanzania wote tukiongozwa na Mheshimiwa Rais Dr. Jakaya Kikwete, tunatakiwa kuwa na upendo na nchi yetu kwa kukemea na kufichua utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji husika katika ngazi mbalimbali serikalini. Mafanikio ya nchi yetu yataletwa na sisi wenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii na kufuata maadili ya kazi.

Rushwa ni adui wa HAKI.
 
Acha wee. Umetumwa? Si anawaweka mwenyewe na kuwadumisha pale. Vipi wewe unaonaje yeye asione.
 
Acha wee. Umetumwa? Si anawaweka mwenyewe na kuwadumisha pale. Vipi wewe unaonaje yeye asione.

Sijatumwa na mtu lakini baada ya kuvurugwa sana pale uhamiaji wizara ya mambo ndani,nikaona ni vyema na haki nikikujuza wewe na wengine wote wanaohusika ili labda kama itawezekana hatua madhubuti na za haraka zikachukuliwa dhidi ya mambo yanayofanyika RITA na ndani ya ofisi za uhamiaji na nje pale wizara ya mambo ya ndani!
 
inakuza gap kwa walicho nacho na wasionacho.

Takwimu zinaonyesha walionacho wanaendelea kuwa nacho eti kwa sababu inasemekana aliye nacho hubarikiwa na kuongezewa! Idadi ya wasio nacho inazidi kuongezeka mpaka hapo walionacho watakapoacha kutuvuruga tusiokuwa nacho!
 
Ndio ada za kusomesha watt zao wanapatia humo
 
Kuna baadhi ya watu wamezoea kutumia usemi wa kijinga kabisa, kwa watu wenye akili timamu huwa tunawashangaa. Kuna watu katika kijadala mbalimbali, hata Bungeni utasikia wanasema. ''Rais wetu anaangushwa na watendaji wake, lakini yeye ni hana tatizo". Au wengine utasikia wanasema, "tatizo sio CCM, tatizo ni watu".

Usemi huu ni wa kitoto sana. Hivi inakuwaje Rais ambae umekabidhiwa mamlaka yote ukaangushwa na watendaji wako ambao una uwezo wa kuwafukuza kazi na kuwapeleka Mahakamani?, nini maana ya kuwa na mkuu wa nchi kama watu wa chini yake wanaweza kumkalia kichwani?.

Watanzania wenzangu ebu tuache fikra za kitoto, kiongozi wa juu akiwa dhaifu ni dhahili kwamba watu wa chini yake watamchezea. Hata katika kampuni ukiwa ni mtu wa kuchekea wafanyakazi wako, watafirisi kampuni yako kweupe. Kama kweli watendaji wanaweza kumuangusha Rais kiutekelezaji wa shughuli za maendeleo, ebu kamuanguishe Rais wa China uone shughuli yake!, kafanye uzembe kwa Obama uone nini kitakutokea!. Enzi za Nyerere watendaji wa chini yake wangemchezea?. Ebu tuache hii tabia ya kijinga ya kumtetea Rais kwa kwa sababu nyepesi. RAIS IMARA HACHEZEWI
 
Kuna baadhi ya watu wamezoea kutumia usemi wa kijinga kabisa, kwa watu wenye akili timamu huwa tunawashangaa. Kuna watu katika kijadala mbalimbali, hata Bungeni utasikia wanamema. ''Rais wetu anaangushwa na watendaji wake, lakini yeye ni hana tatizo". Au wengine utasikia wanasema, "tatizo sio CCM, tatizo ni wanachama wake".

Usemi huu ni wa kitoto sana. Hivi inakuwaje Rais ambae umekabidhiwa mamlaka yote ukaangushwa na watendaji wako ambao una uwezo wa kuwafukuza kazi na kuwapeleka Mahakamani?, nini maana ya kuwa na mkuu wa nchi kama watu wa chini yake wanaweza kumkalia kichwani?. Watanzania wenzangu ebu tuache fikra za kitoto, kongozi wa juu akiwa dhaifu ni dhahili kwamba watu wa chini yeke watamchezea. Hata katika kampuni ukiwa ni mtu wa kuchekea wafanyakazi wako, watafirisi kampuni yako kweupe. Kama kweli watendaji wanaweza kumuangusha Rais kiutekelezaji wa shughuli za maendeleo, ebu kamuanguishe Rais wa China uone shughuli yake!, kafanye uzembe kwa Obama uone nini kitakutokea!. Enzi za Nyerere watendaji wa chini yake wangemchezea?. Ebu tuache hii tabia ya kijinga ya kumtetea Rais kwa kwa sababu nyepesi. RAIS IMARA HACHEZEWI

Kila msiba, rafiki wa wasanii, safari kibao, wakuu wa wilaya manesi, darasa la saba etc!
 
Back
Top Bottom