Kikwete Oyeee, Madaktari Oyeee

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,910
Sina haja ya kuwaponda madaktari.

Baada ya Kikwete kuwaaambia waache kazi kama wanaona mshahara hauwatoshi, leo huduma za tiba zimerejea Mahospitalini.

Sina haja ya kusema madaktari ziiiii. Nasema nampongeza Kikwete kwa kuwa mkweli na muwazi na kuweka msimamo wake kisha kukwaa pipa kuelekea kwa jirani mwema Rwanda.

Madaktari na wao nawapa hongera kwani wameona kuwa walikuwa wanafanya makosa na hakuna faida kwao, wala kwa taifa, wala kwa wagonjwa.

Haya yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
 
Mkuu zombe umetumia busara sana, lakini kiukweli kauli ya JK ilikuwa inatisha. Madaktari wana haki ya kuachakazi na kutafuta mwajiri atakayewalipa 3.5 Milion.

Leo katibu wa madaktari anaongea kama ANALIA Mpoleeeee.

Kweli JK kamanda wa ukweli.
 
Kwa vyovyote utakuwa umeangalia taarifa ya habari ya TBC,
maana ndiyo waliotangaza kuwa huduma zimerudi kama kawaida
na hawakutaka kugusia suala la mgomo wa madaktari bingwa...
 
..baadaye watagoma tena.

..JK atakwenda kwa wazee wa DSM na kuwaponda.

..halafu atakwaa pipa kwenda kwa jirani mwema mwingine.

..kinachotakiwa ni muafaka wa kudumu na siyo kutishana-tishana.
 
..baadaye watagoma tena.

..JK atakwenda kwa wazee wa DSM na kuwaponda.

..halafu atakwaa pipa kwenda kwa jirani mwema mwingine.

..kinachotakiwa ni muafaka wa kudumu na siyo kutishana-tishana.

Soma post #2
 
Huduma zimerejea hosp gn wakati Specialists wameanza mgomo leo?
TBC ni janga la kitaifa!
 
Huduma zimerejea hosp gn wakati Specialists wameanza mgomo leo?
TBC ni janga la kitaifa!

Hao hawana mshiko, ni vijana wetu, kesho tu utaona na wao wanarudi, usiwe na shaka.

Zimerejea Hospitali zote.
 
Mimi sitaki kutibiwa na Daktari aliyejeruhiwa ambaye atasema Liwalo na Liwe , Serikali umeshinda lakini nachelea kusema yanayotokea kwenye elimu yataanza kutokea hospitalini , maana hawa jamaa wameomba kuboreshewa mazingara ya kazi wananchi wanaotibiwa wamewageuka, sasa Liwalo na Liwe ni kilio na kusaga meno , hospital za serikali ni janga la kitafa nionavyo
 
Hahahahaaaaaaa, nimeanza kupata shaka kuwa wewe ni mkurugenzi
wa mawasiliano Ikulu...

Madaktari bingwa wengi Tanzania ni watu makini, hata wakigoma mkikaa meza moja mkaongea mnaelewana, lakini si hivi vitoto vinavyotafuta cv, vikishakuwa na title ya "doctor" basi, ndio havioni havisikii mpaka vivutwe masikio, wakikuwa wataacha.
 
hakuna cha maana ulichoongea zaidi ya USENGErema tu , wewe na mr dhaifu wako , na baada ya wiki 2 walimu wataingia kwenye mgomo , hii nchi haitawaliki am telling you, mr dhaifu must resign
 
Ama kweli nchi imewashinda .mgomo unaendelea nyie mnaleta porojo hapa .kamalizaneni na madakitari acheni uzushi usio na msingi.
 
Madaktari bingwa wengi Tanzania ni watu makini, hata wakigoma mkikaa meza moja mkaongea mnaelewana, lakini si hivi vitoto vinavyotafuta cv, vikishakuwa na title ya "doctor" basi, ndio havioni havisikii mpaka vivutwe masikio, wakikuwa wataacha.

Kumbe ndio maana mkaamua kumvuta kucha na kumng'oa meno Dr Ulimboka kwa kuwa ni kijana na sasa mna mpaango wa kumnyofoa kucha nani eehh? Eti nyie majambazi
 
Kumbe ndio maana mkaamua kumvuta kucha na kumng'oa meno Dr Ulimboka kwa kuwa ni kijana na sasa mna mpaango wa kumnyofoa kucha nani eehh? Eti nyie majambazi

Hapana, sisi tunawavuta masikio tu, kama alivyofanya Kikwete juzi.
 
Mkuu zomba hata mimi nimefurahia uamuzi wa serikali na uamuzi wa madaktari kurejea kazini. Kiukweli maslahi ni mabovu kwa wafanyakazi karibu wote wa serikali, si kwa madaktari peke yao au walimu!
 
Mkuu zomba hata mimi nimefurahia uamuzi wa serikali na uamuzi wa madaktari kurejea kazini. Kiukweli maslahi ni mabovu kwa wafanyakazi karibu wote wa serikali, si kwa madaktari peke yao au walimu!

Kweli kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom