Elections 2010 Kikwete on ITV, maswali na majibu toka kwake

Kama una akili sawasawa utagundua ni maongezi yaliyoandaliwa kwani hata aliyozungumza asubuhi karudia vile vile jamani tunaelekea wapi watz??!???!
KAzI kWEnU...........
 
Kwa kweli jamaa ameboa,yani kimsingi huu mdahalo wake haukuwa participatory,waliohudhuria sio watu wa wa kariba mbalimbali bali ni watu waliochujwa,yani ningejua nisinge angalia kabisa hiki kituko.jamaa kashindwa kusema tumkumbuke kwa nini.
 
Kicheko cha JK funzo la uvumilivu!




Hakika vichekesho na vicheko vinahitajika sana katika jamii. Huleta furaha na faraja. Pia hupunguza makali na masaibu ya maisha.

Hata wanasaikolojia wamedhihirisha kuwa hali ya kufurahishwa hutusaidia tuwe na mzunguko mzuri wa damu. Pia husaidia kuzalisha chachu ya kuchochea bongo zetu. Hali hii hutufanya tuweze kuwa wepesi wa kufikiri, kukumbuka na kutenda.

Hali kadhalika misahafu mbalimbali husisitiza umuhimu wa kufurahi na kufurahishana. Kwa mfano msahafu wa Kikristo unanena waziwazi kuwa "moyo uliochangamka ni dawa nzuri; bali roho iliyopondeka huikausha mifupa." Pia unatuhimiza tuwape cha kuwafurahisha wale walio na uchungu nafsini ili wausahau umaskini wao na taabu yao.

Hivyo, basi, hatuna budi kumshukuru Jalia kwa kutupatia Rais mwenye uwezo wa kucheka na kutuchekesha. Naam si viongozi wetu wa dini wametuhakikishia kuwa Rais wetu ni chagua la Mungu. Tena na msahafu mmojawapo unasisitiza kuwa kila mamlaka hutoka kwa Maulana.

Hotuba ya Rais aliyoitoa Bungeni hivi karibuni imezua mjadala mkali. Wapo waliokerwa sana na kile ambacho Rais alikisema au kutokisema. Hawa hawakucheka hata kidogo wakati wote wa hotuba. Pia wapo waliofurahishwa sana. Hawa wamelazimika kuandamana kumpongeza Rais.

Hapo katikati tupo tuliocheka huku tunalia. Sisi ndio wale ambao ule msahafu unatusema kuwa hata " wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo." Hisia zetu ni tete tena ni tata. Ni vigumu kwetu kucheka bila kulia hata tunapotazama Ze Komedi.

Hulka na haiba ya Rais wetu hakika imefanya awe na umaarufu wa ajabu. Umaarufu wake umefanya watu wambatize majina kedekede, likiwamo la JK. Yeye mwenyewe, kwa utani uliotuchekesha wenye vicheko vilivyo karibu, ameongeza orodha ya majina yake pale aliposema ‘Mabilioni ya Bwana Fulani', akimaanisha ‘Mabilioni ya JK', wakati wa hotuba yake.

Hapa alikuwa anaongelea zile fedha – ama tuziite vijisenti – ambazo zinatolewa kwa kila mkoa kwa ajili ya kuwawezesha wakazi wa mikoa hiyo. Ilibidi Bwana Fulani atenge dakika kadhaa kutoka kwenye takribani dakika 180 za hotuba yake ili azungumzie fedha hizi ambazo zimekuwa gumzo hasa miongoni mwa wale wanaoamini kuwa vifisadi vimezigeuza kuwa vijisenti vyao.

Huyu ndiye Rais tuliye naye. Ni Rais mwenye ujasiri wa kutuchekesha kuhusu masuala mazito yanayoikabili nchi yetu ili kutupunguzia mzigo tulio nao. ‘Usione majentlomeni wametinga tai mtaani hali yao ngumu' na ‘liwa ule' ni ‘sharbati' aliyotuonjesha ili kutuliza kiu yetu ya haki.

Hasira hasara. Ndivyo walivyonena wahenga. Naye Rais ametilia sana maanani wosia huu tena kama ulivyo. Ndio maana amesisitiza kuwa ‘tukienda kichwakichwa' na kuwakamata mafisadi (au ni watuhumiwa tu?) basi Serikali inaweza kuishia kupelekwa mahakamani na kupoteza mamilioni ya fedha. Hasira za mkizi furaha ya mvuvi. Je, hasira za mvuvi furaha ya mkizi?

Huko zamani tuliambiwa Serikali inakwenda hatua kwa hatua. Hata leo bado Serikali inakwenda hatua kwa hatua. Kwetu sisi wenye ‘haraka kuliko upesi' ni vigumu sana kuwa wavumilivu.

Hebu tutafakari upya ombi alilolitoa JK ‘Tanga Kunani Pale!' Alituomba tuwe wavumilivu tunapopitia wakati huu mgumu. Lakini uvumilivu hauji hivi hivi tu. Ndio maana vichekesho vya Rais vinajaribu kutuwezesha sisi wananchi tucheke na hivyo kuvumilia ugumu wa wakati huu.

Huu ni wakati ambapo kuna upungufu mkubwa wa chakula duniani. Ni wakati wa bei ya mafuta kupanda hovyo. Naam ni wakati ambapo hata Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (Mkukuta) unakiri kuwa wananchi wengi wanaona kuwa hali yao ni mbaya kuliko Mkukuta ulipoanza 2005 – mwaka wa ule uliokuwa utatu mpya! ‘Choka mbaya' au sio?

Hizi ni zama za ujasiri wa kifisadi. Lakini hizi pia ni zama za ubwege wa kifisadi. Ni zama ambazo hata kicheko cha fisi mla mizoga kinaweza kumtetemesha simba mla nyama mpaka atapike mzoga. Naam ni zama za kuucheka ufisadi na si kuwachekelea mafisadi.

Hatuna budi kukaza mikanda yetu. Kweli tumelizwa sana na mafisadi. Tukiendelea kulia na kulalama tu hatutaweza kufanya lolote. Tuungane na JK kuchekesha, kucheka na kujichekesha.

Heko JK! Hakika vichekesho vyako vinatufunza mengi. Inahitaji uvumilivu kujicheka. Hahaa!

-------------------
 
Sawa sawa walivyoonyesha channel zote maana kaamua kujimaliza kabisa kampeni haikutosha kummaliza. Wacha hata ulaya marikani na mbingu zote saba wamsikie namna akili inavokosa akili. Hivi ccm wanafikiri bado wanadeal na watu ambao hajaenda shule wanafikiri bado tupo kwenye wakati wa elimu ya watu wazima hawajui watu wameshapata exposure wanafahamu mbichi na mbivu.. JK umeliwa waliokuambia uingie kwenye mdahalo mwenyewe afadhali ungekubali kufanya mdahalo na Dr. Slaa (msomi wa kweli) ungechota some ideas katika kujibu maswali. Eti kutuhumiwa sio hatia hivi una maana mahakama unaituhumu kuwa haijui kazi kwa nini hawa watu kesi zao hazijafutwa huko mahakamani??? CCM IWE NI MWAKA HUU AU MIAKA 20 IJAYO MTAPANDA KWENYE KITI CHA PILATO TU MSIDHANI MTAISHI HIVI MILELE YOTE SIKU INAKUJA TENA INAKUJA KAMA MWIZI.
 
Una maoni gani ya mwisho kuwaambia watanzania wanaokusikiliza "watu waheshimu matokeo fulsa ya kuiba ni ndogo sana ila mpaka uwe na maarifa makubwa sana kuweza kuiba". Dr. Kikwete.
 
magi hana zaiodi ya kampuni ya kushusha mizigo tu...!
fataki: gwiji, kwa hiyo mtei ndo awalipe?
bk: tics ta nani
Nnyamwakaleli: huyu gwiji anabwata tu
gwiji: alikula hela akiwa kiongozi wa eac..,au hujui tukupe habari
gwiji: mbona unajidanganya hali ya kuwa unatamani kufahamu ukweli...?
Nnyamwakaleli: kwa hiyo kikwete na serikali yake hawajui habari za mtei kula pesa za ea
fataki: facts si muhimu, la muhimu ni kwa nn asichukuliwe hatua hao wazee wakalipwa
bk: chakachua mwenyewe
fataki: mwenye dhamana ni mtei au serikali?
bk: tafakari-chukua hatua
Nnyamwakaleli: gwiji uwezo wako wa shule
bk: true------udini ni hatari
bk: hapo i concur na jk
fataki: nakubari udini ni hatari, wauepuke sana
gwiji: facts ni muhimu na ndizo tunazozizingatia..,kama unabisha subiri utakuja kufahamu kuwa wazee wale wa eac walibakizwa vibarua chini ya mtei kama katibu mkuu.
fataki: kipindi kimeisha, nothing new, upouuzi tu
bk: can someone summarize ?
bk: hahaaa
gwiji: if at all u were attentive...?
Nnyamwakaleli: soga tu zilikuwa nying
bk: hahahaa
Nnyamwakaleli: hahaaaa labda makamba
Nnyamwakaleli: asamalize
gwiji: na ktk wale wazee wa eac..,wachaga ni wachache sana kwa nini..,haujiulizi...?
bk: Mungu ibariki Tanzania
msomi: jamani mi natoka, naenda jenga nchi yangu
fataki: hawa watu wanafanya msaha tu
bk: nani huyo anaongelea makabila
Nnyamwakaleli: ernesto sheka a.k.a gwiji]
bk: stupid
gwiji: kuna wakati lazima mufahamu nani anania gani na amejipangavipi..,unaweza kutumika bila kujitambua...!
Nnyamwakaleli: who told you?
msomi: hivi hii habaricom ni ya Makenya?
fataki: gwiji, sidhani we ni mtz
gwiji: I told u...!
Nnyamwakaleli: basi wewe unatumika kwa maslahi ya tumbo lako
gwiji: lakini haimaanishi kuwa siguswi na yale yanayotokea tz
Nnyamwakaleli: tutajuaje kama unaguswa
fataki: inaonekana unachekelea, giwji
Nnyamwakaleli: usitupake mafuta kwa kifuu cha nazi
Nnyamwakaleli: wewe hayo kwako ni raha
gwiji: ikiwa unaufahamu wa sawasawa basi utakubaliana na mimi kuwa ahadi ya kiongozi ya jana ni kodi yako ya leo...!
gwiji: nikimaanisha hakuna bure...!
Nnyamwakaleli: sawa na ahadi ya jk ya leo ni kilo cha kesho
gwiji: udini..,ukabila kamwe haviwezi kuwa silaha ya kuingilia ikulu.
Nnyamwakaleli: kwani kuna mtu hataku kulikpa kodi?
Nnyamwakaleli: sasa kikwete ni mdini no 1
Nnyamwakaleli: anatumia msikiti kupiga kampeni na magazeti ya alnuur kwaandika vibaya washindani wake
gwiji: tunaposema kuwa serikali ya jk imejenga shule..,tunakili kuwa ni kwa nguvu za wananchi wenyewe..,nani asemaye atajenga shule na atalipia kila kitu na mwisho everything is for free...?
Nnyamwakaleli: akili kichwani mwako anamaanisha tukijenga kwa kodi zetu watoto watasoma bure
Nnyamwakaleli: mbona yeye kikwete alisoma bure
Nnyamwakaleli: baada ya mwalimu kuongoza ujenzi wa shule kwa nguvu za wananchi?
gwiji: kama watu wanasema yale yaliyofanywa na jk kiuhalisia basi hawataona dalili za udini hata kwa kulazimisha
Nnyamwakaleli: we unataka kuuona udini kama figure ama?
Nnyamwakaleli: mbona na sasa upo wa kumwaga
gwiji: wakati huo wanafunzi walikuwa wangapi..,shule ngapi na serikali ilikuwa na mzigo kiasi gani...?
Nnyamwakaleli: kwa hiyo uinataka kuniambia sasa serikali ina mzigo mkubwa?
Nnyamwakaleli: kutoka wapi
Nnyamwakaleli: walipa kodi nao ni wengi
gwiji: yapo magazeti yameandika kwa statistics kila wizara na nafasi ya kazi na asilimia kati ya waislamu na wakristu...!
Nnyamwakaleli: lakini ukiwa na akili
Nnyamwakaleli: ukristu siyo majina
Nnyamwakaleli: kwa taarifa yako
msomi: huyo dada nimemzimika
msomi: wa katikati
msomi: mwenye kipedo cheusi
Nnyamwakaleli: hahaaaa wewe
 
Jafar mimi nitakuwa tofauti kidogo na wewe, kwanza thanks kwa kutoa elaboration nzuri sana..ila first question was real good, according to what i understood from the person aliyeuliza swali...it was like this " Umefanya kampeni nchi nzima, karibu kila eneo" Hebu tupe hali unanionaje......muulizaji hapa alimaanisha" hali ya maisha ya watu, maendeleo yao, hatua gani serikali yake inachukua katka kuondoa hayo mapungufu yaliyobaki (Kama watakuwa wamefanya part). Bahati mbaya the so called mgombea hata hakuelewa.......the same to Kibonde, swali lilionekana gumu pamoja na kwamba alikuwa ameshaandaliwa majibu....kichwa cha panzi.....
 
Kikwete ameshindwa kumjibu Kibonde kuhusu 'sura' ya serikali yake. Hapa hata kama hujaenda shule na kusoma 'political science' kikwete 'atakapoingia' tena kwa awamu nyingine atatengeza mhimili 1 tu wa serikali ambao ni utawala 'executive. Ameshindwa kusema idadi ya wizara na Mawazi. Kumbukeni ni lala salama yake,anaenda 'kushukuru washkaji wake'. Kuna hatari ya kuundwa wizara 40 ili akina 'SOPHIA SIMBA' WAPATE ULAJI. Twafaaaaa...!
 
Safi sana, ndio CCM wenzake sasa watampa kura Slaa maana wameona jamaa ya hoyi kabisa.
 
Siku zote hizo alikuwa anajitungia maswali ya kuulizwa. leo ndio kaibuka, kweli kiboko sasa kasema anataka mwalimu mmoja afundishe wanafunzi wengi kwa wakati mmoja kupitia fibre optic cable umeme anao?

kasema serikali ina mpango wa kufundisha walimu wengi zaidi ili kuinua kiwango cha elimu, wachache waliopo sasa wanampa tabu kuwalipa.

eti pia wana mpango wa kutoa huduma za afya kwa e-medicine yaani daktari akiwa marekani anaelekeza mtu anapasuliwa tanzania, wale jamaa wa muhimbili waliopasuliwa vichwa badala ya miguu walikuwa wanapata maelekezo wakiwa na mtaalam hapohapo, hivi wakiwa wanapokea maelekezo kutoka unyamwezini kupitia screen tutapona kwel,i si watatukata shingo kabisa?


duh nimecheka mpaka basi.
 
Kweli popo ni ndege, aah sory ni mnyama, yes ndioooo! Hivi ulikuwa mdahalo au kikao cha wajumbe wa kamati kuu na chama cha waandishi wa ccm au story za babu, au kujisifia kwenda kuchai ulaya. Duh sielewi! Mungu nisaidie nikiamka asubuhi aliyoyasema yule bwana yafutike nipambazuke na mawazo mapya taree 31. Amen
 
Jafar mimi nitakuwa tofauti kidogo na wewe, kwanza thanks kwa kutoa elaboration nzuri sana..ila first question was real good, according to what i understood from the person aliyeuliza swali...it was like this " Umefanya kampeni nchi nzima, karibu kila eneo" Hebu tupe hali unanionaje......muulizaji hapa alimaanisha" hali ya maisha ya watu, maendeleo yao, hatua gani serikali yake inachukua katka kuondoa hayo mapungufu yaliyobaki (Kama watakuwa wamefanya part). Bahati mbaya the so called mgombea hata hakuelewa.......the same to Kibonde, swali lilionekana gumu pamoja na kwamba alikuwa ameshaandaliwa majibu....kichwa cha panzi.....

Mi nakubali asilimia kubwa ya maswali yalikua mazuri tu na yanayojikita kwenye dira ya maendeleo ukiacha machache ya kipuuzi. Kilichofanya maswali yaonekane kama bomu ni mjibu maswali, the so called 4th president, yaliyokuwa ovyoo hadi wauliza maswali wanashangaa wenyewe japo waliandikiwa hayo maswali. I said from the beginning kuwa hakuna jipya kwa JK wala Lipumba, Dr. Slaa alishamaliza kila kitu na mbaya wasikilizaji waliweka Dr. Slaa as a reference point. Kwa kushindwa kwao kumfunika wamejichimbia kaburi la kisiasa wao wenyewe.

God bless Dr. Slaa
 
This guy ni bonge la mbumbumbu wa hatari...kachota idea ya wamarekeani waishio marekani last week walikuwa wakihojiwa.....nae kabeba kama ilivyo bila kuzingatia mazingira gani tuliyomo.....kweli hii aibu ya mwaka. If and only if the guy becomes a presda through uchakachuaji au any other means....basi dunia yote itaamini kile alichoambiwa baba wa taifa na Mzee Jomo Kenyata juu ya watu anaowaongoza. Presda akiwa na akili za hivyo, what about citizens wake.....Kama alivyo baba basi hata waishio humo hufanana nae.
 
Back
Top Bottom