Kikwete: Nani hao akina "na mimi mwenzenu"?

Kikwete: Nani hao akina "na mimi mwenzenu"?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
753
Reaction score
1,261
Leo, June 21, 2025, JNICC katika kongamano la sheria kuelekea uchaguzi mkuu, lililoandaliwa na Chama cha mawakili wa serikali, Mh. Jakaya kikwete, amesimulia kisa cha kufikirisha sana.

Kwakifupi sana; kisa hiki ni cha mlevi wa gongo, kuzamia kikao cha kahawa, na kujitambulisha "na mm mwenzenu" akidhani kikao kile kilikuwa cha walevi wa gongo. Wanywaji wa kahawa wakamtimua.

Kisa hiki kimenikumbusha maneno ya Mh. Rais Samia, May 31, 2025, katika mkutano mkuu wa CCM, kuwa "mcheza ngoma si yake ataharibu" akitoa wito wa kukitenga chama na magwajima, hivyo aliwataka wana CCM kuwakataa majuzuhu. June 1, 2025, Bishop Gwajima, akiwa kanisani kwake, alijibu mashambulizi aliyoelekezewa kwa kusema "CCM mm ni hazina yenu"

Katika theology, kuna kanuni ya kutafsiri maandiko ya Biblia inaitwa Hebrew parallelism. Katika kanuni hii aya moja, iliyoandikwa kwa lugha moja, hufuatiwa kwa aya yenye lugha tofauti, kusisitiza maana ya kwanza.

Kwakutumia kanuni hii, Je, "Na mimi mwenzenu" wa kisa cha mlevi wa gongo aliyevamia kikao cha kahawa, siye Juzuhu wa kisa cha "mcheza ngoma si yake ataharibu"?
 
Leo, June 21, 2025, JNICC katika kongamano la sheria kuelekea uchaguzi mkuu, lililoandaliwa na Chama cha mawakili wa serikali, Mh. Jakaya kikwete, amesimulia kisa cha kufikirisha sana.

Kwakifupi sana; kisa hiki ni cha mlevi wa gongo, kuzamia kikao cha kahawa, na kujitambulisha "na mm mwenzenu" akidhani kikao kile kilikuwa cha walevi wa gongo. Wanywaji wa kahawa wakamfukuza.

Kisa hiki kimenikumbusha maneno ya Mh. Rais Samia, May 31, 2025, katika mkutano mkuu wa CCM, kuwa "mcheza ngoma si yake ataharibu" akitoa wito wa kukitenga chama na magwajima, hivyo aliwataka wana CCM kuwakataa majuzuhu.

Katika theology, kuna kanuni ya kutafsiri maandiko ya Biblia inaitwa Hebrew parallelism. Katika kanuni hii aya moja, iliyoandikwa kwa lugha moja, hufuatiwa kwa aya yenye lugha tofauti, kusisitiza maana ya kwanza.

Kwakutumia kanuni hii, Je, "Na mie mwenzenu" wa kisa cha mlevi wa gongo aliyevamia kikao cha kahawa, siye Juzuhu wa kisa cha "mcheza ngoma si yake ataharibu"?
Huyu mbona kama ni yule
 
Back
Top Bottom