Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
Nilidhani nimechanganyikwa, sasa nina uhakika nimechanganyikiwa, yaani kuchunguza kamati iliyochunguza uchunguzi wa kile kilichochunguzwa?
Hii inanikumbusha ila kamati ya madini imbayo inapitia yale yaliyochunguzwa na kamati ya Masha na yale yaliyochunguzwa na Mboma ambaye naye alichunguza yaliyochunguzwa na Kilokola na Mangenya.
Sasa katika nchi hii ambao uchunguzi uliochunguzwa nao unachunguzwa basi uwezekano wa kuchunguza kilichochunguzwa huwa ni kawaida na wa daima (perpetual)
Tunakumbuka jinsi Muhimbili walivyochunguza wale wagonjwa wa Muhimbili ambapo baada ya uchunguzi wao ripoti yao ikakataliwa na kumfanya Mwakyusa aunde kamati nyingine ya uchunguzi wa kilichochunguzwa na kamati ya awali.
sasa, kwanini tusiamue kubadili jina la nchi yetu na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Watu Wanaochunguzwa?
Mimi naona at-least awamu ya nne kuna viuchunguzi vinafanywa (BoT), watu wanapelekwa mahakamani (Balozi wa Tanzania Italy, Zombe, Dito), tume zinawaingiza mpaka wapinzani (Madini Zitto).
Awamu ya nyerere, BoT imepakuliwa mpaka ikachomwa moto! Hakuna tume wala uchunguzi wala kufikishwa mtu mahakamani. Lord Rajpar, kauziwa meli ya serikali kwa njia ya mkato, hakuna kilichotokea, kimya.
Awamu ya mwinyi, huyu ndio kila kitu ruksa...hakuna uchunguzi, wala tume, wala mahakamani, kimyaa.
awamu ya nkapa, kaunda tume ya warioba, mpaka leo kaikalia. kafunguwa biashara binafsi ikulu, kimya...
awamu ya nne, si at least tunayaona yanayofanyika..., "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni", au hamuijuwi system ni nini?
Wandugu zangu wa visiwani wana wimbo wao "ukichunguwa usichunguwe utayajuwa", kwa hiyo usiwe na shaka na uchunguzi, mradi mambo yaende na tuyaone, kama tunavyoyaona awamu hii yanavyokwenda. Au hujuwi system ni nini?Ulisikia alichosema juzi Kikwete kuwa anataka kuchunguza wazazi wa wanaJF wanaopenda kulialia kama watoto kila mara? Uko kwenye nchi ya uchunguzi, kinachofuatia, hilo jina unalotumia hapa litachunguzwa kama linafanana na memba fulani hapa alikuwa na tabia ya kulialia kila mara ili apewe maziwa!
Wandugu zangu wa visiwani wana wimbo wao "ukichunguwa usichunguwe utayajuwa", kwa hiyo usiwe na shaka na uchunguzi, mradi mambo yaende na tuyaone, kama tunavyoyaona awamu hii yanavyokwenda. Au hujuwi system ni nini?
Kikwete akatangaza kutengua uteuzi wa Balali na kuipa bodi ya BOT (ambayo ndiyo iliyoshiriki katika wizi wa awali) miezi sita kuchunguza kile kilichochunguzwa na waliochunguza ile kamati iliyochunguza ile kampuni iliyochunguza yale CAG aliyochunguza baada ya kampuni ya uchunguzi kuchunguza uchunguzi wa .....nimechanganyikiwa sasa.
Mwafrika wa Kike,
Hata kama ungekuwa ni wewe, unaweza kukata tawi ulilokalia? Ripoti ya Slaa inamtaja Kikwete kwamba naye ni mchafu kama Balali, sasa amshitaki ili iweje? Aumbuke na yeye?
Ni ngumu sana.
Tumsubiri Balali aje aseme yale mabilioni alikula na nani!
IDIMI,
Kila siku unasikia story huko Asia (esp Japan) za mawaziri kujiuzulu na kuacha madaraka pale inapodhihirika kuwa kuwepo kwao kunahatarisha maisha na uchumi wa mamilioni ya raia wenzao.
Kikwete anaweza kufanya the right thing hapa na kukata mzizi wa fitina na kuwatosa wenzake huku akitumia machine ya uongozi kuzima kila aina ya upizani watakaoanzisha.
Kusubiri Balali aje inaweza kuwa ni ndoto sasa hivi. Kuna uwezekano mdogo kuwa jamaa ataenda bongo. Kikwete pia haonekani hata kama ana mpango wa kumleta Balali ili ashtakiwe.
Kwa sasa mimi narudisha mpira kwa Kikwete. Yeye ana nafasi nzuri sana ya kuomba msamaha kwa MUNGU na kwa wananchi wa Tanzania na akasaidia kuwatosa kina Patel, Mramba, Mgonja, na wenzake ili nchi ikapumua kidogo.
"unanisulubu bila kosa"Consider yourself ignored by Mwafrika wa Kike from now on unless........
Wapinzani mnamtesa sana JK yaani kaja na kila mbinu sasa anagota .Karibia ataamua kukata tawi aanguke chini . JK seriously alikuja kuia CCM na CCM itakufa kwa mwendo huuu.Kama iafi basi JK ajiandae kutoa amri kama Kibaki ya shoot to kill.
Mwafrika wa kike kila kukicha inaonyesha ur not matured enough kua hapa JF.Or Usitake sisi watu wa zamani turejee ktk imani yetu ya zamani kua KINA DADA BADO MUDA WA KUWAPA PLATFORM ZA KUJADILI NA KUTOA MAAMUZI BADO MUENDELEE KUKAA JIKONI NA KULEA WATOTO.Consider yourself ignored by Mwafrika wa Kike from now on unless........