Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,186
- 56
Ukaguzi wa kawaida wa ndani ulifanyika ukagundua kuna tatizo kubwa sana. Deloitte wakafanya ukaguzi wakagundua kuna tatizo kubwa zaidi na walipoanza kupiga kelele wakafukuzwa. CAG nayo ikaingilia ikakuta tatizo ni kubwa zaidi. Wenye uchungu wakaanza kuvujisha mambo kwa wapinzani na Jamboforums.
Habari zikaenea kwa haraka sana kuwa kuna watu wachache wanafilisi nchi. Lipumba akaongea na waandishi wa habari lakini ccm wakapuuza maneno yake. Dr Slaa akataka kuwasilisha hoja bungeni lakini Spika akasema ni uzushi. Dr Slaa akasisitiza tena kuleta hoja bungeni, usalama wa taifa ukaandika barua kali ya onyo kwa Lowasa kuwa asimruhusu mbunge hata mmoja wa ccm kuijadili hoja ya Slaa- wabunge wa sisiem wote wakanywea.
Mwenye uchungu na nchi akavujisha barua ya usalama wa taifa (TISS) kwa Lowasa hapa JF na kwa wapinzani. Serikali ikashindwa kukana au kuikubali hiyo barua. Katika kipindi hicho hicho Zitto akaleta hoja binafsi kuhusu Buzwagi. Wabunge wa ccm chini ya Lowasa na Malecela wakamfukuza Zitto bungeni. Spika akaonya kuwa yeyote anayeleta hoja bungeni za kuipaka serikali matope kwa "maneno ya kizushi na uongo" ataadhibiwa na bunge.
Dr Slaa akatoa hoja yake bungeni na akaipa serikali muda hadi sep 15 kufanya uchunguzi wa wizi mkubwa kabisa benki kuu lakini serikali chini ya kikwete ikapuuzia. Dr Slaa akaishtaki serikali kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara. Zitto naye akaendelea kuishtaki serikali kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara. Wananchi wa Tanzania kwa mara ya kwanza kabisa wakaanza kuzomea viongozi wa ccm kila walikoenda. Lowasa akaulizwa swali na mtoto mdogo akakasirika sana na kumshambulia mtoto yule na mwalimu wake. Serikali ya ccm ikajua kuwa mambo yameanza kuharibika.
Dr Slaa akatembelea Marekani na kukutana na watu wengi tu. Wana JF wa America wakapeleka hoja ya Zitto na Slaa kwa serikali ya America na wafadhili. Serikali za nje zikamtia presha Kikwete afanye uchunguzi wa BOT. Serikali ikaingia mkataba na E&Y kuchunguza yaliyotokea BOT. E&Y ikapewa muda na ikatoa report yake. Report ikavuja JF, Serikali ikakalia report kwa zaidi ya mwezi mmoja. Balali akaandika barua ya kujiuzulu na serikali ikazuga kuwa haikupata barua ya Balali. Kikwete akatoa vipande tu vya report na kutaja makampuni 22 tu yasiyojulikana huku akiacha wapambe wake wa karibu nje. Wapinzani wauliza kupewa report ya E&Y wakaambiwa kuwa hilo ni jambo la usalama wa taifa.
Kikwete akatangaza kutengua uteuzi wa Balali na kuipa bodi ya BOT (ambayo ndiyo iliyoshiriki katika wizi wa awali) miezi sita kuchunguza kile kilichochunguzwa na waliochunguza ile kamati iliyochunguza ile kampuni iliyochunguza yale CAG aliyochunguza baada ya kampuni ya uchunguzi kuchunguza uchunguzi wa .....nimechanganyikiwa sasa.
Baada ya miezi sita, Kikwete anajiandaa kuunda kamati ambayo itahusisha viongozi wa dini na vyama vya upinzani ili vifanye uchunguzi wa kile bodi itamaliza kuchunguza baada ya miezi sita. Kuna habari kuwa hiyo kamati itapewa miezi 18 kumaliza kazi yake.
Pamoja na PR strategy na maneno ya vitisho ya kumfuta kazi na kutaka kumshitaki Balali, Kikwete na serikali yake iliyowekwa madarakani na pesa za wizi toka BoT, hawana ubavu kabisa wa kumshtaki Balali au yeyote aliyehusika na wizi wa BoT unless.........
Wana JF, watch this thread..............