Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Nadhani kuna mtu anatakiwa kusema; hawa viongozi sasa hivi wanawanchanga wananchi. Wanapita mikoani wakifanya shughuli za serikali huku wakiwaasa wananchi kuwa waangalifu na watu wanaopiga kampeni kabla ya muda wake. Wanatoa maonyo kuwa "muda wa kampeni bado"!
Lakini wao wenyewe wanapigiwa kampeni na hawaoni tatizo na wakati mwingine wao wenyewe wanawapigia kampeni watu wengine. Angalia Kikwete alipoenda Tanga sijui kule na Makamba akampigia kampeni waziwazi na yeye hakusema kitu na hivi majuzi Pinda akiwa Igunda, Irambo nk ambako naye amewapigia kampeni wabunge wa sasa kuwa wachaguliwe tena; amefanya hivyo pasipo kuuma maneno!
Sasa nina ombi: Kama hawataki kumaanisha wasichosema basi wasikiseme; kama watu wengine ni makosa kuanza kupiga kampeni mapema ndani ya CCM wao ni kina nani hata waanze kuwapigia wengine kampeni? Kwanini wanaonesha upendeleo wa wazi kwa wanachama wengine wa CCM wakati jukwaa halijafunguliwa kwa wote!
Nasema mnawachanganya wananchi au nyinyi wenyewe mmechanganyikiwa!