rusesa
JF-Expert Member
- Jun 1, 2013
- 538
- 233
Kipindi hicho cha awam ya nne JK alituhamisha kutoka analogia kwenda digital. Digital hii ilisifiwa sana, ati itakuwa safi na iliyotukuka na yenye manufaa kwa wananchi wa Tanzania.
Makampuni makubwa kama startimes, azamtv, ting, continental n.k yalianza kutoa huduma kwa wananchi, huku bei ya visimbuzi ikiwa chini na channel za nyumbani ikiwa ni bure kwa wananchi wa kipindi cha kikwete!
Sasa ni utawala mpya na mambo mapya. Mambo sasa ni tofauti ving'amzi hivi sasa bei juu. Vifurushi navyo bei juu pia. Mbaya zaidi serikari hii hawawabani hawa watoa huduma wanafanya wanavyotaka! Hata channel za nyumbani lazima zilipiwe. azamtv kifurushi sh. 15000 startimes(dish) 18000 n.k
Huu utawala unaojinasibu kutetea wanyonge je nyie hamuoni kama wananchi hawamdu bei hizo za vifurushi? hadi channel za nyumbani? uhuru wa kupata habari kwa mwananchi uko wapi? Hawa wenye ving'amzi wasiposimamiwa na serikari kupitia TCRA nani atamfunga paka kengere?
Kwa mwanchi wa kawaida kuangalia Tv kwa sasa ni anasa! watu wanaishi chini ya dola moja, mlo mmoja kwa siku je mwananchi kama huyo ataweza kulipia gharama zote hizo? yaani hata haki ya kupata channel za nyumbani ni nongwa?
Serikali ya utawala huu angalieni tena upya suala hili. Mbona nchi zingine local channel huwa ni bure? mbona nchi zingine wanamitambo ya kuvisimamia vingamzi hivi mfano kama umelipia kifurushi na wakati huo huo hujawasha Tv kifurushi chako kinakuwa hakitumiki! sawa sawa na luku ya umeme, ukizima switch umeme hautumiki. Lakini kwa sasa ukinunua kifurushi cha king'amzi halafu ukasafiri hata kama hukuwasha Tv utakuta kifurushi kimeisha!
Kwanini mliingia kwenye digitali kwa kukurupuka? TCRA MKO WAPI?
Magufuli TCRA ni jipu kuu.
Nawasilisha!