Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 2,375
- 3,559
Aliyekuwa waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliwahi kusema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na taasisi za kimataifa, Tanzania inashika nafasi ya sita kwa Bara la Afrika kwa kuwa na gharama za chini za bando “vifurushi” huku ikishika nafasi ya 50 Duniani kwa gharama ya chini ya data.
Nape alitoa ufafanuzi huo wakati aliposhiriki kipindi cha Power Breakfast on Saturday cha Clouds TV na redio, Agosti 20, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo alisema na kudai kuwa bei ya data kwa wastani wa 1GB ni Dola 1.71 sawa na shilingi 3990. Maneno ya Nape yalikuwa “Tanzania kuwa miongoni mwa Mataifa yenye gharama za chini za mawasiliano haimaanishi kuwa itapunguza malalamiko kwa kuwa uchumi wetu haufanani na wananchi wengi wana kipato cha chini”.
Nape alidai kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kufanya tathmini ya gharama za uwekezaji, utunzaji na usafirishaji wa data kila baada ya miaka minne na tathmini nyingine inafanyika mwaka huu ili kupata uhalisia wa gharama za bando kama zitapanda au kushuka.
Aidha, Nape aliweka wazi kuwa Serikali imeruhusu ushindani kwa kuweka mazingira wezeshi ya kuwa na kampuni nyingi zinazotoa huduma za mawasiliano ambapo huduma ya vifurushi ni huduma ya ziada inayotolewa na makampuni hayo na kuleta unafuu wa gharama za mawasiliano.
Kama ni mfuatiliaji wa mtandao na habari za ulimwengu basi ni wazi umepata kuona viongozi wa Safaricom Kenya wakikutana na kitu kizito sana kutoka kwa Elon Musk, dharau zao sasa zimekuwa majuto kwao kwa kile ambacho Starlink wamekuja kuwapatia nafuu ya gharama za mtandao ndani ya Kenya. Kwa taarifa za wazi kutoka mtandao wa X unadai kuwa mtu anaweza kufurahia mtandao kwa gaharama ya 40657.50 sawa na dola 15 za kimarekani.
Safaricom kwa sasa hawana ujanja tena kwa kile ambacho kinaendelea ndani ya Kenya, ni Safaricom ambao walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea na kiburi kikubwa, huduma mbovu kupita maelezo na kuzima mtandao kwa maagizo ya serikali. Starlink anakuja katika Wakati ambao wakenya wengi wamechoshwa kupita maelezo. Kwa sasa sijui utamwambia nini Mkenya aendelee kutumia huduma za mtandao kutoka Safaricom Wakati ameona kuna nafuu kubwa sana ya kutumia Starlink.
Mageuzi haya yasiishie tu ndani ya Kenya bali Starlink fanya hima na Tanzania mje ili mitandao yetu hii ipate kujifunza na kukaa kwa adabu! Mara kadhaa gharama za bando zimekuwa zikipanda tu bila mpangilio wowote wa msingi huku TCRA akiwa kimya kama haoni kinachoendelea. Starlink akija Tanzania atatuonesha wapi panavuja na wapi kuna tatizo kabsa ndani ya hizi kampuni za mawasiliano.
Je unadhani Starlink akija Tanzania, utaendelea kununua bando la wiki kila siku au utahamia Starlink bila hata kuaga mtandao wako?