Rais , Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete amesema wale wote wanaombeza kuhusu utendaji kazi wake wataona
aibu atakapomaliza muhula wake 2015.
Rais ameyasema hayo wakati akizindua mradi wa kusambaza umeme katika
mikoa ya Mwanza na Geita unaofadhiliwa na mfuko wa Changamoto wa
Milenia(MCC).
Rais amesema Serikali yake itavunja recodi ya kusambaza umeme katika
vijiji vingi nchini.
Jk amesema Tanzania inaongoza kwa mtandao wa barabara ambao ni bora
afrika mashariki huku akiwahakikishia wakazi wa Kagera kuwa meli mbili
alizowaahidi wakati wa kampeni ziko njiani zinakuja.
Rais alikuwa akishangiliwa na wananchi wakati wote wa hotuba yake.
Alisema Tanzania ni nchi kubwa kuliko nchi nyinine za Afrika Mashariki
,lakini ina mtandao mkubwa wa barabara kuliko nchi kama Kenya , lakini
akawalaumu watu wanaoisifia nchi hiyo jirani na kubeza mafanikio ya
serikali yake.
Aidha, Rais Kikwete amewashangaa baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na
wananchama kushindwa kuzungumzia mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya
CCM na badala yake wamekuwa hodari wa kujadili wanapobezwa na wapinzani"
Source: Mwananchi