Kikwete Msanii- Kujenga majengo kwa Machinga ! Kilimo kwanza vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Msanii- Kujenga majengo kwa Machinga ! Kilimo kwanza vipi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Masanilo, Oct 22, 2010.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Na Angetile Osiah
  JUMATATU nilishangaa kusoma habari kubwa kwenye magazeti mbalimbali ikielezea mkakati wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete aliyoitoa kwa wafanyabiashara ndogondogo wanaojulikana kama Wamachinga.

  Kikwete, ambaye amekuwa akitoa ahadi zinazozidi 71 sasa tangu aanze kampeni, aliahidi kuwa atajenga majengo mengine matano ya kufanyia biashara kwa Wamachinga katika kuhakikisha kuwa wanafanya shughuli zao kwenye maeneo bora.

  Mbali na ahadi ya kujenga, Kikwete pia aliahidi kuwa atasimamia ugawaji wa nafasi za kufanyia biashara baada ya jengo la kwanza lililopo wilayani Ilala, Machinga Complex, kugubikwa na ugawaji uliozingatia undugu, ukabila na urafiki.

  Ni ahadi ambayo ingeweza kushangiliwa na wafanyabiashara hao ambao hadi sasa hawajaweza kudhibitika licha ya halmashauri za wilaya kutenga maeneo mazuri kama vile hilo la Mtaa wa Lindi (Machinga Complex), Temeke Stereo na mengineyo.

  Lakini si ahadi inayoendana na kukua kwa jiji na mahitaji ya dunia ya leo. Kusema ukweli Wamachinga ni vijana ambao hawana elimu yoyote ya biashara ambao walikimbia vijijini kutokana na kilimo na shughuli za ufugaji kutokuwa na malipo mazuri.

  Katika maeneo mengi ya vijijini, nguvukazi ya vijana sasa haipo maana vijana wote wamekimbilia mijini kuja kuuza soksi, mashati, miswaki, leso, maua, dawa za meno, viatu 'feki', sumu za panya na mende, na vitu vingine visivyodumu ambavyo hununuliwa na wafanyabiashara wakubwa nje ya nchi kwa fedha nyingi za kigeni.

  Karibu miaka minne iliyopita, ripoti ya Benki Kuu (BoT) ilionyesha kuwa fedha nyingi za kigeni zilifujwa kwenye kununua bidhaa kama hizo ambazo si muhimu sana katika ukuaji uchumi, ukiachilia mbali kununua petroli na dizeli. Sasa tunataka tutumie fedha zaidi kununulia bidhaa hizo kwa kuwatengenezea Wamachinga mazingira mazuri ya kuuzia vitu hivyo?

  Sidhani kama JK alifikiria tatizo ambalo Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akipambana nalo sana la vijana kukimbilia mijini. Utawala wa Nyerere ulijaribu kwa kila hali kujenga mazingira mazuri vijijini ili vijana waone umuhimu wa kuzalisha badala ya kukimbilia mijini kutafuta kazi au kufanya biashara hizo ndogondogo.

  Ahadi hiyo ya Kikwete inamaanisha kuwa sasa vijana hawatakuwa na kizuizi cha kuendelea kumiminika mjini maana tayari wameandaliwa makazi; wameandaliwa maeneo bora ya kufanyia hizo shughuli zinazoitwa biashara ndogondogo; hawana haja tena ya kuzalisha nyanya kwa sababu zinauzwa Shoprite; hawana haja ya kuzalisha matunda kwa sababu yapo Shoprite.

  Vijana wa Tanzania hawana haja tena ya kuzalisha viazi mviringo kwa sababu vipo Shoprite; hawana haja tena ya kuzalisha ndizi kwa sababu zipo Shoprite.

  Na kwa sababu serikali ya Afrika Kusini haitaki 'wataalamu' hao wa biashara ndogondogo huko, imeandaa mazingira mazuri vijijini ili vijana wa huko Sauzi wabaki mashambani wakizalisha matufaa (aple) , nyanya, ndizi, viazi, machungwa na bidhaa nyingine za kilimo ili ziletwe huku Tanzania ambako serikali imewafanya wasipende kilimo; "wanataka kuwa wafanyabiashara ndogondogo".

  Shoprite wanajua kuwa huku kuna "Kilimo Kwanza" cha mdomoni ndio maana wanatuma taarifa Afrika Kusini kutaka vijana wa huko waendelee kuzalisha bidhaa za kilimo ili ziletwe Tanzania.

  Na leo Shoprite watakuwa wamefurahia kusikia mtu ambaye ameshika nchi na kuhubiri Kilimo Kwanza, kuwa ndiye aliye tayari kukaribisha vijana wanaokimbia kilimo huko Muheza, Tukuyu, Mchinga, Nzega na kwingineko kwa kuwajengea majengo yatakayowawezesha kuuza bila bughudha bidhaa ambazo hawazizalishi kama kama bazoka, peremende, tochi, vikombe, mashati mawili kwa siku na miwani 'feki' ya jua.

  Wenzetu wanafikiria kujenga majengo makubwa (shopping malls) kwa ajili ya wafanyabiashara wakubwa na kuweka mazingira mazuri kwa wakulima ili bidhaa za kilimo zipate soko kirahisi na kuuzwa kwenye mashoprite yao badala ya kusubiri nyanya na nyama ya ng'ombe kutoka Afrika Kusini.

  Nadhani tatizo la kwanza la kilimo ni soko la bidhaa zake. Iwapo serikali itaweka mazingira bora ya kuwezesha bidhaa za wakulima kuwa na soko, hakutakuwa vijana ambao wanadharau maisha ya shamba. Watathamini kilimo na kuongeza juhudi. Hizo power tillers watanunua kwa kuona umuhumu wa kilimo.

  Lakini leo hii hawaoni umuhimu wa 'power tillers' kwa sababu hizo bidhaa wanazozalisha kwa jembe la mkono hazina soko; nyingi zinaozea shambani au barabarani. Kwanini wasikimbilie mijini.

  Kama kweli JK ana mpango wa kujenga hizo Machinga Complex tano zaidi ili ziwe sita, basi hana budi kubatilisha mawazo yake mara moja na kufikiria ni jinsi gani hizo fedha alizotenga kwa majengo hayo, zinaweza kutumika katika kuweka mazingira bora ya soko la bidhaa za kilimo.

  Kilimo kikiwa na thamani, hao Wamachinga hawatakubali kuja Dar es Salaam kutembea kilomita 15 kila siku kuuza pakti tatu za dawa za meno; au kushinda kutwa pale Karume kuuza soksi jozi tatu; au kushinda Buguruni kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 5:00 usiku kuuza mifuko 10 ya nailoni kwa Sh100 kila mmoja.

  Kipindi cha kampeni si cha kutoa ahadi ambazo utekelezaji wake ni wa mazigazi. Ni kipindi cha kunadi sera na kuambiana ukweli kuhusu mipango ya maendeleo hata kama mipango hiyo itaumiza watu.

  Source: Mwananchi
   
 2. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Alikuwa wapi siku zote hizi!?? A fool will always think that hes fooling others but in fact those others are not fools and they sees him as a foolish!!
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  raisi katoka chalinze ,unategemea nini kipya
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwenzenu huwa nikimsikiliza Kikwete naishia kucheka tu! sijawahi msikia akiongea kitu cha maana hata siku moja! Mhhhhh
   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Narudia tena, kuwepo na kuzagaa kwa wamachinga ni dalili ya tatizo kubwa ambalo linatakiwa ufumbuzi, sio kulipalilia!
   
 6. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  hivi yuko nafasi ya ngapi katika marais bogas kuwahi kutokea?
   
 7. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  We uliona wapi mtu na akili zake anawadanganya wananchi kuwa atanunulia nets kwa ajili ya kuepa Malaria!?? Wth!??:crying::crying:. He doesnt even know that to solve the problem you need to deal with, what caused the problem (source)! hiyo ni theory simple you don't need to be genius!! Yakk! na atanunua hizo net mpaka atie akili lakini he will never solve the problem! hellllppp!!!!
   
 8. WA MAMNDENII

  WA MAMNDENII JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2010
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kaaazi kwelikweli hiyo degree ya uchumi ya JK aliyopata mlimani ndiyo inayomtuma uchumi wa nchi utakuwa kwa kujenga magulio ya kuuza bidhaa feki kutoka ng'ambo?
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamaa mweupe sana!
   
 10. r

  realtz7 Senior Member

  #10
  Oct 23, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  o wananchi ambao still wanamshangilia km dhahabu, mbaya zaidi ndo hao hao masikini zaidi na wanaotuletea matatizo ktk nchi hizi za kiafrika! shabashh
   
Loading...