Kikwete mnyongeni lakini haki yake mpeni!

mie nakuunga mkono kabisa mdau, imefika wakati watanzania tujaribu kuchanganua mambo kwa mapana na marefu, tunahitaji kuwa na serikali inayojali utawala wa kisheria na demokrasia matatizo ya kiuchumi yaliyopo TZ kama utakuwa umetembea nchi nyingi za afrika bado watanzania tuna nafasi kubwa ya kusema tuna uchumi mzuri ukilinganisha na nchi zingine kama kenya, uganda, burundi hata rwanda, sudan nk. Ukubwa wa TZ huwezi linganisha na rwanda, mfumo wa barabara na miundo mbinu bado tz tuko vizuri tuuunge mkono serikali ili tuzidi kujiimarisha kiuchumi, tusubiri 2015 kama mnataka kubadilisha chama basi tumieni haki yenu ya kikatiba lakini mkianza kampeni leo kwa kweli mnatuyumbisha wananchi wengine, tafakari, chukua hatua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…