Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,904
- 1,364
Amejiandaa kujibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wananchi? Hofu yangu ni kwamba mengine yanaweza kuwa embarrassing kwa mkuu wa nchi. Hii imekaaje? Au kuna watakaoandaliwa kuuliza maswali?
huu ni uzushi ndugu wadanganyika..hizo simu mtu baki hutazipata...na ukipiga zikaita hazitapokelewa live..watakaosikika redioni ni wale walioandaliwa..na RAIS mpaka sasa maswali anayo..toka kwa walio andaliwa..hili ni changa la macho jamani..kama anajiamini..aende ukumbi wa hbr maelezo au ikulu aite waandishi wote tu..wampige maswali pale..live..sio kutudanganya na mambo ya TBC
Nitakuwa busy na big brother huyu muungwana hana kipya!
Jamani nafasi imepatikana.Wengi humu ikitolewa hoja huwa tunataka uthibitisho au wadau wenyewe wajibu.
Presha ya wadau imezaa matunda,nyoka katoka pangoni,ni wakati wa kuandaa maswali ambayo tunaona hayajapata majibu stahili,Halafu kesho great thinkers wanaingia kazini kufanya uchambuzi.
Shime tutumie nafasi hii adhimu kupata na kushinikiza hoja zetu,tukiendelea kuponda haisaidii na ndipo vilaza watapata nafasi ya kuuliza maswali dhaifu.
Aidha, Rais atasikiliza matarajio ya wananchi katika jitihada zao za kuboresha maisha yao kwa kujiletea maendeleo.
Mzee wa nchi na nchi na wapambe wake hawana jipya, ameshindwa kumrudi Lowasa na richmond, ameshindwa kumrudi Rostam kwa ufisadi na zaidi ameshiriki kumsulubu Sita. Anataka tumuulize maswali gani??? Labda atuambie ataondoka lini kwenye pango takatifu kutoa fulsa ya kumwingiza mtu muungwana na muadilifu
Aidha, Rais atasikiliza matarajio ya wananchi katika jitihada zao za kuboresha maisha yao kwa kujiletea maendeleo.
Kwa hiyo itabidi umjibu kwanza. Nini matarajio yako?
Naona hata baada ya kukaa Ikulu kwa miaka 4 bado hayajui!!!😕
Maswali yangu kwa Rais ni haya;
Ndugu Rais, ni lini unatarajia kujiuzulu?
Na ni lini utafukuza viongozi na wafakazi wote wa serikali ambao ni wazembe na wafujaji?
Watu wanakufa Loliondo, Mara, Morogoro na sehemu nyingine nchini lakini sioni wewe kama Rais unafanya nini.
Mikataba ya kifisadi bado inaendela kufanyika nchini, bado umefumba macho.
Kama mtendaji mkuu wa serikali, maazimio ya Richmond bado yako tete kutokana na uzembe wa serikali yako.
Elimu nchini inadidimia siku hadi siku, bado hakuna lolote linalofanywa na serikali yako.
Ajali za barabara zinagharimu maisha ya watu, nguvu kazi na rasilimali nyingi za nchi lakini sioni wizara husika/serikali ina mpango gani.
All this make me sick to my stomach!!
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kesho, Jumatano, Septemba 9, 2009, atazungumza moja kwa moja na wananchi kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na vyombo vingine vya utangazaji nchini kuanzia saa mbili na nusu usiku. Mbali na TBC, televisheni nyingine za ITV, TVZ, Mlimani TV, Tumaini TV na Channel Ten zinatarajia kuonyesha mazungumzo hayo.
Rais atatumia aina mpya ya kuwasiliana na wananchi kwa kusikiliza hoja zao, kwa kujibu maswali yao, kusikiliza ushauri wao na kupata maoni juu ya mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu, Serikali yetu na maendeleo yetu.
Aidha, Rais atasikiliza matarajio ya wananchi katika jitihada zao za kuboresha maisha yao kwa kujiletea maendeleo.
Mazungumzo hayo yatakayochukua muda wa dakika 90 kuanzia saa mbili unusu usiku (saa 2:30 usiku) hadi saa nne kamili usiku.
Aidha mazungumzo hayo yatatangazwa kwenye redio za TBC-Taifa, Sauti ya Tanzania, Zanzibar, Radio Mlimani, Radio Clouds, Radio Tumaini, na Radio Uhuru.
Maswali, maoni, hoja, ushauri utapokelewa moja kwa moja na TBC kupitia simu nambari +255-22-2772448, +255-22-2772452 na +255-22-2772454.
Aidha, maswali, maoni, hoja ama ushauri unaweza kutumwa moja kwa moja TBC kupitia ujumbe mfupi wa SMS kwenye nambari 0788-500019, 0714-591589 na 0764-807683 ama kupitia kwenye barua pepe swalikwarais@yahoo.com kuanzia leo.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inawashauri wananchi kutumia kikamilifu nafasi hiyo ya kuwasiliana moja kwa moja na Rais wao.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM .
08 Septemba, 2009
Jamani nafasi imepatikana.Wengi humu ikitolewa hoja huwa tunataka uthibitisho au wadau wenyewe wajibu.
Presha ya wadau imezaa matunda,nyoka katoka pangoni,ni wakati wa kuandaa maswali ambayo tunaona hayajapata majibu stahili,Halafu kesho great thinkers wanaingia kazini kufanya uchambuzi.
Shime tutumie nafasi hii adhimu kupata na kushinikiza hoja zetu,tukiendelea kuponda haisaidii na ndipo vilaza watapata nafasi ya kuuliza maswali dhaifu.