Kikwete: Kwanini nilimpa Ridhiwani fomu atembeze | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Kwanini nilimpa Ridhiwani fomu atembeze

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jul 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Asema ilikuwa kazi binafsi si ya chama
  [​IMG] Aeleza miaka miwili alikuwa anajifunza
  [​IMG] Aahidi hana mpango wa kuongeza mke  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete (kulia) akirudisha fomu za kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa katibu wa CCM Yusuf Makamba katika ofisi za makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amesema uamuzi wa kumtuma mwanaye, Ridhwani, kutembeza fomu yake mikoani kutafuta wadhamini ni sahihi kwa vile suala la kugombea urais ni lake binafsi na si la chama.
  Rais Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akihutubia maelfu ya wanaCCM waliohudhuria hafla ya kurejesha fomu yake ya kukiomba chama ridhaa ya kutetea kiti hicho, baada ya zoezi la kupata wadhamini mikoani kukamilika.
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Yusufu Makamba, jumla ya wanaCCM waliomdhamini Rais Kikwete, ambaye ni mwanaCCM pekee aliyechukua na kurejesha fomu hiyo, ni 14,069 kati wadhamini 2,800 waliokuwa wakihitajika.
  Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM mjini hapa na kutawaliwa na mbwembwe nyingi, zikiongozwa na wasanii wa ngoma za asili, muziki wa dansi, kizazi kipya, sarakasi kwa vijana na kwaya kutoka kikundi cha uhamasishaji cha chama hicho cha Tanzania One Theatre (TOT) chini ya kiongozi wake, ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Mashariki, John Komba (CCM). Rais Kikwete alisema mara baada ya kuamua kumtuma Ridhiwani kutembeza fomu yake mikoani kutafuta wadhamini, yalizuka maswali mengi, moja likihoji kwa nini atumwe Ridhiwani na wengine kudiriki kutamka kwamba, kwa kumtuma mwanaye, amewadharau viongozi wa wilaya na mikoa wa chama.
  “Yameulizwa maswali mengi, kwa nini Ridhiwani? Na mimi nikawauliza kwa nini si Ridhiwani? Mimi kugombea urais, si jambo la chama. Ni langu miye. Linapokuwa langu miye, wa kumtuma wa kwanza si mwingine isipokuwa mwanangu na marafiki zake na wenzake,” alisema na kuongeza:
  “Na wapo waliosema kwa kumtuma Ridhiwani, amewadharau viongozi wa wilaya. Sivyo.Viongozi wa wilaya na mikoa wajibu wao katika zoezi hili ni kuandaa wanachama wa kuwadhamini wagombea.
  Zoezi la kutembeza fomu kutafuta wadhamini ni la mgombea mwenyewe. Kazi yake yeye, anaigharimia yeye, anahangaikia yeye. Yakimshinda, yamemshinda. Akiweza kwenda, Katibu Mkuu yeye ni kungojea tu. Viongozi wa wilaya na mkoa kule wanangojea kwenye ofisi za chama. Mgombea amepita, hakupita shauri yake.”
  Alimshukuru Ridhiwani, Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Benno Malisa, Katibu Mkuu wa Umoja huo, Martin Shigela, pamoja na marafiki zao, kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kutembeza fomu yake kutafuta wadhamini mikoani.
  Pia alimshukuru Yusufu Makamba kwa kupokea fomu yake bila mizengwe.
  Vilevile, aliwashukuru wote waliomchangia kwa hali na mali na kudhamini fomu yake na kusema hana cha kuwalipa, isipokuwa watalipwa na Mwenyezi Mungu.
  Rais Kikwete alisema wanaCCM wenye sifa ya kuwa Rais ni wengi sana kwenye chama hicho, lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza baada ya yeye kuchukua fomu.
  Alisema jambo hilo ni kielelezo cha imani kubwa waliyonayo kwake, wamempa heshima kubwa, hivyo hana budi kuwashukuru.
  Pia, alimshukuru Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CCM), kwa uamuzi wake wa kuondoa nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM na kumchangia Sh. 200,000 taslimu kwa ajili ya kusaidia kampeni zake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Fedha hizo alikabidhiwa na Shibuda katika hafla hiyo jana.
  “Matumaini yangu ni kwamba Halmashauri Kuu itapitisha na kupendekeza jina langu kwa Mkutano Mkuu na Mkutano Mkuu utaniteua na baada ya uteuzi, ni matumaini pia wananchi watanichagua tena kwa kishindo kikubwa wanipe ridhaa na fursa ya kuendelea kuwahudumia na kuwatumikia Watanzania wenzangu kwa nafasi ya Rais,” alisema Rais Kikwete.
  Alisema iwapo atachaguliwa tena, atafanya vizuri zaidi kuliko alivyofanya katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano iliyopita, kwa vile kazi ya urais haina shule ya kusomea, bali mtu anajitokeza na wenzake wanamuamini na yeye kujiamini, wanamchagua na kuanza kazi.
  “Ukiwa na bahati ya kumkuta mwenzako aliyekutangulia, akakuelekeza jinsi mambo yanavyofanywa kama alivyonisaidia mzee Mkapa (Rais Mstaafu wa awamu ya tatu), unajua namna ya kuanza,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
  “Lakini hata hivyo, kuna mwaka mmoja mpaka miwili ya kwanza bado unajifunza. Unajaribu hili liko hivi, unajaribu hili haliendi sawa sawa, unajaribu lile.
  Hatimaye kwenye mwaka wa tatu, wa nne na wa tano ndio unakuwa umezoea, unapata kasi nzuri na mambo unaelewa vizuri,” alisema.
  Kutokana na hali hiyo, alisema katika miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake, kulikuwa na miaka karibu miwili ya kujifunza, ambayo serikali yake imeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, miaka mitano ijayo, ambayo haina tena la kujifunza, ana uhakika itafanya makubwa na vizuri zaidi.
  “Ninachoomba wanaCCM wenzangu mkiunge mkono, mkipigie kampeni chama chetu kipate ushindi mkubwa, wananchi waendelee kuunga mkono serikali ya Chama Cha Mapinduzi tutakayoiunda iwapo tutachaguliwa. Kwa hiyo, tunakwenda kwenye uchaguzi kwa msimamo wetu uleule, mafiga matatu,” alisema Rais Kikwete.
  Alimshukuru mkewe, Salma, kwa ushirikiano mkubwa alioutoa kwake pamoja na wanawe na kusema: “Sina sharti la Askofu (la kuoa mke mmoja tu) maana mimi ni Muislamu, (wake) wanne. Ninaye mmoja, nina nafasi tatu, lakini sikusudii kuzijaza, maana umri nao unakwenda.”
  Kauli hiyo ilitolewa na Rais Kikwete, baada ya Makamba, ambaye alitumia muda mwingi kunukuu vifungu mbalimbali vya Kur’ani Tukufu na Biblia Takatifu kueleza kuwa Rais Kikwete anazo sifa za Uaskofu zilizotajwa katika Waraka wa Paulo Mtume kwa Timotheo na kusema: “Kwa hiyo, wewe Mheshimiwa Rais ni mtumishi wa Mungu. Sifa zote unazo, lakini sina hakika ile moja ya kuwa na mke mmoja kama unayo.”
  Awali, Makamba alisema utabiri alioutoa wakati Rais Kikwete anachukua fomu kwamba, dalili zinaonyesha kuwa atakuwa ni mgombea pekee wa urais, umethibitika jana kwa vile hadi mchakato huo unahitimishwa jana, hakuna mwanachama mwingine aliyejitokeza kuchukua fomu. Makamba alisema hali hiyo inaonyesha jinsi gani wanaCCM walivyo na imani na Rais Kikwete kwa vile ndiye mtaji mkubwa kwa chama na kwa hiyo, anaamini kuwa atakivusha chama katika uchaguzi wa Oktoba.
  “Tunamuomba Mungu atuchagulie Rais na huyo Rais asiwe mwingine uwe wewe kwa sababu wewe ni mzuri.
  Hata Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema Rais anaweza kutoka chama chochote, lakini Rais mzuri atatoka CCM,” alisema Makamba.
  Hafla hiyo ilianza saa 5:10, mara baada ya Rais Kikwete akifuatana na mkewe pamoja na wanawe, kuwasili katika viwanja hivyo, huku gari lake likisindikizwa na msafara wa magari na pikipiki, zilizokuwa zikiendeshwa na watu waliovalia mavazi rasmi ya CCM.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Naona Kikwete kaamua kuwakata ngebe wanaosema ana mke mwingine, kutoka ukoo wa Rostam, au New York au bint 'Al kharoos'.
   
 3. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Si dhani kama hii ni sababu....Swala hapa ni kuwa Ridhiwani anaandaliwa mazingira salama ya kuachwa pazuri kisiasa ili hapo baadae nae aweze kuwa kama baba yake. Si swala geni ila ni style tofauti na kina Mwinyi kama alivyomfanyia Dr. Mwinyi au Rais anaeondoka madarakani visiwani Zanzibar....Kikwete sio wa kwanza, kuna akina Bongo, kabila nk. so point hapo ni kumuacha Mwanawe pazuri kisiaza na kumpa uzoefu ajue game likoje siku nae akiingia asiwe mgeni kama mie. Ni maoni tu....
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Duh urais una majaribioa miaka miwili ? thought its not on job training,ok ndio bongo .
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jul 3, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kikwete ni bogasi sana:

  (a) Kudai kuwa akigombea uraisi basi ni jambo la familia ni makosa makubwa sana hasa katika mazingira ya Tanzania ambapo misingi ya utawala bora haijaimarika; kufanya hivyo ni kama kuhalalisha ugawanyaji wa madaraka ya uraisi kifamilia.

  (b) Majibu haya ya Kikwete yana contradiction kubwa sana kulingana na majibu yaliyotolewa na Ridhiwani mwenyewe siku anapokea hati ya uwakili. Yeye alidai kuwa ni kwa sababu ni mjumbe wa UVCCM siyo kwa sababu ni mtoto wa Kikwete, lakini Kikwete anadai ni kwa sababu Ridhiwani ni mtoto wake!!! Funny!!

  (c) Kuwa na learning curve inayo-stabilize baada ya miaka miwili kunaonyesha kuwa yeye ni kilaza sana; hawezi kujifunza mambo kwa haraka haraka. Katika nchi nyingi zilizoendelea au zinazoendelea kwa kasi, kiongozi anakuwa madarakani kwa miaka kati ya mitatu hadi minne tu: Kikwete atatumia muda wote huo kujifunza bila kufanya kazi alioomba.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  That's Kichuguu for you.Concise and to the point in this case. I love that contradiction between Kikwet and Ridhiwani, ust shows how unstrategic the Kikwete campaign is, kama kauli za Jakaya Kikwete na Ridhiwani Kikwete zina contradiction hivyo tutegemee vipi coherency kutoka kwa rais wakati atakapo kuwa ana deal na watu kutoka the diversity of CCM / Tanzania ?
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Ukiona mtu mzima anabadili kauli zake mara kwa mara ujue kuna jambo. But to you my beloved president...I offer my friendship and sympath. Siasa hazina mathematical formulations. Zinabadilika kuliko uranium fission and fussion in the nuclear reactor.
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mhh hapo kwenye mke kadanganya:twitch:
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kweli nimeshangaa JK kusema alitumia miaka miwili kujifunza wakati alishakuwa waziri huko nyuma. Je Mawaziri aliwachagua walitumia muda gani kujifunza. Wakuu wa mikoa aliowateua na kuwahamaisha wanatuia muda gani kujifunza?

  Pili JK na Ridhwani na wale watto wa vibosile na wazazi wao wasome kitabu cha mtoto wa warren buffet kinaitwa Life is What You Make it: Finding Your Own Path to Fulfillment"

  Yahoo waliwai kufanya summary ya hicho kitabu kama ifutavyo

  NB. Hiyo money rich parent unaweza kureplace na parent wit political power
   
 10. A

  August JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  na kama alikuwa anajifunza, si unajifunza kutoka kwa watu waadilifu?, ni sawa na mimi nikitaka kujifunza nitafanya urafiki na watu ambao naona nitapata mazuri toka kwao ni sio kwenda Mtaa wa ohio, au Kinondoni makaburini nikasema nilikuwa najifunza tabia njema.. pili kuna vitu vingine vipo pia wazi kabisa, havihitaji kujifunza bali akili ya kuzaliwa. Nyerere kuna wakati aliwahi kusema kwa kutumia maisha yake kwamba yai bovu anailelewa. Hivyo kiongozi yoyote muuadilifu mkataba mbovu anaujua.
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,066
  Trophy Points: 280
  "Mimi kugombea urais, si jambo la chama. Ni langu miye. Linapokuwa langu miye, wa kumtuma wa kwanza si mwingine isipokuwa mwanangu na marafiki zake na wenzake," alisema na kuongeza"
  Angalia kiongozi wetu asvyo na upeo! yaani yeyer hajaona tatizo!!! kweli?? hivi kina Salim aliwashinda nini huyu mtu dhaifu hivi?
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Jakaya ni mtu wa ajabu sana!! Mtu unapoomba kazi ,huendi kujifunza jinsi ya kuifanya hiyo kazi bali unakwenda kutekeleza yale yanayokupasa kutekeleza kwani unakuwa na sifa stahili. Sasa huyu bwana anaposema ametumia miaka miwili kujifunza katika kipindi cha miaka zaidi ya kumi aliyokuwa kwenye cabinet alikuwa anafanya nini kama sio kusinzia!! Kama kazi ya kutembeza fomu za kuomba wadhamini ni ya familia mbona mwaka 2005 familia yake haikufanya kazi hiyo na nduguze walikuwepo? Ukweli ni kwamba anatafuta justification ya kumpa madaraka mwanae na marafiki zake wakina Malisa kwa kigezo cha kutafuta wadhamini period. Hivyo basi jitayalisheni hapo Ridhwani atakapokuwa CO-presida na kuteua viongozi wa serikali ya bongo kipindi cha 2010-2015!!
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  hovyooooo
   
Loading...