Kikwete kumalizia kumsafisha Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kumalizia kumsafisha Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 17, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kuletwa tena na serikali ripoti ya utekelezaji wa maamuzi ya bunge juu ya richmond Lowassa atakuwa amesafishwa rasmi-siyo na bunge, siyo na magazeti bali na rafiki wa siku nyingi na mshirika wake katika safari ya siasa. Si kwamba JK ana uchaguzi katika hilo; hana. Na wana CCM wote (hamaanisha wote) watasema "amina". Na bomu la wapiganaji ccm litakuwa limeteguliwa kitaalam. EL ametambua kuwa : mlete rafiki yako karibu lakini adui yako karibu zaidi.
   
  Last edited: Sep 17, 2009
 2. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwanakijiji mada imekaa kiana aina ebu tueleze ulichokusudia.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,901
  Trophy Points: 280
  usishange hata lowasa nae akijiunga na wapinga mafisadi-tunapigwa changa la macho
   
 4. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hili balaa!
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Tusubiri tuone itakuwaje. kama kweli itakuwa ndivyo hivyo lazima tukubali kuwa sisi ni wajinga. Yaani ndivyo tulivyo. Lowassa hasafishiki, kama mtu amewahi kulidanganya bunge lenye maprofesa kuwa uchumi unapaa wakati hata Rostowian theory hajui, amejaribu kuwaghilibu watanzania kwa mvua za bandia ambazo hatuzihitaji, na Richmond and so on then tutakuwa wajinga....tusubiri. lakini sitaki kuamini kama bunge litarui kulekule kuwa mhuri.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ukiona mtu amechafuka na tope na maji yanayomzunguka ni ya matope ujue kwamba yeyote atakayejaribu kumsafisha kwa maji hayo naye atajikuta amechafuka na tope.
   
 7. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Weli at the end wote watachafuka. Swala la msingi ni jee mmoja au wote wakichafuka SISI tunafanya nini? Baada ya kuona uchafu no one cares. By the way ni lini huyu msafishaji aliwahi kuwa Msafi ndo sasa tuseme atachafuka??
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,901
  Trophy Points: 280
  Lakini atasafishika kivipi???????
   
 9. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Umenena kweli. Huyu mtu laona anuanuka uvundo wa chuma, ili atakate labda akaoge oil ya gear box au Acid, vinginevyo hatakati kabisa
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mwanakijiji,

  Na inasemekana ktk mkutano wa bunge ujao mwezi Novemba, wabunge wote wa CCM watakaa kama kamat ya chama na kukubaliana kuanza upya na kusahau yaliyopita na hapo watatangaza rasmi kuwa hoja ya ufisadi imefungwa ndani ya chama na yaliyobaki yashughulikiwe na vyombo vya dola.

  Baada ya hapo itafuata ripoti ya utekelezaji ya masuala ya richmond (iliyofanyiwa marekebisho na mkulu) na hapo itatamkwa wazi kwamba EL hakuwa na kosa kisheria bali alishauriwa vibaya na wataalamu ambao wamekwisha onywa.

  Serikali kupitia waziri mkuu itatoa taarifa ya kuufunga mjadala wa richmond ndani ya chama na nje ya chama. Huu ndio utakuwa mwisho wa kikundi cha akina Mwakyembe na EL atakuwa huru rasmi baada ya kikao hicho cha bunge.
   
 11. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Tena atachafuka kuliko yeye, kwani msafishwa atatakata na msafisha atachafuka.
  Ni sawa na kusafisha samaki unabaki na shombo
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Juzi hapa kasema wametoka mbali na Mkuu wa Kaya hawajakutana barabarani na hata hawatatenganishwa barabarani na watu wanao mchafua mlitegemea nini hapo ndicho tunacho kisubili sasa kama maamuzi ya Bunge kuhusu swala la Richomnduli kuna kauvivu flani kushughulikia basi tutarajie kusafishwa rasmi EL na tutegemee atachukua nchi 2015 Uswahiba unaendelea.
   
 13. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Njaa bwana, ninaamini kama vya vya upinzani vingejiunga pamoja kama walivyo fanya Kenya CCM ingetoka, shida wataanza kugombania madaraka.
   
 14. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Katika hindu mythology kuna kitu kinaitwa 'Karma',msingi mkuu wa dhana ya Karma ni kama ule wa Murphy's law kwamba 'la kuwa litakuwa tu',tuko pamoja Wakuu wa jamvi?
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Vyama vya upinzani visahau kuchukua nchi kwa njia ya kura unless mambo yafuatayo yafanyike kwanza.

  1. Waongeze nguvu zao katika kudai mabadiliko ya Katiba ili kuwe na Tume huru ya uchaguzi itakayodhibiti mbinu zote chafu za wizi wa kura na kumanipulate final tallies of election results- Kwa hili sisiM imejipanga vilivyo kulizima.

  2. Wakiisha pata Tume huru ya Uchaguzi, wagombee ubunge kwanza si Mbowe, Lipumba et al ili kulichukua bunge yaani wawe na filibuster majority ya kupitisha agenda za mageuzi, hili nalo kwa sisiM ni bora punda afe mzigo ufike wapo tayari kwa lolote.

  3. Kukiisha kuwa mazingira ya usawa na haki na uhuru katika chaguzi, na baada ya kuwaonesha wananchi kuwa wapinzani wanaweza tena zaidi ya sisiM hapo tunaweza pata rais wa kwanza wa kidemokrasia halisi katika historia ya nchi.

  Vinginevyo haya yoote tunayoongea ni kelele za mlango, sisiM wanajua wanachokifanya kwani style yao ni kuwa, Jeshi la wananchi, UWT, Polisi na kila chombo kilicho katika serikali ni lazima kijue kuwa masilahi yao ni masilahi ya CCM, kushindwa kwa CCM ni kupoteza kwaoa maslahi hayo. Hivyo wamekula viapo vya mioyoni kuwa watailinda CCM mpaka tone la mwisho.

  Ukweli ni kwamba Tanzania ilitakiwa ifikirie kuingia kwenye siasa za vyama vingi labla mwaka 2080. VINGINEVYO KUWE NA WA KUFANYIWA KAFARA KWA AJILI YA UKOMBOZI WA KWELI WA KULETA DEMOKRASIA- Un-option which is not recommended by any one unless you feel useless and stranded for you life is no difference to death because of "POVERTY"
   
 16. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  wajinga ndio waliwao, huyu EL kama tayari amesharudi kwa hii serikali ya jk
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Jasusi, maneno mazito sana haya, sio siri kwamba the mafisadi's plan ni Lowassa kurudishwa next cabinet, katika capacity ya foreign au defense, ili aweze kuwa na nafasi nzuri ya urais 2015, lakini tatizo la hii theory ni wapiganaji na Membe, ambaye sasa hivi sio siri ndiye namba two,

  - Kwa maoni yangu ni kwamba Lowassa hatakuja kuwa anything tena zaidi tu ya alipofikia sasa, kosa kubwa sana alilolifanya kisiasa ni kukosa umakamu wa CCM kwa sababu tu ya tamaa zake za fisi, mbio zake zote huko pembeni ni bure tu na wala sio siri kwamba anatumia hela nyingi sana za kifisadi kujitengeneza njia ya kurudi, lakini CCM as a chama hawawezi ku-afford maana ni kuwapa Chadema risasi za bure.

  - CCM haiwezi kupambana na Chadema majukwaani bila ya kuwa ya wabunge wake wapiganaji 11, majuzi wamejaribu maji kule NEC, wameona response ya media na wananchi na hata baadhi ya viongozi mbali mbali kuanzia wa dini mpaka wa upinzani, tatizo la Lowassa ni hawa wapiganaji 11 ambao hana dawa ya kuwamaliza au kuwatoa kwenye picha, kwa hiyo he is stuck and done, ingawa hatakwenda hivi hivi.

  Respect.

  FMEs!
   
 18. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2009
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  I support your point, ni kweli tutapiga kelele bila tume huru na kuondoa mbinu chafu za CCM hamna kitu ushindi na kuiondoa madarakani
   
 19. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  sentensi nzito sana hiyo. Kuna hidden message hapo. Nadhani wanaJF tungependa ufafanuzi zaidi...
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hasa ukizingatia kuwa Six naye alishapigwa bit la nguvu
   
Loading...