Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Nilisema zamani, safari zimeanza siku nyingi. Sasa JU imekuwaje ametoswa? Si walipatana sana? Mbona imebadilika?
Nini kiketokea tangu miaka hiyo ya 70 mpaka leo?
kumbe huyu ni JU na aliwahi kuwa karibu na kikwete?
lakini kumbukumbu zinaonyesha ju alishawahi kuwa mkuu wa wilaya kadhaa hapa nchini na mara ya mwisho alikuwa mkuu wa wilaya ya ilala kabla ya kuingia katika ujjasiliamari wa kuanzisha vyombo vya habari
JU alikuwa serikalini. Alikuwa mkuu wa wilaya ya Ilala. Wakati wa kuanza kwa vyama vingi wakuu wa wailaya ndio walikuwa wakitoa vibali vya mikutano ya vyama basi akawa anatoa vibali bila kinyongo wala uoga na tukawa tunafanya mikutano kwa kujinafasi. Serikali kuona hivyo ikamhamishia Singida; akaachana na ukuu wa wilaya na kujianzishia gazeti la Dimba akiwa na wenzake toka magazeti ya uhuru na mzalendo.
Ninachofahamu kwa dhati ni kwamba Mama Salma sio Mke wa Kwanza Wa Rais Jakaya Kikwete.
Mama huyu (ambaye kwa Taaluma ni Mwalimu) ameolewa rasmi kati ya miaka ya mwisho mwa 1980 wakati huo Rais Kikwete akiwa Waziri Wizara ya Madini,nakumbuka kwenye Harusi hiyo Juwata Jazz walitumbuiza na nilisikia Kiongozi wa Bendi hiyo Mzee Muhidin Ngurumo ana undugu wa karibu ama na Rais au Mkewe. Kipindi hicho cha harusi watoto wa Rais, Ridhiwan na Salama walikuwepo. Mkuu wa Nchi alifanya Harusi hiyo pale nyumbani kwake Regency Estate.
Katika kuandika haya tujaribu kuepuka kejeli na lugha za matusi, vinginevyo thread itaondoa maana yake. Heshima ni kitu cha bure!
Hao "Wenzake" ni pamoja na marehemu John Rutayisingwa, , akina Dr. Gideon Shoo na Bwana Johnson Mbwambo ambaye wako wote mpaka sasa pale Raia Mwema
Roger that Pasco.
Pia Superman, ungetuelezea ni jinsi gani wewe unamjua Kikwete ( Kama Raisi na kama binadamu wa kawaida). Ungeanza kwa mazuri (kama ulivyofanya) kisha ukamalizia na udhaifu wake alafu sisi wadau tungemalizia tunayoyajua. Ila kwa kutupa habari kutoka UHURU (Gazeti la chama) na Wikipedia, unatuweka katika wakati mgumu kwani hatujui hata unachotaka sisi tuonge ni nini.
Jile79, share na sisi kwa nini CV iliyobandikwa hapo si ya maana?
Kikwete ana watoto nane kama ifuatavyo:-
Mke wake wa kwanza Marehemu, Mama Aziza Sabuni alikuwa na watoto wawili, Ridhiwani na Salama.
Mke wake wa pili, Mama Salma (ambaye alimuoa baada ya mke wa kwanza kufariki) ana watoto Miraji, Ally, Khalfan, Mwanaisha na Rashid Chodo.
Mtoto wa nane ni wa kuasili, alimchukua akiwa mdogo wakati huo pia akiwa Rais na kumfanya ni mwanae, ni mtoto yatima.
Hongera Super Man, unafanya kazi nzuri, ili usiishie kwenye kupitisha ufagio peke yake kwa kufagilia tuu, baada ya kufagia, sio vibaya ukachoma na takataka pia, ili kuuhalalisha huo usafi ulio ufagia, sio mbaya ukasema na uchafu uliosafishwa.
The guy is good, ila binafsi nina mashaka na intelect yake, kugraduate sio issue enzi za Nyerere, GPA jee?.
Wizara zote alizopita alifanya nini na aliacha nini cha kukumbukwa (kila kona alipitia, kila kilichokatiza mbele ya macho yake ali...!)
He is married to Salma na wana watoto 8!, find out hao watoto 8 kama mama yao ndio huyo! you'll be surprised!.
Kufagilia tufagilie, lakini hapa JF, twende deep zaidi kidogo kwa kwenda over and above google na wikipedia, kwa vile JK ni rais wetu, tunaishi nae, tunamfahamu kwa karibu his streghths ni katika kusmile, na weaknesses zake jee?, yeye ni binadamu tuu kama binadamu wengine, tena dhaifu sana, sio tuu kwenye mambo ya kitaifa!, jamaa ni dhaifu!...
Tuendelee na kufagilia.