Amesema kweli kabisaHabari wadau.
Kuna video inasambaa mitandaoni ikimuonyesha Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete akimuelezea aliyekuwa Rais wa tano wa Tanzania hayati Dkt. Magufuli kuwa tangu akiwa waziri alikuwa adui mkubwa wa wanafiki, wazembe na wababaishaji kazini. Kikwete amesema watu hao hawakumpenda akiwa waziri na hata alipokuwa Rais na ikizingatiwa kuwa nchi yetu inakabiliwa na wimbi kubwa la watu kuwa wazalendo mdomoni lakini kwa vitendo wanafanya mambo tofauti kabisa.(MIGA)
Kikwete kwenye hiyo video amefafanua kuwa wakati akiwa Rais jembe lake alikuwa waziri Dkt. Magufuli na alimpa kazi ya kuunganisha mikoa yote kwa barabara za lami na kweli mpaka anaondoka madarakani mwaka 2015 walikuwa wamefanikiwa kuunganisha mikoa yote isipokuwa katavi tu.
Kikwete amesema bila ubunifu na kujituma kwa Dkt. Magufuli isingewezekana.
Seen mkuu
Kwani wewe mbw hutakaa kaburini!?hayati magufuli alikuwa mtu mzuri sana sema tu ni ule ujinga wake wa kuua nzi kwa bunduki ndio unamdmfanya aonekane jitu moja katili kwelikweli ambalo sehemu pekee linakoweza kukaa ni kaburini
Kikwete kawiva kisiasa haswa.Yaan usije ukafanya kosa kubwa kumuanin kikwete huyu ni master wa vita ya kisaikolojia anakulaghai huku mwenyewe ukishangilia kwa kupiga makofi kwa mikono na sio miguu kama zuzu .ninamifano miwili ya kwanza ishu ya katiba mpya aluliwaita ikulu wapinzan akawapa chai na mandaz na juis juu na kusikiliza hoja zao kisha kukubaliana nazo na kuunda tume ya katiba mpya haraka sana na akaaaid kabla hajaondoka katiba mpya itapatikana tume ikapewa hela ikaanza kaz wapinzan wakaona mtu ndio huyu mwaka mmoja kabla ya kuondoka madarakan akawajibu kua suala hilo aliwez limenshinda wasahau ,
Pili kipind cha uchaguz wa mgombea urais wa ccm lowasa alikua na nguvu na kuungwa mkono na wajumbe wote ilikua bila lowasa kupita mkutano uvunjike na yeye aliliona hilo bas bwana yule wakat anaingia ukumbin akakutana na hamasa na shauku ya wana ccm wakisisitiza tunamtakalowasa tu huku wakiimba mbele ya mwenyekit na mwenyekiti akaanza kuimba nao wakaona mpaka. Mwenyekit anaimba nas suala limeisha hilooo kilichokuja kutokea kila mjumbe alipigwa na butwaaaa lowasa alichinjwa gafla bin vuuu