Kikwete: Hata kama Mtu anayechochea Wananchi ana mapembe, tutayakata!

sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
566
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh Jakaya Kikwete leo akihutubia katika Mkutano wa CCM mkoani Dodoma huku akionekana mwenye hasira, amesema kua Serikali haipo tayari kuwavumilia wale wote wanachochea wananchi kufanya Vurugu baada ya Waziri wa Nishati na Madini kuwasilisha hotuba yake leo.

Alisema kua wapo watu Viongozi wanaochochea kwa Maslahi ya kisiasa na kwamba watahakikisha wote wanakamatwa iwe wapo ndani au nje ya nchi na kuwafikisha katika vyombo vya Sheria.

Akiongea kwa hasira alisema kua "Hata kama anaechochoe Wananchi kufanya Vurugu Ana PEMBE watamkamata na kumkata hizo Pembe."

Source: TBC1 TAARIFA YA HABARI.

TAMKO LA IKULU:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amelaani vikali fujo na ghasia zilizofanyika mjini Mtwara leo, Jumatano, Mei 22, 2013, akisisitiza kuwa raslimali yoyote inayopatikana katika sehemu yoyote ya nchi yetu ni mali ya Watanzania wote na lazima itumike kuwanufaisha wote.

Rais anaamini kuwa ni jambo lisilokubalika kuwa raslimali ya nchi inaweza kuzuiliwa isitoke katika eneo ambako inapatikana kwa vile hakuna nchi yoyote duniani inayoruhusu jambo la namna hiyo. Nchi hiyo haipo na wala sera za namna hiyo haziwezi kuanzia Mtwara.

Aidha, Rais anasisitiza kuwa Sera ya Serikali ni kwamba kila mtu, kila Mtanzania anayo haki ya kunufaika na raslimali ya nchi yetu yakiwemo maeneo ambako inatoka raslimali.

Rais Kikwete haoni sababu yoyote ya msingi ya kufanyika kwa fujo na ghasia za Mtwara. Fujo hizo hazina kichwa wala miguu, hazina mshiko na wala waliofanya fujo hizo hawaelezi wanataka nini isipokuwa kuhitimisha nia na dhamira yao ya kufanya fujo na kuharibu bila sababu mali za wananchi na zile za taasisi za Serikali.

Itakumbukwa kuwa wakati zilipotokea fujo na ghasia kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa mwaka huu, Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda alikwenda Mtwara akakutana na akazungumza na makundi mbali mbali na wananchi wa Mtwara. Ilionekana kama ulikuwa umepatikana mwafaka wa kuhakikisha kuwa jambo hilo halitokei tena.

Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Pinda aliwaelezea kwa undani kabisa fursa nyingi zinazowasubiri wananchi wa Mtwara kwa sababu ya ugunduzi wa gesi asilia na mipango ya Serikali kuhakikisha kuwa Mtwara na maeneo jirani yananufaika. Miongoni mwa mambo mengine, Mheshimiwa Pinda aliwaeleza yafuatayo:

  1. Kwamba kiasi cha viwanda 57 vya shughuli mbali mbali vitajengwa Mtwara ili kuhudumia shughuli za uzalishaji wa gesi asilia na maendeleo ya uchumi wa Tanzania kutokana na gesi asilia hiyo. Idadi hii ya viwanda haijapata kujengwa katika eneo lolote la nchi hii katika historia.
  2. Kwamba kiasi cha gesi asilia ambacho kitatoka Mtwara kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa shughuli nyingine za kitaifa ikiwamo kufua umeme ni asilimia 14 tu, na kuwa kiasi kinachobakia cha asilimia 86 kitabakia Mtwara kwa ajili ya kuzalisha huduma mbali mbali na kuhudumia idadi hiyo kubwa ya viwanda.
Isitoshe, Rais anajiuliza kuwa kama gesi asilia isipotoka Mtwara itabakia huko inafanya nini kwa sababu bidhaa yoyote ni lazima ifikishwe sokoni ili iweze kuuzika. Gesi asilia hiyo ikibakia katika eneo la bahari la Mtwara itawafaisha vipi wananchi wa Mtwara hata kama wakifanya fujo kila siku?

Rais Kikwete anawakumbusha wafanya fujo wa Mtwara na vinara wa fujo hizo kuwa Serikali inao wajibu wa kulinda usalama wa wananchi pamoja na usalama wa mali zao. Hivyo, Rais Kikwete hakubali fujo na ghasia zilizofanyika Mtwara leo. Anazilaani vikali na wala hatakubali wafanya fujo wachache kuvuruga amani na usalama wa nchi yetu popote walipo na kwa kisingizio chochote kile iwe ni kutafuta umarufu wa kisiasa ama kulinda maslahi binafsi ya kibiashara.

Serikali itawasaka na kuwakamata wote walioshiriki katika fujo za leo na kuwafikisha mahakamani. Aidha, Serikali itawasaka na kuwakamata viongozi na vinara wa fujo na ghasia hizo na kuwafikisha mbele ya sheria hata kama wana mapembe makubwa kiasi gani.

Rais Kikwete anawapa pole sana wananchi wa Mtwara ambao wameathirika binafsi kwa kuumizwa ama mali zao kuharibiwa katika fujo na ghasia za leo. Anapenda kuwahakikishia kuwa Serikali yake itachukua hatua za kukomesha vitendo hivyo vya fujo na ghasia katika eneo hilo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Mei, 2013

Kikwete atoa Tamko kali

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amekemea vikali vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Akizungumza katika eneo la Kizota, Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete alisema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali.

Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote... "Hivi watu wa Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?," alihoji kwa ukali Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka wale wote wanaoongoza vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo... "Tutawasaka hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata."
Alichosema Waziri Muhongo.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema mradi wa kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, umeanza kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda huko wiki ijayo kuweka jiwe la msingi.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini jana, Waziri Muhongo alisema:

"Mradi wa kujenga bomba la gesi uko palepale na unaendelea kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ataenda kuweka jiwe la msingi wiki lijalo."
"Tumezungumza mengi kuhusu suala hilo na hata viongozi wa watu wa Mtwara walipelekwa nje kujifunza faida zake, lakini hata kama hawajaelewa, nimetoa kijitabu kinachozungumzia faida mbalimbali watakazopata wana Mtwara katika mradi huo."

Profesa aliyeanza hotuba yake kwa kueleza machapisho mbalimbali yaliyotolewa na wizara yake kufafanua faida za gesi ya Mtwara kwa taifa, alisema mradi huo uliozinduliwa Novemba mwaka jana na Rais Kikwete, unahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 532 na kipenyo cha nchi 36.

"Bomba hilo lina uwezo wa kusafirisha futi za ujazo za gesi milioni 784 kwa siku. Mradi utahusisha mitambo miwili ya kusafirisha gesi asilia katika maeneo ya Mnazi Bay- Madimba (Mtwara) na Kisiwa cha Songosongo (Lindi). Utagharimu Dola za Marekani 1,225.3 milioni," alisema.

Alisema kazi za usanifu wa mradi na ulipaji fidia kwa wananchi wapatao 3,092 waliopisha maeneo ya mradi, zimekamilika na hatua za awali za ujenzi wa mitambo ya kusafirisha gesi asilia zimeanza.

Source: Mwananchi
 
Bure kabisa na wala hamna kitu pale!!!!!!!

Kile wanachokililia watu wa Lindi na Mtwara tayari tunayo kwenye sera yetu ya taifa - KUONGEZA THAMANI RASILMALI YOYOTE NCHINI PALE PALE INAKOVUNWA - sasa hadi hapo chokochoko na vyama vya upinzani vinaingia vipi tena????????
 
Kufuatia sakata la gesi Mtwara mh rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania atoa tamko la serikali,serikali haitavumilia chokochoko la uvunjifu wa amani,asema mtwara ni ya tanzania yote.Kuwashughulikia wanasiasa wote wanaoeneza chokochoko na uchochezi bila kujali nyadhifa zao!sheria ya vyama vya siasa kutazamwa upya.



Kikwete Mbabaishaji na mbinafsi, si aseme tu anapeleka Bagamoyo!

Kama siyo kweli kwanin asipanuwe bandari ya Tanga au mtwara?

Badala yake anaanzisha nyingineo Bagamoyo kwanini bagamoyo na siyo Tanga au Mtwara?

Utanzania wake upo kwa gesi ya mtwara tu mbona kwenye bandari hatujauona huo Utanzania?
 
Sems baba maana ukimya wako hawautumii kwa manufaa ya watanzania umewapa midomo sasa wanaitumia visivyo kamata wote hao vinara wa jambo hili na wanamtwala kaeni chini na serikali mpate ufumbuzi wengine watawadanganya tuu na kuwaacha mkiuana wenyewe.
 
CCM ni marafiki wa wa China na wao hawaamini katika haki za watu wote na asemacho JK ndiyo hasa mawazo na msimamo wa wa China kuua kwa ajili ya madini na faida ya Wachina .
 
Vurugu za Lindi na Mtwara, Saed Mwema fuata maelekezo ya sheria zetu za nchi na ukawakamate haraka sana maafisa wetu hawa, Rais Kikwete na Waziri Muhongo, kwa kupindisha maelekezo ya sera (na kusababisha michafuko) yetu ya taifa inayowaelekeza wao kama maafisa wetu wa taifa kufanya maamuzi yanayohakikisha rasilmali zote zinaongezewa kwanza thamani pale pale kunakovunwa.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani mh Jakaya Kikwete leo akihutubia ktk Mkutano wa Ccm mkoani Dodoma huku akionekana mwenye hasira, amesema kua Serikali haipo tayari kuwavumilia wale wote wanachochea wananchi kufanya Vurugu baada ya Waziri wa Nishati na Madini kuwasilisha hotuba yake leo.

Alisema kua wapo watu Viongozi wanaochochea kwa Maslahi ya kisiasa na kwamba watahakikisha wote wanakamatwa iwe wapo ndani au nje ya nchi na kuwafikisha ktk vyombo vya Sheria.
Akiongea kwa hasira alisema kua Hata kama anaechochoe Wananchi kufanya Vurugu Ana PEMBE watamkamata na kumkata hizo Pembe.

Source: TBC1 TAARIFA YA HABARI.

mkwara kuku badala ya kutafuta suluhuu yeye anatafuta mchawi
 
Mhnnnn...maelezo hayo na mengine niliyosikia kama tamko la mkuu wa kaya itv yamkini yasilete mwafaka na maridhiano ya fukuto la mgogoro wa gesi Mtwala.
 
Mimi sidhani kama wananchi wa mtwara wanachochewa haja yao gesi isisafirishwe bali umeme ndio usafirishwe sasa nani anachochea,Kikwete atimizi majukumu yake na si kuongea na vyombo vya habari muda wote
 
TAIFA LETU LINAANGAMIA KWA BAADHI YA VIONGOZI WETU KUKOSA HEKIMA NA BUSARA KATIKA KUSIMAMIA MASWALA NYETI YENYE MASLAHI MAZITO KWA UMMA

Sakata la Gesi kule Lindi na Mtwara ni kielelezo cha UTAWALA WA MTU (Rais Kikwete) apendezwavyo na kutelekeza kabisa dhana zuri ya UTAWALA WA SHERIA (Sera yetu ya taifa ielekezyo kuongeza dhamani rasilmali kunakovunwa) kusiginwa kwa kutumia nguvu ya dola.
 
Wale wa EPA walimshinda kukata hata unywele sembuse hao.
Tena watachanganyikiwa wakisikia Arusha tarime mbeya morogoro na kagera wajiunga kuwasapoti wana mtwara.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani mh Jakaya Kikwete leo akihutubia ktk Mkutano wa Ccm mkoani Dodoma huku akionekana mwenye hasira, amesema kua Serikali haipo tayari kuwavumilia wale wote wanachochea wananchi kufanya Vurugu baada ya Waziri wa Nishati na Madini kuwasilisha hotuba yake leo.

Alisema kua wapo watu Viongozi wanaochochea kwa Maslahi ya kisiasa na kwamba watahakikisha wote wanakamatwa iwe wapo ndani au nje ya nchi na kuwafikisha ktk vyombo vya Sheria.
Akiongea kwa hasira alisema kua Hata kama anaechochoe Wananchi kufanya Vurugu Ana PEMBE watamkamata na kumkata hizo Pembe.

Source: TBC1 TAARIFA YA HABARI.
Wachochezi ni CCM. Hamtaki kukaa na wananchi.
 
Kutumika kwa nguvu kubwa mtwara siyo suluhu matokeo ya kutumia nguvu kubwa Mtwara kutasababisha vifo vya wananchi wengi wakati vifo vinaweza kuepukwa kwa serekali kukaa na wanamtwara ili isikilize wanacho kihitaji ni kitu gani.Si amini kama wanamtwara hawataki gesi hiyo isiwanufaishe na watu wengine.Wanamtwara wanachotaka hapa pamoja na gesi kuwanufaisha watu wengine lakini kabla ya watu wengine kuanza kunufaika na hiyo gesi.Wao wanaanza kunufaika vipi na gesi hiyo ambayo iko katika maeneo yao.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Tatizo ni ukosefu wa hekima, busara na maarifa ya uongozi lkn pia ulevi na hang over ya madaraka
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom