Kikwete: Harakisheni sheria ya Usalama mitandaoni

Kikwete: Harakisheni sheria ya Usalama mitandaoni

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Rais Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhakikisha mchakato wa Sheria ya Usalama kwenye mitandao unakamilika na kuanza kutumika, ili kudhibiti wanaotoa siri za nchi kwa kisingizio cha uhuru wa habari.

Hayo aliyasema jana kwenye hafla ya uzinduzi wa mtambo maalumu wa usimamizi na uhakiki wa Mawasiliano ya Simu, (TTMS), iliyofanyika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Dar es Salaam.

Rais Kikwete alisema hakuna nchi yoyote duniani ambayo haitunzi siri zake, kwa kuwa jambo hilo ni muhimu kiusalama, hata kwa mataifa ambayo yamekuwa mstari wa mbele kutetea uhuru wa vyombo vya habari.

Alisisitiza kwa kumtolea mfano aliyekuwa Jasusi wa Marekani, Edward Snowden, anatuhumiwa kuvujisha siri za nchi hiyo kwenye mtandao, ambaye sasa amekimbilia mafichoni Urusi. Aliwapongeza TCRA kwa hatua hiyo, akieleza kuwa inawezesha uchumi wa nchi kupata kichocheo cha kukua kwa kuwa sasa kutakuwa na udhibiti wa mawasiliano hasa ya simu za nje ya nchi na kuongeza kipato kwa taifa.

Chanzo: Mwananchi la leo
 
Sasa wangedhibiti tungejuaje mambo ya EPA, Meremeta, Deep Green Finance, Mwananchi Gold, Mabilioni ya Uswisi, nk?
Kwa hali ilivyo ni afadhali mitandao iachwe ifanye kile kifanywacho sasa hadi tutakapopata Uongozi ambao uko serious na maslahi ya nchi yetu!
 
Ni kweli hongera mheshimiwa rais ikiwa siri za nchi yetu zitavuja basi utakuwa ndo mwisho wa uhai wa taifa letu
 
Samuel Luhanga bana huwa simuelewi wakati mwingine.Anasema kuwa kuna watu wanautumia vibaya uhuru wa habari kwa kutoa siri za nchi ila anachoshindwa kuelewa ni kuwa hiyo sheria ya usalama wa vyombo vya habari ikianza kufanya kazi Watawala wataitumia vibaya kuficha uovu wao kwa sababu hizo hizo anazozisema Samuel Luhanga but at the worst case scenerio.Hope the upcoming new constitution will put all these crazy laws to rest.
 
Ha ha ha. we ni mchokozi sana .Samuel Luhanga umetukumbusha mbali sana, wakipitisha hiyo sheria tutakuwa tunalitumia sana hilo jina kumzungumzia yeye.
 
Hataki watu wajue alipewa suti hana lolote au île habari ya mwanaye na drugs imemuuma
 
Tulisaini sheria ya utandawazi sasa tunataka kuikacha? Siri za nchi zinaeleweka na hakuna mtu atakayethubutu kizivujisha humu. Yote mengine hasa kama serikali inafanya visivyo ni haki ya wananchi kujua ili tuchukue hatua mapema.
 
Sisi ndiyo wenye nchi, watoto wetu wanauza madawa ya kulevya, sisi tutatawala milele.
Zote hizo ni siri za nchi.
Shughuli ya Kinana ni siri ya nchi, wananchi hamtakiwi kujua.
 
Sisi ndiyo wenye nchi, watoto wetu wanauza madawa ya kulevya, sisi tutatawala milele.
Zote hizo ni siri za nchi.
Shughuli ya Kinana ni siri ya nchi, wananchi hamtakiwi kujua.

wacha wee !
 
hapo safi sana Mkuu. umesomeka vizuri sana hakuna kuvunja sheria za mawasiliano kizembe.
 
Hilo ni muhimu kufanyika hata chumba changu cha kulala kina haki ya usiri kikatiba na kisheria, kwa hilo Mh. Rais naunga mkono hoja ya serikali
 
Back
Top Bottom