Kikwete , Dk Slaa hapatoshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete , Dk Slaa hapatoshi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 14, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kikwete , Dk Slaa hapatoshi

  Na Waandishi Wetu

  WAKATI kampeni za uchaguzi mkuu zikikaribia kumaliza mwezi mmoja, mashambulizi baina ya wagombea yanazidi kuwa makali baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa kutangaza nia ya kumpandisha kizimbani mke wa rais, huku Jakaya Kikwete wa CCM alirushia makombora wanachama waliokimbilia upinzani.

  Kampeni za uchaguzi zilianza rasmi Agosti 21 na kasi yake ilipunguzwa kutokana na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, lakini sasa zinazidi kupamba moto baada ya vyama vyote kuanza rasmi kuwania tiketi ya kuingia Ikulu, Bunge la Jamhuri ya Muungano, Baraza la Wawakilishi na kwenye mabaraza ya madiwani.

  Dk Slaa, ambaye amekuwa akieleza jinsi mke huyo wa rais, Mama Salma Kikwete anavyotumia mali za serikali kumpigia debe mkewe, jana alikwenda mbali zaidi alipotangaza kuwa atamfungulia mashtaka ya kutumia vibaya mali za umma.

  Akihutubia wananchi wa Kibara kwenye Jimbo la Mwibara jana, Dk Slaa, ambaye amebobea kwenye sheria, alisema Chadema inafikiria kumfungulia kesi Mama Kikwete dhidi ya matumizi hayo ya mali za umma.

  Dk Slaa aliueleza umati uliokusanyika kwenye mkutano wake huo kuwa katiba ya Jamhuri ya Muungano haimtambui Mama Salma Kikwete kama mfanyakazi wa umma, hivyo hapaswi kutumia mali za umma.

  "Mama Kikwete amekuja Musoma kwa kutumia ndege ya serikali yenye namba za serikali 5HTGF kitu ambacho ni kinyume cha makubaliano yaliyopo,'' alidai Dk Slaa.
  Alisema tangu kampeni zianze, Mama Kikwete amekuwa akifuja fedha za serikali wakati hana mkataba na umma wa Watanzania.

  Kwa mujibu wa Dk Slaa anachofanya mke huyo wa Rais Kikwete ni kama alichofanya mke wa rais wa Zambia kumpigia kampeni mumewe kimakosa na ndiyo maana amefikishwa mahakamani kwa kufanya kosa.

  Alisema kuwa bajeti ya Kikwete ya Sh150 bilioni si ya mke wake bali ni za Kikwete mwenyewe kuutumikia umma.

  Mama Kikwete ni mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama) na amekuwa akifanya ziara mikoani kwa muda mrefu, lakini katika siku za karibuni amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akishawishi wananchi wampigie kura mgombea huyo urais wa CCM.

  Akiwa mkoani Singida hivi karibuni, Mama Kikwete aliwataka wananchi wawachague wagombea wa CCM kabla ya kuwatambulisha na baadaye kutaja orodha ya ahadi zilizo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM.

  Kumekuwepo na kauli mbili tofauti kutetea safari zake mikoani na kujihusisha kwake na kampeni. Ikulu iliwahi kukaririwa ikisema kuwa mke wa rais naye ana fungu lake, wakati CCM ilishakaririwa pia ikisema kuwa safari za Mama Salma zinagharimiwa na chama hicho.

  Mbali na Mama Kikwete, Dk Slaa alimtaka Kikwete asipoteze muda kuwadanganya Watanzania kuwa amejenga madarasa wakati elimu bora hakuna na darasa la saba halimsaidii Mtanzania kufika mbali.

  "Serikali ya CCM ni wizi mtupu kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali,'' alisema Dk Slaa.
  Katika hatua nyingine, Mama Kikwete jana alikuwa Mwibara kusuluhisha mgogoro ambao unadaiwa kuwepo baina ya wana-CCM wa jimbo hilo baada ya kuchakachuliwa katika kura za maoni kwa aliyekuwa mbunge wajimbo hilo, Charles Kajege.

  Wakati Dk Slaa akielekeza shutuma hizo kwa mke huyo wa rais, mumewe alikuwa akiendelea kuwashukia makadawa chama hicho waliohamia upinzani akisema kuwa wamepotea kwa kuwa wapinzani hawana sera.

  Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akizungumza kwenye kampeni zake zilizofanyika mji mdogo wa Maramba wilayani Mwibara.

  Ingawa Kikwete hakuwataja makada hao walioihama CCM baada ya kura za maoni, baadhi yao ni aliyekuwa mbunge Jimbo la Maswa, John Shibuda na Thomas Nyimbo ambao wote wamehamia Chadema.

  Kikwete alisema ni vyema makada hao wangekubali matokeo kuliko kukasirika na kujiunga na vyama vya upinzani.

  "Wale waliojiunga na vyama vya upinzani baada ya kura za maoni wamepotea kwa kuwa wamekwenda kusiko na sera, mtandao wala miundo thabiti bali baadhi huibuka tu wakati wa uchaguzi," alisema Kikwete.

  Alisema kimsingi hakuna chama kinachofanana na CCM kwa kila kitu ikiwamo muundo, sera, mtandao na hata mpangilio kwani chama hicho kiko kila kona nchini na kinatambulika kwa wananchi.

  “Vyama vingine ni vya uchaguzi tu, utaona bendera nyingi wakati huu tena zote mpya, lakini uchaguzi ukipita huoni wanachama wala chama,” alisema Kikwete ambaye aliwataka wagombea wa CCM wasikose usingizi kwa sababu ya wapinzani.

  “Unapochukua fomu kuwania uongozi usijiwekee asilimia 100 ya kushinda, bali jione kuwa unaweza kushinda au kushindwa hiyo haitakupa presha ukishindwa,” alisema Kikwete.
  Mgombea huyo alisema iwapo atachaguliwa kuwa rais katika kipindi kingine cha miaka mitano, Serikali yake itaanzisha kilimo cha zao la kakao ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.

  Alisema kwa maeneo ya pwani zao hilo litasaidia kuongeza kipato kwani hivi sasa minazi imeingiliwa na ugonjwa aliouita ukimwi ambao hata hivyo alisema serikali yake ipo katika harakati za kulitafutia ufumbuzi.

  Kikwete aliahidi pia kuwa kati ya mwaka 2011 na 2015 vijiji 11 vilivyopo wilayani Mkinga, vitakuwa vimepatiwa maji safi ili kuondokana na tatizo sugu la uhaba wa maji.
  Alisema mradi huo utakaogharimu Sh427 milioni utakuwa kuwa mwarobaini wa tatizo la maji wilayani humo.

  Akiwa uwanjani hapo, Kikwete aliwanadi wagombea udiwani akiwamo wa Kata ya Maramba, Said ambaye alisoma naye Shule ya Sekondari ya Tanga.

  “Huyu Said nilisoma naye Tanga School nikiwa kiranja wake. Naomba mumpe kura ili niendelee kuwa kiranja wake nikiwa Rais wa Jamhuri,” alisema Kikwete na kuomba pia Dastan Kitandula achaguliwe kuwa mbunge wa jimbo la Mkinga.

  Source: Mwananchi:


  My take: (Kwenye red) Kwa nini NEC ya Malakame isimkemee mama huyu? Makame anaogopa nini na hali kisha pitilza muda wake wa kustahafu?
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Makame amkemee mama wa kwanza? Utaona mizengwe atakayofanyiwa!
   
 3. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  heh, hadi nilisahau wadau...kumbe KAKAO bado ipo, eti JK kaahidi kakao, teh teh teh.....
   
 4. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  walitakiwa waongozane wote kwenye kampeni...!

  sasa ukimwi utadhibitiwa vipi..? manake na haya ma bodigadi sio wakuwaamini..!

  mnakumbuka yule Mamba wa swaziland alipommega first lady..!
  :becky::becky::becky:
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  My take: (Kwenye red) Kwa nini NEC ya Malakame isimkemee mama huyu? Makame anaogopa nini na hali kisha pitilza muda wake wa kustahafu?


  Amkemee mama wa "SHUKA KWA SHUKA " ataanzia wapi anaweza nyimwa na mafao yake yote :becky::becky:
   
 6. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #6
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  CCM wametaharuki. Huko vijijini hali si shwari. Watu wamechachamaa. Wamesema liwalo na liwe, CCM hairejei madarakani, na hawa ni wale maskini waliozoea kudanganywa kila ufikapo uchaguzi mkuu. Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Masasi, amenukuliwa akisema hajawahi kuona uchaguzi mgumu kama huu. Amesema wana-Masasi wamegawanyika, haswa wanachama wa CCM, kila mmoja yuko kwenye kundi la aliyekuwa mgombea Ubunge na Udiwani wakati wa kura za maoni. Lakini wote wamesema kwamba kura kwa CCM hazitatolewa kwenye Jimbo la Masasi; kura zote, Ubunge na Udiwani, zinaenda upinzani. Wamesema imetosha, viongozi waliowataka kuwachagua wameenguliwa na NEC, wamepitishwa mavuvuzela. Haya ndiyo madhara ya CCM NEC kutaka wabunge na madiwani ambao HAWATATETEA maslahi ya wananchi kwenye bunge lijalo na mabaraza ya madiwani. Wananchi wameshtuka, wamesema HATUDANGANYIKI!

  Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alipotabiri upinzani "wa kweli" kutoka ndani ya CCM, hakueleweka. Alichomaanisha ni kwamba, upinzani huo ungeletwa na WANACHAMA wa CCM, na si viongozi wanaokimbilia kambi za upinzani. Wanachama wanakitaka chama chao, wanakipenda, lakini wao ndio wapinzani wakuu, wenye kutaka mabadiliko. Hii ndiyo siri ya CCM kushindwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu, kwa kuwa wamewadanganya wananchi miaka nenda rudi, sasa wananchi wamechoka.

  Na hiki ndicho chanzo cha CCM kuajiri mamluki wengi wanaokuja humu ndani kujenga HOJA ZA KIPUMBAVU kwa nini CCM irejeshwe tena madarakani. Hata mimi ningekuwa na "channel" ya kifisadi, nikawaambia wahusika wa kampeni, kwamba naweza kuja kuijengea CCM hoja humu ndani, ningemwagiwa mabulungutu ya fedha, ili mradi tu nimekuja kujenga HOJA ZA KIPUMBAVU na KIFISADI!

  Tunawajua mamluki. Binafsi sitawajibu tena, lakini najua watajibu hoja yangu hii ili nionekane sijui nisemalo.

  Ukweli ni kwamba, mkojo hauachi kuwa mkojo kwa kuwa tu umetiwa sukari!

  -> Mwana wa Haki

  2010 HATUDANGANYIKI
   
Loading...