Nimepitia kwenye post zote na nimeona
MtamaMchungu analogic sana na yaelekea wote waliotoa hawana uelewa sana na hii system ya elim ya tz. Kwanza kabisa nia ya kujenga shule za kata kwangu mimi haikuwa kuwapa elimu vijana wa kitanzania la hasha bali ilikuwa ni njia mbadala ya family planning ama niseme fighting VS early marriages. Waliotoa sera za MMEM &MMES walikuwa na lengo moja tu kwamba kama kijana atakaa elim ya msing for 7 yrs bila hata kuwa na mwalim itampunguzia muda wa kufanya uovu kuliko kutokwenda darasan kabisa pia kijana huyu akienda sekondar kwa miaka 4 ukiassume kuwa alimaliza std 7 akiwa na miaka 14 au 15 basi ukimuwekea mingine 4 atakuwa amepevuka zaid na umempunguzia muda wa kuzaaa akiwa mtoto. Lengo la mbinu hii limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya wanafunzi wanaokwenda shule ni wengi sana.
Coming back kwenye ubora wa elimu hapa zoez hili limeshindwa kufanikiwa kabisa kwani hao wanaokwenda kwenye kata wanatoka kwa kiwango kikubwa cha kufeli. sasa hivi tunaona miongoni mwao wahitimu wa seondari wanafaulu kwa kiwango cha daraja la 3 na la 4 kuliko la 1&2.
Ribosome labda nikuulize wewe ulisoma miaka ile ya 80-99? ulionaje ufaulu wa wanafunzi wa shule za makanisa? Natumaini utasema ulikuwa mkubwa sana na hii ni kweli kabisa. ukiangalia tena kwa makini zaid utagundua kuwa matokeo ya kidato cha nne ni shule za makanisa tu zilizofanya vizuri sana za serikali zile kongwe zilifuatia na za kata ndizo zilizokuwa na mass failiers.
Hata matokeo unayosikia Ndalichako akisema ufaulu umeongezeka huwa wanachukulia tu wale ambao kwa kufaulu kwao wanaweza kupata vyeti vya kitaaluma na si kuangalia wamefaulu kwa madaraja gani ya kielim. Ingependeza kama kweli baraza lingekuwa linatuambia ufaulu katika daraja la i ni asilimia ngapi and so on hapo ungeona umuhimu wa kusifia au kutosifia.
Makanisa yamefanikiwa sana kwenye sera ya elimu kuliko serikali jambo ambalo lazima ifike mahali serikali ione aibu. na tean ishukuru zaid ELCT na RC kwa mika le ya zamani walitaifisha shule zao kama pugu, weruweru, ashira girls, machame girls, minaki etc na sasa shule hizi makanisa wanazitaka sijui itakuwaje. manake weruweru wanairudisha kuwa ASSUMPTA COLLEGE upo hapo?
Hizi shule za kata ni hasara sana kwa taifa hili manake hazina tija yyte zaid ya kudelay early marriages basi.