Katika mwendelezo wa ziara ya Jakaya Kikwete nchini Kenya, leo Rais Jakaya Kikwete ametembelea City Hall Nairobi na kukutana na gavana wa Nairobi, Evans Kidero. Rais Kikwete amesema anaamini ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya utaimarika zaidi kama matokeo ya ziara yake.
Pia Rais Kikwete ameahidi kuendelea kuzuru nchini Kenya hata baada ya kustaafu kwake, Rais Kikwete alifanyiwa sherehe ya kukabidhiwa funguo za kuingilia mji wa Nairobi kama ishara ya upendo. Katika hatua nyingine barabara ya milimani(Milimani road) imebadilishwa jina na sasa itaitwa Jakaya Kikwete Road.
Baada ya hapo, Rais Kikwete alitembelea kiwanda cha magari nchini Kenya, General Motors(GM). Kiwanda hicho kimelalamikia Tanzania kuiwekea vikwazo kwa madai kuwa ni kiwanda cha uunganishaji na sio kutengeneza magari hivyo kutopata nafuu iliyopo kwenye ushirikiano wa Afrika Mashariki. Rais Kikwete akijibu hilo amesema ameona na atarudi kuwaambia watanzania ili kuona jinsi gani watasonga nalo mbele.
Huyu jamaa anapenda sifa sijawahi kuona..... bora anaondoka..angekua wakujifunza tungeua mbali mno maana hakuna anachojifunzaga pamoja na kuzurula kote huko.....
.
.
Hapo nadhani kulikuwa na maslahi kidogo, ila ni jambo poa pia. Mimi ni mmoja wa waliochafukwa na Obama, shoga mtarajiwa kupewa jina la barabara ya Ikulu... Ndio maana nahoji na hili pia.
Huyu jamaa anapenda sifa sijawahi kuona..... bora anaondoka..angekua wakujifunza tungeua mbali mno maana hakuna anachojifunzaga pamoja na kuzurula kote huko.....
.
.
Umesema kweli. Kwa mtu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nchi za Nje kwa zaidi ya miaka kumi, kutumikia serikali tatu kwa viwango vya juu.....halafu utendaji wake ukawa hivi......kwa kweli hajifunzi.
Halafu...anawazungumzia Kiingereza Wakenya? Speak of exporting Mercedes Benz to Germany!
Hiyo ya 'Wamarekani woote' kwamba walilaani Bush aliporushiwa [vile viatu havikumpata hivyo hakupigwa] vile viatu si kweli.
Kuna idadi kubwa tu ya Wamarekani waliofurahishwa na lile tukio ingawa pia kuna idadi kubwa ya Wamarekani, bila kujalisha itikadi zao za kisiasa, waliolaani kitendo hicho.