Kikwete atekeleze ahadi zake za serikali kutenga maeneo mbadala ya wamachinga kufanya biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete atekeleze ahadi zake za serikali kutenga maeneo mbadala ya wamachinga kufanya biashara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Apr 5, 2012.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Tarehe 03/04/2012 wachangiaji kadhaa mmetaka kauli yangu kuhusu matukio yaliyojitokeza Ubungo Mataa, sikutaka kueleza chochote kwenye hatua hiyo mpaka kwanza nikutane na wahusika.

  Naomba kuwajulisha kuwa tarehe 04/04/2012 nilifanya mkutano na wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga zaidi ya 500 walioondolewa katika kata ya Ubungo.

  Nilianza kwa kuwaeleza wazi kwamba siungi mkono biashara kufanyika katika maeneo hatarishi na maeneo yasiyoruhusiwa kisheria; hata hivyo nimekutana nao kwa kuwa: Mosi; waliniita hivyo nimefika kuwasikiliza kwa kuwa kazi yangu ni kuwakilisha wananchi wote. Pili; kuwaeleza sijaridhika na namna ambavyo serikali imetekeleza zoezi hilo bila kutimiza ahadi zake kwa wafanyabiashara ndogondogo na bila kutushirikisha au walau kutupa taarifa yoyote wakati wowote viongozi wa kuchaguliwa wa eneo husika. Tatu; kukubaliana hatua za pamoja za kuchukua ili kupata mwelekeo muafaka kwa kuzingatia haki, utulivu na fursa kwa waathirika kuendelea na shughuli za kujikimu bila kuwa katika maeneo hatarishi.

  Matatizo ya wafanyabiashara ndogondogo katika Jiji na Dar es salaam ni maeneo mengine ya mijini nchini ni ya muda mrefu. Mwaka 2005 Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni aliahidi kwamba serikali yake ingeyapatia ufumbuzi wa haraka, hata hivyo Oktoba 2006 mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa baada ya kushughulikia msingi wa matatizo aliongoza uamuzi wa siasa kanyaboya wa kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo kinyume na alichowaahidi wakati wa uchaguzi.

  Maelezo aliyoyatoa Rais Kikwete wakati huo ni kuwa tunawaondoa maeneo yasiyorasmi ili kuwapeleka kwenye maeneo rasmi muweze kupata anuani, mafunzo na mitaji; ahadi ambayo haijatekelezwa kwa ukamilifu.
  Mkuu wa Mkoa ametoa kauli sasa kuwa wafanyabiashara walioondolewa Ubungo waende Machinga Complex suala ambalo nalo ni propaganda kanyaboya kwa kuwa anafahamu kuwa eneo hilo lina uwezo wa kubeba wafanyabiashara takribani 4,500 wakati ambapo wafanyabiashara ndogo ndogo katika mkoa wa Dar es salaam walio katika maeneo kinyume cha sheria ni zaidi ya 150,000. Hivyo, Mkuu wa Mkoa anapaswa kuonyesha mfano wa kuwapeleka wafanyabiashara ndogondogo waliombele ya ofisi yake na maeneo jirani katika Machinga Complex, ambao pekee watajaza. Nimewaeleza kwamba kama suala ni kuvutia wafanyabiashara ili soko lizoeleke watekeleze ushauri niliowapa kwenye vikao husika wa kuongeza ruti za daladala kupitia eneo husika watoe likizo ya kodi kwa wafanyabiashara ndogondogo kwa muda maalum katika jengo husika kama inavyofanya kwa wafanyabiashara wakubwa kutoka nje wanapokuja kuwekeza nchini.

  Nikawaeleza kwamba nilitarajia serikali iweke mkazo katika kukabiliana na vyanzo vya mgogoro wa muda mrefu katika serikali na wafanyabiashara ndogondogo badala ya kujikita katika kushughulikia matokeo pekee. Wafanyabiashara ndogondogo wajaibuka ghafla katika eneo la Ubungo, walianza taratibu huku serikali ikiwaachia na hata kuwatambua kwa njia mbalimbali; hivyo kuwaondoa lazima kutanguliwa na maandalizi ya maeneo mbadala ya kufanyia biashara.
  Aidha, wananchi kufanyia biashara katika maeneo yasiyorasmi ni matokeo ya udhaifu wa muda mrefu wa serikali wa mipango miji na kushindwa kutenga maeneo ya biashara na kuuza kinyemela maeneo machache yaliyotengwa kwa huduma za msingi za kijamii. Hivyo, uamuzi wa kufungua ukurasa mpya kurekebisha hali hiyo lazima uambatane na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara na huduma nyingine za msingi za kijamii.

  Serikali ina wajibu huo pamoja na kuwa biashara inaweza kutazamwa kuwa ni suala la mtu binafsi kwa kuwa wanunuzi wa biashara hizo ni wananchi hususani wa kipato cha chini na hali hii ya kuongezeka kwa uchuuji ni sehemu ya athari za kupungua kwa uzalishaji nchini.

  Hali ya taifa ya kiuchumi na kijamii ni chimbuko la ongezeko la wafanyabiashara ndogondogo Jijini Dar es salaam, mathalani kasi ndogo ya ukuaji wa ajira hasa katika viwanda na kilimo ikilinganishwa na idadi kubwa ya vijana wanaohitimu shule na vyuo; biashara hizo ni sehemu ya jitihada za vijana wenyewe ‘kujiajiri' hivyo kuwaondoa bila mfumo mbadala ni kuchangia katika umaskini.

  Pamoja na hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Manispaa ya Kinondoni, Wizara zinazohusika na Wafanyabiashara wenyewe; nimetoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kueleza hatua iliyofikiwa katika kutekeleza ahadi yake ya aliyoitoa tarehe Oktoba 2010 wakati wa kampeni ya kujenga Machinga Complex nyingine tano; ili kuwe na maeneo ya namna hiyo ya biashara mawili kwenye kila manispaa. Kama serikali ingekuwa imetekeleza ahadi hiyo katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja toka Rais Kikwete aingie madarakani kungekuwa hivi sasa na eneo la wafanyabiashara ndogondogo zaidi ya elfu saba katika Jimbo la Ubungo. Ahadi hii ingeweza kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa kuwa Rais Kikwete alisema mwenyewe Oktoba 2010 kuwa tayari serikali ilikuwa imepata ufadhili wa bilioni 100 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo. Serikali inayokusanya kodi kwa wananchi wote ikiwemo wafanyabiashara ndogo ndogo inawajibu wa moja kwa moja kushughulikia chanzo cha mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati yake wafanyabiashara hao badala ya matokeo. Serikali inatumia nguvu kubwa kwenye kushughulikia matokeo badala ya vyanzo, kama nguvu hizo hizo zingetumika kushughulikia mafisadi wanaoua viwanda na kukosesha ajira kwa vijana au wanaohujumu ruzuku katika kilimo nchi ingepiga hatua kwa haraka zaidi. Hivyo, kusimamia utawala wa sheria kusiishie kwa wafanyabiashara ndogondogo bali nguvu kubwa hiyo itumike pia kuwaondoa katika maeneo yasiyoruhusiwa wafanyabiashara wakubwa ambao wengine wamepora viwanja vya wazi vya umma na wengine wamevamia maeneo ya hifadhi ya barabara.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Kwanini msipeleke Bungeni a bi-partisan bill (wabunge wa Dar mkiwa pamoja) ambao utaelekeza nini kifanyike, wapi, na nani halafu mkatengea fedha mradi huo kisha rais apelekewe ili ufanyike kuwa sheria? hata kama RAis aliahidi at the end ni nyinyi wabunge ndio mnaopanga fedha ziende wapi kwa kutumia sheria (appropriation bill). Vinginevyo, Rais anakuwa na umuhimu mkubwa ambao si wa lazima; anaweza kufanya kile ambacho sheria inamtaka afanye.
   
 3. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,857
  Likes Received: 499
  Trophy Points: 180
  Ndugu Mbunge Wangu Mteule Nashukuru sana Kwa Jitihada Zako!! Najua UGUMU NA Tabu unazozipata Kushauri na Kutetea Mambo yote ya Ukandamizaji!! Ila kwa Dar es Salaam kwa sasa Matatizo yanazidi kuwa Mengi! Tuliowengi hatuwezi kutetea uvunjifu wa sheria, Tunataka sheria zichukue nafasi yake bila upinzani wowote!! Ila na sisi watunza sheria tufanye wajibu wetu!!
  Katika hii dunia nenda Ulaya, nenda Japan nenda kokote!! Huduma za haraka kwa mahitaji ya kila siku ya mwanadamu zimewekwa kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu!! mostly kwenye stand za mabasi, stend za Treni na kwenye Viwanja vya ndege!! sasa kwa sisi kwetu huku na hasa hasa Dar es salaam Maandalizi hayo hayajafanyika Kabisa!! Pia nataka kuwakumbusha Halmashauri za jiji na wengine wengi wanaohusika na planning za maeneo Haya ndio Chanzo kikubwa cha mapato, na sio kulilia mapato ya mabango ambayo sio endelevu!!
  Hivyo basi kwa Haya Machache niliyoyaeleza nashauri yafuatayo kwani bado Hatujachelewa!
  1: Eneo Lote la ubungo lenye YENU BAR HADI KWENYE MTO LITENGEWE FIDIA NA LIJENGWE SOKO KUBWA AMBALO LITAHUSISHA WAFANYABIASHARA WA MADUKA,MASOKO NA VITU VINGINE VINGENE VINGI KWA MAHITAJI YA KILA SIKU YA MWANADAMU
  2: Pia eneo la Mwenge same as Ubungo
  3:pia Manzese
  4: Magomeni naona wamebomoa eneo Kubwa sio Mbaya kama litakuwa na Matumizi hayo pia
  5: Kimara njia ya Bonyokwa, Hapa pia itakuwa ndio Mwisho wa Mabasi ya DART
  Na kwingineko kwingi kadri ya Mahitaji!! Na iwe ni Kosa kubwa kwa mfanyabiashara yeyote kufanya biashara kiolela bila KULIPA KODI NA KUZUIA WAENDA KWA MIGUU!!
   
 4. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Pole sana Kamanda ila endelea kupigana
   
 5. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kikwete aliahidi mambo mengi na sidhani kama anakumbuka achilia mbali uwezo legelege wa serikali yake katika kutimiza ahadi zake, ahadi nyingine ni kujenga reli kutokea tegeta hadi ubungo, tatizo la maji dar kuwa historia hilo alilisema pale Mbagala zakheim, kule kigoma alisema ataibadilisha kuwa dubai, ahadi ya kununua meli tatu kubwa, uwanja wa ndege wa kisasa mwanza, barabara ya serengeti, chuo kikuu butiama, fly overs, magari ya kasi dar na nyingine kibao.
  so sina uhakika na hili la wamachinga kama hata analikumbuka
   
 6. m

  mtolewa Senior Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Serikali inatumia nguvu kubwa kwenye kushughulikia vyanzo badala ya matokeo, hapo rekebisha ni kinyume chake!
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kulikuwa na umuhimu wowote wa kukopi bandiko zima?
   
 8. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hizi siasa za nchi hii unaweza kulishwa hata uchafu ilimradi tu mtu apate pa kupitia
   
 9. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji, Tanzania ni zenye kuweka ukuu katika bunge dhidi ya mihimili mingine ya utawala au walau nchi ambazo kuna mgawanyo thabiti wa madaraka baina ya mihimili ya dola. Tanzania muhimili wa rais na mhimili wake wa utawala una nguvu kuliko wabunge, ingawaje Rais ni sehemu ya bunge. Kuna mipaka ya katiba hii mbovu kuhusu ni miswada ya aina gani ambayo mbunge anaweza kuiwasilisha kama miswada binafsi au bunge linaweza kuwasilisha kama miswada ya kamati. Pendekezo unalolitoa lingewezekana kirahisi katika nchi ambazo bunge na wabunge wana mamlaka makubwa juu ya bajeti, sio Tanzania. Hata hivyo, kuna njia nyingine ya kibunge ambayo nimepanga kuitumia ikiwa mamlaka hazitasikiliza katika kipindi hiki cha siku tatu za kuungana na wamachinga katika kudai haki zao. Leo nitakuwa na wamamchinga watakapokuja kukutana na Manispaa ya Kinondoni, najiandaa sasa hivi kuelekea mkutanoni hivyo nitarajea kwenye mjadala huu usiku, kama sitakuwa rumande.

  JJ
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kiini hapa ni suala la tatizo la ajira, tatizo hili ni zito sana na haliondosheki kwa ahadi za kisiasa, wala matamko ya cheap politics ya akina Mnyika. Hakuna snapshots solution kwa matatizo ya msingi kama haya, huo ndio ukweli mchungu. Mojawapo ya misingi ya kujenga uchumi bora ni kuwa na division of labor, kuwa na labor capacity, mitaji na mipango bora, to mention a few. Huezi ukakwepa kutatua matatizo kisayansi..kutetea baunsa anayezunguka kuuza nyembe za mia mia au maji ya kunywa, eti apewe eneo la biashara is just ridiculous, nlitegemea ninyi watu wa upinzani mna maono kidogo kumbe ndio walewale. Suala la msingi ni kukaa chini na kuishauri serikali kuhusu long-term plans za kutafuta nafasi mpya za ajira, huku ndio kumpiga nyoka kichwani na kumuua, sio hizi blah blah za kujikimu kisiasa, mnaudhi sana aisee.
   
 11. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu umepiga pumba ya mwaka hapa, umeweka wazi upumbavu wako kwa kutosoma hata thread, utafikiri ulikuwa unasubiri sura ya Mnyika ili uanze kutoa povu.
  Soma tena thread soma hoja ya Mwanakijiji soma jibu la Mnyika kwa Mwanakijiji.....
  Mnashauriwa hapa JF muwe mnasoma zaidi kuliko kuchangia.

  Baki na ndoto zako za Tz kuwa kama Ulaya kwa usiku mmoja!
   
 12. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mnyika mnataka kwenda kuandamana? kwa sababu kikwete hatatimiza ahadi au kwa sababu wamachinga wamekatazwa kufanya biashara chini ya mitambo ya gesi na umeme mkubwa
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  It is obvious who is of less intellect here, #uwontwastemytime
   
 14. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Natofautiana na wewe kwenye red kwani hayo yoote unayoyasema serikali inayafahamu. Kama rais asingejua kuna tatizo la ajira asingetoa ahadi anayoizungumzia Mnyinka yaani JK kuahidi kutatiua tatizo la wamachinga. Pia plans serikali inazo nyingi ila isichokuwa nacho ni utashi na strategies za ku -execute hizo plans. Kama kuna utajiri ambao serikali yetu imejaliwa kuwa nao basi ni mipango ya muda mfupi na mrefu isiyoyotekelezeka na badala yake kufanya mambo kwa mtindo wa kushtukiza. Hizi blaha blaha wewe umeziona wapi acha uchuro
   
 15. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Kamanda wangu, hatuombei hayo yatokee ila hatupo tayari kuona Mbunge wetu ukiwekwa ndani kwa kutetea wanyonge. Na kimsingi haupingi wao kuondolewa kwenye maeneo haya ila unapinga kutotolewa kwa mbadala wa maeneo ya watu hao kufanyia biashara zao. Maeneo walioelekezwa hauitaji kuwa umemaliza darasa la saba kugundua kuwa sio friendly kwa watu hao. Kwanza kwa idadi yao, wingi na miundo mbinu ya maeneo husika haiwavuti wateja wengi kama wanavyowapata sasa.
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Mkuu joune Gwalu,
  Alichokisema Abdulhalim umekielewa au na wewe unakurupuka tu kumjibu?

  Hivi kweli Viongozi wanapiganisha kumshauri Raisi atenge eneo la mtu kwenda kuuza Key Holders na Nail Cutters au Mitumba na CD za Ngono? Hivi kweli hiyo ndio Ajira inayowafaa Watanzania?
  Kama tuna pamba hapa Tanzania na Manpower hipo tunashindwaje kuwa na viwanda vya kisasa vya nguo?, Raisi kila siku anasafiri nje, anashindwaje kuwaleta hao wawekezaji wa kweli kwenye sekta ya nguo na Kilimo?

  Watanzania wanaoenda China wanafika mpaka kwenye viwanda na kuweka order na design ya nguo wanazozitaka, serikali inashindwaje kwenda na kuwashawishi hao wenye viwanda waje kufungua viwanda hapa Tanzania?

  Mkuu hizo sio ajira na ni kupandikiza bomu tu, Wabunge wapiganishe viwanda vifufuliwe, kilimo cha kisasa kisiwe cha kisiasa (Kilimo kwanza) bali cha kivitendo, Raisi na Serikali yake pamoja na wabunge waweke nguvu huko kwenye ajira rasmi, ambayo inaweza kumpa mtu uelekeo wa maisha na sio mtu mwenye akili zake timamu na nguvu kushinda juani kutwa nzima akitembeza leso
   
 17. Mtz-halisi

  Mtz-halisi Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Abdulhalim
  umenifurahisha sana, sasa hao wafanyabiashara wadogo wadogo unataka wasubili long term plan!!!! navyojua mimi kwenye malengo kuna short term na long term plan, sasa mtu analala njaa leo unamwambia nina mpango mzuri juu yako subiri baada ya mwaka au miaka 4. njaa ya leo inabidi itatulike leo hata kama ni kwa kupiga debe. Mnyika pambana leo pia jitahidi upambane kesho.
  Mimi najua kunawafanya biashara pale wanajua kuhesabu pesa tuu kwa sababu hata kusoma hawajui, unawasaidiaje hao au ndiyo unawapelea elimu ya watu wazima wakasome waache familia inakufaa njaa.


  Tuombe Mungu atusaidie tuvuke na hapa
   
 18. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  policcm wana kazi moja tu waliotumwa. kubaka demokrasia kama walivyoweza kuibaka huko arusha kwa kushirikiana na idara ya mahakama.
   
 19. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wafanya biashara ndogo ndogo hawapendi kukaa kwenye maeneo yaliyotengwa wanapenda maeneo yasiyo rasmi , si unaona Machinga Complex pale hawataki kuhamia!
   
 20. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kituko!

  Hayo mnayoyaeleza mbona Mnyika kayazungumzia kwenye thread?
  Abdul kaja moja kwa moja na matusi kwa Mnyika utafikiri alimpania huku akisahau anachoeleza ni upande wa pili wa hoja ya Mnyika!

  Machinga ni waathirika wa mfumo kama jamii lazima kuwe na ufumbuzi wa immediate problems hyo haimaanishi hamna long-term plans!

  Machinga wanaenda na soko, hii ni nchi ya kichuuzi saiv chochote sokoni twende ndio tulichoambulia toka kwenye sera za utandawazi, sasa leo hii kuja kuwalaani Machinga nadhani itabidi tufikirie nani wa kupimwa akili hapa!

  Ndio maana nkasema tuwe na utaratibu wa kusoma katikati ya mistari, Mnyika kaeleza vitu vingi kwa pande zote!
   
Loading...