Ulukolokwitanga
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 8,396
- 7,968
Tatizo la ajira nchi hii litatuandama hadi tutakapokuwa na viongozi wenye mtazamo hasi juu ya ukosefu wa ajira. Hapa Tanzania watawala wanaamini kuwa tatizo la ajira litatatuliwa na wazungu kupitia njia ya uwekezaji, yaani wakileta mitaji yao hapa nchini. Kwa nchi ambayo ina inflation ya 20% katika uchumi unaokuwa kwa 7% utawapata wawekezaji matapeli kama wa Dowans. Hata ukienda Marekani na nchi yoyote iliyoendelea the biggest employer is SMALL BUSINESSES. Wenye Salon, Mashine za kuchomelea, viduka vidogo, migahawa, mama Lishe nk ndio sehemu kubwa ya ajira inakotokea hata katika uchumi ulioendelea. Kinachotakiwa ni serikali kuzisimamia vizuri na kuzisajili hizi biashara ndogo ndogo ili ziende katika mfumo ulio rasmi na zilipe kodi. Dalili kubwa kabisa ya uchumi wa hovyo hovyo na ukosefu wa ajira duniani ni uwingi wa wachuuzi au machinga. Kama ulivyosema Mh Mnyika, na nashukuru kuwa umekuwa kiongozi wa kwanza Tanzania kulizungumzia hadharani na kuweka ukweli bila kujali kama unauma, tatizo la ajira ni kubwa kuliko wanasiasa wanavyolizungumzia na hakuna hata mtu mmoja atakuja kifua mbele kutuambia ana takwimu sahihi za tatizo la ajira. Utazipataje kama hata vitambulisho vya utaifa hakuna, hakuna hata national database ya ajira...