Kikwete asema serikali ni ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete asema serikali ni ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 5, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa upande wake, Rais Kikwete alisema kuwa wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini wamemchagua Zitto kuwa mbunge wao, lakini pamoja na hilo Zitto hana serikali, bali Serikali ni ya Chama Cha Mapinduzi haina kinyongo kwa yoyote.
  Alisema ndiyo maana licha ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, imeamua kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wote bila kinyongo wala ubaguzi.

  IPP Media

  Kwa uelewa wangu serikali ni wananchi ambao wana haki yao na kuchagua viongozi wa kuiongoza. CCM imeunda serikali baada ya kushinda uchaguzi na wala si kwamba serikali ni ya CCM. Na ndani ya serikali kuna wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa na watumishi wengine wasio wanachama wa chama cho chote cha siasa.
  Kauli ya Rais Kikwete kusema serikali ni ya CCM anawadanganya wananchi.
   
 2. wasaimon

  wasaimon R I P

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli serikali ni ya wanachi ila chama kinachoshinda ndicho kinapata fulsa ya kuiongoza hiyo serikali. Sasa basi serikali inaongozwa na ccm na wala serikali si mali ya ccm.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hizo ndiyo siasa anazozijua Rais wetu .Na si yeye pekee bali ma CCM yote yanawaza hivi hivi .Kuwaeleza vinginevyo utaiwa mhaini .Kama unabisha ongeza sauti usikie
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Baada ya kufungua barabara alikosa cha kuongea, ikabidi aanze mambo ya uswazi!
   
 5. K

  Kanda ya Ziwa Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  acha waendelee kujifariji kwani kufunmba na kufumbua watakuwa hawana la kujitetea. Yangu macho na masikio ndo hayo!!
   
 6. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kikwete usisahau fedha zilizotumika si ada ya wana-CCM aka Magamba bali ni kodi ya watanzania wakiwamo waliomchagua Zitto Kabwe. Siku nyingine ukifungua barabara au mradi wowote uwashukuru wananchi kwa kulipa kodi unayowezesha ujenzi wa miradi hiyo. Si ilani ya CCM bali ni kodi za wananchi zimewezesha ujenzi huo! Mtizamo lazima ubadilike, ni haki yao na wala si fadhila ya CCM!
   
 7. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kifupi anaukweli ndani yake kwani nchi inaongozwa na chama kilichotengeneza serikali.
  Therefore ilani ya chama hicho ndiyo inyoongoza serikali.
   
 8. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  baba kwa mipasho huyu!!!!
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Rubani wa ndege anapoajiriwa kuendesha ndege maana yake anahodhi kabisa ndege ni yake?
  Kama serikali ingekuwa ni mali ya CCM iweje kuwepo na vyombo na idara mbalimbali za kuilinda na kuiongoza ambazo hazina itikadi za kichama kama mahakama na vyombo vya usalama?

  Si kila mara ilani ya uchaguzi ya chama kilichoshika usukani wa kuongoza serikali inatekelezeka, na mara kadhaa tumeshuhudia ilani ya vyama vya upinzani kutekelezeka kama madai ya katiba mpya, suala la posho nk.
  Hayo yanadhihirisha maana ya serikali nini.

  Hizi semina elekezi wanaelekezana nini?
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wanachama wa ccm wanakawaida ya kuhodhi kila kitu na kuona wanapowajibika kwa wananchi ni hisani kwa wananchi. Tunahitaji Chadema waongeze kasi kuelimisha umma wajue majukumu ya serikali kwa wnanchi.
   
 11. MANI

  MANI Platinum Member

  #11
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Zed tatizo hapa ni kuwa elimu ya uraia haipo kwa wengi na watu wanashindwa kutofautisha kati ya wajibu wa serakali kwao.Kama serekali inakusanya kodi niwajibu kutoa hizo huduma kwa wananchi wake sasa serikali haitufadhili kwa kujenga barara wala shule kwani hata serekali ya mkoloni ilifanya hivyo. Ni jukumu letu kuelimisha umma nini wajibu wa serakali kwao.
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Somo la uraia Chadema walishaanza katika mikutano yao kwamba yanayofanywa ni serikali ni stahiki yao na ni kutokana na kodi zao. CCM haipendi somo la uraia litolewalo na Chadema ndio maana wanapinga maandamano na mikutano ya Chadema kwa nguvu zote
   
 13. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wasiwasi wa kupopolewa
   
Loading...