Kikwete arejea kukagua mafuriko Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete arejea kukagua mafuriko Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Halisi, Dec 22, 2011.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  [FONT=&amp]UNITED REPUBLIC OF TANZANIA[/FONT]
  [FONT=&amp]DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS[/FONT]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Telephone:[/FONT][FONT=&amp]255-22-2114512, 2116539[/FONT]
  [FONT=&amp]E-mail: [/FONT][FONT=&amp]press@ikulu.go.tz[/FONT]
  [FONT=&amp]Website: www.mawasilianoikulu.go.tz[/FONT]
  [FONT=&amp]Fax: 255-22-2113425[/FONT]

  [/TD]
  [TD="width: 118"][/TD]
  [TD="width: 266"]
  [FONT=&amp]PRESIDENT'S OFFICE,[/FONT]
  [FONT=&amp] THE STATE HOUSE, [/FONT]
  [FONT=&amp]P.O. BOX 9120, [/FONT]
  [FONT=&amp]DAR ES SALAAM[/FONT][FONT=&amp].[/FONT]
  [FONT=&amp]Tanzania[/FONT][FONT=&amp].[/FONT]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [FONT=&amp]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI[/FONT]
  [FONT=&amp]RAIS KIKWETE AKATISHA MAPUMZIKO KUWAJULIA[/FONT] [FONT=&amp] HALI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO DAR[/FONT] [FONT=&amp]Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011, amekatisha mapumziko yake ya sikukuu kurejea Dar es Salaam kujionea mwenyewe madhara na uharibifu wa mafuriko pamoja na kutoa mkono wa pole kwa waliopoteza ndugu zao, kuumia ama kuharibiwa nyumba zao na mafuriko hayo.[/FONT] [FONT=&amp]Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K Nyerere akitokea kwenye Mbuga ya Wanyama ya Serengeti, mkoani Mara, ambako alikuwa anapumzika, Rais alilakiwa na mawaziri na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Said Mecky Sadiq.[/FONT] [FONT=&amp]Mheshimiwa Sadiq amemweleza Mheshimiwa Rais kuhusu hali halisi ya mafuriko katika Mkoa wa Dar es Salaam na madhara yake akisema kuwa mpaka sasa watu 20 wamethibitishwa kupoteza maisha na watu wengine 68, wakiwamo wakazi 66 wa Wilaya ya Ilala, wamejeruhiwa kutokana na mafuriko hayo.[/FONT] [FONT=&amp]Mkuu huyo wa Mkoa pia amemweleza Rais Kikwete kuwa watu 4,909 wamepatiwa hifadhi ya muda katika sehemu mbalimbali, hasa katika shule za msingi na sekondari, baada ya nyumba zao kuharibiwa katika mafuriko hayo yaliyotokana na mvua zilizoanza kunyesha tokea usiku wa kuamkia Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu hadi leo.[/FONT] [FONT=&amp]Amemwambia Rais Kikwete kuwa kata zote 30 katika wilaya zote tatu za Mkoa wa Dar es Salaam zimeathiriwa na mafuriko hayo na kuwa wengi wa watu ambao nyumba zao zimeharibiwa na kubomolewa katika mafuriko hayo wamehifadhiwa na wanapatiwa huduma na Serikali.[/FONT] [FONT=&amp]Mara baada ya kupatiwa maelezo hayo, Rais Kikwete amepanda helikopta kukagua maeneo yote yaliyoathiriwa na mafuriko hayo hasa yale yaliyoko katika Bonde la Mto Msimbazi na baada ya ukaguzi huo alikwenda kuwapa mkono wa pole na kuwajulia hali wananchi waliopewa hifadhi katika Shule ya Msingi ya Mchikichini katika Wilaya ya Ilala.[/FONT] [FONT=&amp]Kuna kiasi cha watu 1,900 katika shule hiyo na akizungumza nao, Rais Kikwete amesema kuwa alikuwa amefika kuwapa pole kwa matatizo yaliyowafika. "Nimekuja kuwapeni pole na maafa yaliyowafika. Nimekuja kuwahakikisheni kuwa tupo, tuko nanyi na tutahakikisha kuwa mnapata huduma zote za msingi za chakula, za afya, za usafi kwa maana ya kila aliyeko hapa kupatiwa godoro, blanketi na chakula."[/FONT] [FONT=&amp]Rais Kikwete pia ametumia nafasi hiyo kuwaagiza wote wanaohusika na mipango ya miji na usalama wa wananchi kuhakikisha kuwa wanatafuta na kupata majawabu ya kudumu ya watu kuathiriwa mara kwa mara na mafuriko kwa sababu ya kujenga na kuishi katika maeneo ya mabonde.[/FONT] [FONT=&amp]"Fanyeni uamuzi wa kutokujenga tena ama kutokurejea tena katika maeneo ya mabonde. Fanyeni uamuzi wa kutokuishi katika mazingira ya mashaka ya usalama wenu na wa familia zenu kila mvua inaponyesha. Hasara mnaijua zaidi nyie, hasara za kujenga upya, hasara za kusafisha tope, hasara za kununua samani mpya kila mvua inaponyesha," Rais Kikwete amewaambia wananchi hao.[/FONT] [FONT=&amp]Rais amewaagiza maofisa wanaohusika kuwasaidia watu wanaoishi mabondeni kuhamia sehemu nyingine. "Napenda kuwahakikishieni kuwa tutawapatia maeneo ya kuishi nje ya mabonde na maofisa wote wanaohusika wako hapa wamenisikia."[/FONT] [FONT=&amp]Rais Kikwete pia amesimama kwa muda kwenye Barabara ya Morogoro na kuwajulia hali walioathiriwa na mafuriko katika eneo hilo ambao wameweka makazi yao kwenye miti iliyoko barabarani hapo baada ya nyumba zao kuzingirwa na kuharibiwa na maji katika eneo hilo.[/FONT] [FONT=&amp]Kwa mujibu wa uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam eneo la ekari 200 na lenye uwezo wa kutoa viwanja 2,800 limeainishwa katika eneo la Mbopo, Wilaya ya Kinondoni, kwa ajili ya kutoa viwanja kwa walioathiriwa na mafuriko hayo baada ya wenye viwanja hivyo kulipwa fidia.[/FONT] [FONT=&amp]Imetolewa na[/FONT][FONT=&amp]:[/FONT] [FONT=&amp]Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais[/FONT][FONT=&amp],[/FONT] [FONT=&amp]Ikulu,[/FONT] [FONT=&amp]DAR ES SALAAM[/FONT][FONT=&amp].[/FONT] [FONT=&amp]22 Desemba, 2011[/FONT]

  View attachment 43892
   

  Attached Files:

 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MZEE MKAPA ALITUACHIA UWANJA WA KISASA WA MPIRA ILIOTUWEKA KWENYE RAMANI MPYA KIMCHEZO DUNIANI, RAIS KIKWETE CHONDE TUACHIE 'KIKOSI CHA ZIMAMOTO, MAJANGA NA UOKOZI' CHA KISASA KOTE NCHINI MAANA KATIBA NAONA IMEKUGOMEA

  Jeshi letu la Wananchi (JWTZ) nikiona hivi; guys I am now proud of you.

  December 2011 22:38 [​IMG]

  Tanzania People's Defence Forces personnel ferry Jangwani Valley residents out of their flooded homes where they were trapped for hours after a downpour lashed Dar es Salaam yesterday. PHOTO | said POwa

  Rais Kikwete waongezee Kikosi Cha Zimamoto na Uokozi utaalam na vitendea kazi vya kisasa ili kikosi hiki nacho kipate kuheshimika, malipo na marupurupu kuboreshwa na kufika mahala ikawa nayo pia ni taaluma ya kugombaniwa mojawapo nchini.

  Kwa nini tuwaache Kikosi chetu cha Zimamoto na Uokozi KIPIGIKE KWA KILA KITU KIASI HIKI JAMANI????????????????????

  Mhe Rais, ombi hili kalichukue na kusimamiwa na wewe moja kwa moja toka ikulu magogoni ili baada ya miaka miwili toka sasa tuone:

  1. Vikosi hivi vikidhaminiwa kama wenzao tulivyowaona kwenye TV za Ulaya miaka hiyo kule World Trade Centre,

  2. Vituo vya faya vikiongezwa hadi ngazi ya kata ili tujihisi kweli tuko salama wakati wote na mali zetu,

  3. Uitishe michango ya kufa mtu ili kila kata kiwe na walau magari mawili ya zimamoto na uokozi kote nchini,

  4. Tuone Meli na Boti kibao za kisasa zaidi kote baharini na Ziwani tayari kwa kazi ya uokozi wakati wote,

  5. Miundombinu ya kupatikana maji ya kuzimia moto ifanye kazi masaa 24 ili vijana wetu wasiwe ni wenye kufedheheka kila wakati na kuishia kupigwa mawe na wananchi wenye hasira pindi wanaposema ukweli kama ulivyo kwamba ama hawana maji ya kuzimia moto au wameishiwa mafuta.

  6. Kikosi cha zimamoto, majanga na uokozi kisomeshwe kwa sana na hata kuombewa kufanya kazi walau kwa mwaka moja chini ya vikosi vya nchi nyingine zilizoendelea ili wapate kugema maarifa zaidi kuja nayo nyumbani kutusaidi (ni dhamani gani ya mali na maisha tunaopoteza kila mwaka nchini bila hata mtu yeyote kuonekana kushtukia????)

  7. Jinsia ipewe kipaumbele ili wakinamama wakakamavu nao wajumuishwe mle,

  8. Zile ndoto za za Kapten Chiligati kujengwa kwa Chuo Kikuu cha Zimamoto, Majanga na Uokozi nchini ufikiriwe kwa haraka zaidi lakini bila kutawanya bure rasilmali finyu tulizonazo cha msingi:

  i. tuanzishe mafunzo ya certificate, na diploma yake pale pale DIT na Digree zote zifanyikie kule kule Engineering Mlimani

  ii. tunahitaji uokozi wenye weledi mkubwa hasa ukizingatia kwamba tumeanza kuchimba na kusambaza gesi kote nchini,

  iii. tunawahitaji waokozi kwenye mashimo migodini ili tusiwe ni watu wa kulia kila siku

  iv. Kikosi cha Zimamoto, Majanga na Uokozi kiwe na wataalam Wapigambizi zaidi ya 400 kila mwaka kwenye umri mbalimbali za kutegemeka

  9. Mhe Rais, nikiwa bado nakumbuka Jeshi la Msumbiji ilivyoonyeshwa ikimuokoa mama mmoja na kitoto chake kwapani wakiwa juu ya mti baada ya mafuriko kutanda kote nchini humo, natamani kukuona ukitumia kodi zetu kuwanunulia hawa hawa kikosi cha zimamoto hii inayodharaulika na kudhalilishwa sana nao wawe na helikopta kwa ajili ya kazi za uokozi.

  10. Fungua milango kisera na kisheria ili ushiriki wa taasisi binafsi kwenye kazi ya uokozi kwenye Majanga na Uokozi uwe mkubwa zaidi, wa kiushindani zaidi, muitiko murua na wa ksi zaidi na gharama nafuu zaidi katika sekta hii.

  11. Kuwepo na taasisi maalum sawa tu na EWURA itakayokuwa refarii wa shughuli zote za Majanga na Uokozi nchini pamoja na kusimamia ushiriki wa taasisi binafsi yote nchini.

  NB: Hatupendezwi nchi yetu kuwa ombaomba hata kwa maambo ambayo tukijipanga vizuri kwa vipaumbele vyetu kama taifa wala hatuhitaji msaada toka nje.

  Idara ya Zimamoto, Uokozi na Majanga ukiangalia bajeti yake bungeni ni vichekesho vitupu, bure kabisa na wala hamna kitu pale!!!
   
 3. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Yan anaenda kupumzika wakati watanzania wengine wako makazini? Dah huo ni mfano wa kuigwa? Km angekuwa likizo sawa ila mapumziko tu i dont understand, eti MAPUMZIKO YA SIKUKUU wakati haijaanza, basi wangetuambia wote tukapumzike.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,136
  Trophy Points: 280
  ..haijawahi kuanguka mvua kubwa kiasi hiki in the last 57 yrs.

  ..pamoja na hayo unaambiwa Raisi alikuwa anapumzika!!
   
 5. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  Zile picha zilikuwa kweli?Dah
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Baada ya kutembelea mafuriko leo atarejea kwenye mapumziko au?
   
 7. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Dah mi mwanzoni nilidhani hali si mbaya sana mh ila kwa sasa naona ni critical aisee na nashangaa hatua za haraka hakuna....mambo yanapelekwa taratiiibu
   
 8. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,155
  Likes Received: 3,346
  Trophy Points: 280
  Anapumzika kwa kazi ipi haswa aliyoifanya?
   
 9. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hahahahahahaaaa yan hilo si la kuuliza tena ukizingatia sikukuu ndo hata haijaanza teh*
  Kwanza utakuta alisharudi huko Long time we unadhani yuko jijini kumbe keshaenda "kupumzika"
   
 10. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Kucheka Cheka
   
 11. e

  elly1978 Senior Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sikukuu za mabwenyenye huwa ni weeks siyo kama hohe hae kaa sisi, tunaojua sikukuu ni tar 25 dec, hata mabox hatufungui
   
 12. e

  elly1978 Senior Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Shiiii, ametoka uganda majuzi ambapo alitoa hotuba ndefu, nzuri na kuvutia, sasa atakuwa anechoka sana,
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Tatizo siyo watu wanaoishi "mabondeni" bali ni watu wanaoishi "magogoni" - M.M. Original Quote...
   
 14. regam

  regam JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni bora hata huyo mtoa taarifa asingesema kuwa Raisi alikuwa kwenye mapumziko! Tena anatanabaisha kuwa alikuwa kwenye mapumziko ya sikukuu kwenye mbuga za wanyama serengeti. Yaani sikukuu haijaanza, kuna mafuriko halafu mtu anaenda kupumzika?
  Kweli mkere una mambo? Kila kukicha anawaza shughuli tuuu!
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Game Theory 1 alileta taarifa ya JK kuwa likizo watu wakampinga.
   
 16. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Teh ndo tumejizoelea mkuu tutafanyaje na ndo mazingira halisi?
   
 17. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Ndo ujue hata wewe unaweza kuwa Mkuu wa Kaya
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Angalia Presidential Suite ambayo ni 22,000$ per day......linganisha na hali halisi ya maisha mtanzania wa dodoma pale vijijini kabisa ambaye anakosa panadol sh 100 tu!!
   
 20. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Mh! Haya weeeeee.......
   
Loading...