Kikwete anamshinda Membe kwa safari za nje ya nchi

Fareed

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
328
135
Rais Jakaya Kikwete, mkwea pipa maarufu, sasa amepanga kufanya state visit Afrika ya Kusini mwezi ujao (19 to 20 July 2011). Hii itakuwa ni mara ya 3 kwa Kikwete kutembelea Afrika Kusini mwaka huu.
Safari za nje za kila mara za Rais huyu mpenda kupanda ndege, zimekuwa zikiigharimu taifa mabilioni ya shilingi kutokana na kulipa gharama za usafiri za Rais na delegation yake, gharama za malazi, pamoja na posho za safari.

Mwaka huu peke yake, Kikwete ameshaenda Afrika Kusini (mara 2), Switzerland (mara 2), Egypt, Mauritania, Ethiopia, Uganda, Seychelles, Malaysia, etc. Amekaa nje ya nchi kwa zaidi ya mwezi mmoja, kama ukihesabu siku zote alizo safiri na kuzijumlisha. Kikwete anaendelea kuwa mzigo mkubwa kwa taifa na kulisababishia hasara kubwa sana zisizo lazima.

Kwa mwenendo huu, Rais wa nchi amekuwa anasafiri mara nyingi hata kumshinda Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye kazi yake ndiyo inamtaka asafiri kila mara.
 
Du kama sindbad vile,uchumi wenyewe kama wa ugiriki patamu hapo.ukitaka kula sharti uliwe kidogo hahahahahaaaaaaaaaa
 
jamani atakae muona huko aliko amwmbie nyumbani wamekata umeme na maji arudi tunateseka
 
jamaani mmesahau kuwa mwenzenu anaandaa mazingira ya makazi baada kuachia kiti? kwani kuna uwezekano mkubwa akafunguliwa kesi za ufujaji wa mali za uma so anaandaa makazi!
 
Polisi wanaua raia bila kosa, wananchi kimyaaaa.... totoroooooo
Wanajeshi wanatembeza mkongoto, wananchi kimyaaa totorooo
Rais na wapambe wake wanavunja hazina na kupora mabilioni, wananchi kimyaaa, totorooo
Umeme hakuna na hamna anayejishughulisha ktatua tatizo, wananchi kimyaa totoroooo
Wanajitokeza wabunge wanasema mshahara wao ni mkubwa sana wapunguziwe, wananchi kimyaaa totorooo
Sasa unataka viongozi waogope nini... badala ya kuponda mali kabla hawajafa!
Waacheni bwana ni 'haki yao' kwani hamna wa kuwafanya lolote.
Si umeona bunge limetuma chapchap ujumbe UK kufuatilia fedha za rada na wakati kuna matukio chungu nzima yanatokea hapa hapa
Tanzania lakini hata kuulizia hawauliziii...
 
Kaka Mkweree si wakumfananisha na Mbembe! Hakuna wa kufanana na yeye kwa sasa duniani! Amesafiri mara 311 tangu aingie magogoni mwaka 2005!!
 
Membe amesafiri mara ngapi? kuna mtu yoyote anyejua orodha ya safari za membe atuwekee
 
Fareed inaelekea huna kazi ya kufanya ndio maana kila siku unakesha kuhesabu safari za Rais, wewe ulitaka asifanye kazi zake za urausi. Kwa kweli unaboa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom