Kikwete Amedanganya wananchi hawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Amedanganya wananchi hawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mkongo, Nov 21, 2009.

 1. mkongo

  mkongo Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania haki iko wapi? Tutaiendekeza CCM mpaka lini?

  Najumuika Ulingoni kuwaonyesha link yenye video ya yaliyotokea mwaka 1996 huko Bulyanhulu wakati wananchi walivyoondelewa kwa nguvu bila huruma na uvunjaji wa haki, tena nchini kwao kumbuka serikali yao walioiweka madarakani ndiyo waliofanya vitendo hivi.

  Pia Rais wao Jakaya Mrisho Kikwete amewadanganya wakati wa kampeni... nasema NAMCHUKIA kwasababu ni Mnafiki.

  Hata faida inayopatikana na machimbo haya haiwafaidishi wananchi hawa ni kwa viongozi wachache ambao wanapenda kujinunulia magari ya kifahari. kuishi maisha ya kifahari, kujilipa mishahara minono, wenye sifa ya umimi na sio mimi na wewe na yule. Jamani tuwaonee huruma asilimia kubwa ya wananchi vijiji wanaoishi kwa maisha ya tabu.

  Asante kwa waliotengeneza video hii kutuonyesha yaliyotokea huko. Mimi binafsi nimesikitika sana na imenigusa.

  Asante

  [ame]http://vimeo.com/7690704[/ame]
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Nov 21, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Karibu sana ndugu, naona umekuja na kasi mpya, post ya kwanza tu imegonga Ikulu!
   
 3. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Video yenyewe ipo wapi?

  Sie tulikuwa na hasira kuliko zako hizo kule Nyenzi.com mpaka BCS, ila tumepoa kwa sasa hatuna misimamo mikali. Tumegundua kuwa waTanzania ndo wajinga kukubali kudanganywa.

  Asante mkuu
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Aisee video hii inasikitisha sana...watu wanaposhika silaha msifikiri hawana akili
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mwanangu Mkongo haya ndiyo mambo yaliyomtoa Naomi machozi, Tanzania is a police state, hatuwezi kubisha.

  Inabidi watu wapelekwe mahakamani, hata ikibidi katiba kurekebishwa ili watu waweze kuisue serikali.

  Wanasheria wa bongo mbona wamelala?

  Huyu Generali Kiwelu Kawajibishwa vipi?

  Kuna watu katika video wanasema "Muheshimiwa tunaomba turuhusiwe kuuliza maswali" "Tanzania nchi huru uhuru wenyewe ndio huu?" "Tanzania nchi ya amani amani yenyewe ndiyo hii?"

  Inatia huruma sana!
   
 6. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2009
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,126
  Likes Received: 23,736
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha hii site enzi hizo ilkuwa bomba kishenzi, hivi iliishia wapi ?.
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nilisikia tetesi kuwa Che Nkapa ni shareholder katika kampuni ya dhahabu ya Kahama.
  Baada ya kuangalia hii video naelewa kwa nini nguvu zilitumika chini ya utawala wake kuwafukuza wananchi hao.
   
 8. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  Naomba niulize jamani tumlaumu nani? kama Wasukuma wenyewe wenyeji ndo wanaongoza kupigia kura CCM, jamani hivi Wasukumu hata nusu ya namba yao wangepigia kura upinzani si wasingejikomboa jamani? Hao wawakilishi wao wa CCM wakina Chenge na Mwanyika wamewasaidia vipi au wamejishibisha bila aibu na kuacha umaskini huu ukiendelea na ajabu Chenge ataingia bungeni tena 2010! Endeleeni kulia tu labda muendelee kuua albino kwa vile kwenu nyie ni rahisi zaidi ya kujikomboa (samahani nitakayemkwaza) kuondoa CCM madarakani wakija Chadema na CUF ku washauri mnadai ati chama cha Wachagga na Uislamu kwani hawa watu si Watanzania wenzenu? wapeni nafasi muone kama watawaangusha au endeleeni kula propaganda huku mkimezwa na kufisidiwa! Inasikitisha
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Nov 21, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Bluray, acha usingizi huo! Hivi unafikiri kwamba kwa sasa huwezi kuishtaki Serikali mpaka Katiba ibadilishwe? Kasome The Government Proceedings Act uone kawa huwezi kuishtaki Serikali!
   
 10. mkongo

  mkongo Member

  #10
  Nov 22, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  FairPlayer huoni hiyo video hapo mwanzoni?
   
 11. T

  T_Tonga Member

  #11
  Nov 22, 2009
  Joined: Jul 24, 2007
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani pale wapemba wakiikataa ccm si mnaona ni wajinga sasa ndio muone wapemba wameuliwa na nyinyi mlikuwa kimya bado mtaipigia ccm mkipewa pombe na flana tu basi mmeridhika amkeni bado mmelala mkidanganywa tu kidogo basi sasa hiyo ndio hali muuone wapemba wao wameshajijua na ndio maana ccm anafanya afanyalo pemba hana kitu
   
 12. a

  alibaba Senior Member

  #12
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Picha na taarifa kama hizi husikitisha na kuhuzunisha sana, Mbali na ubadhirifu wa mali za Taifa uliojitokeza kwa Nguvu mno wakati wa uongozi wa Mkapa pia Wananchi wamepoteza maisha kwa sababu za kisiasa au za kujaribu kutetea baadhi ya haki zao, Vyombo vya dola vimeariwa kutumia nguvu ambazo zimesababisha vifo. Kama tunavyoona katika video hii, na kadhaa zimepita kama Pemba na Mwembe Chai. Uongozi wa Serekali iliyopo unaelekea umeshindwa kuchukua hatua zozote na Wanasheri wetu inaelekea wanaogopa kutia Kitumbua cha Mchanga. Kwa hali hiyo labda tujaribu kufungua Kesi nje ya nchi katika Mahakama za kimataifa ili kuongeza Presure/mbinyo kwa viongozi kuwa they can run, but they cant hide/Wanaweza kukimbia lakini hawawezi kujificha.
   
 13. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Hii video ya 2008, lengo la kuitengeneza sijui kama limefikiwa zaidi ya hzi posts za blogs, it seems was posted from Canada ......


  Kwa ya Buly Mining Report zipo kibao ikiwemo "Special Investigation Report" ya 2002http://www.miningwatch.ca/sites/miningwatch.ca/files/Bulyanhulu.pdf

  Council of Canadians, Sept 27, 2001 http://www.canadians.org/  Documentary Film ya Mattias Ylstra, Stan van Houcke, 2004
  http://www.ylstra.nl/bulyanhulu.html

  Just you can see jinsi gani hao hao Wazungu wanavyafanya juu ya tabu zetu....
   
 14. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Bila ya kuingia msituni hakuna haki itakayopatikana. Naona maneno matupu hayazai kitu.
   
 15. mkongo

  mkongo Member

  #15
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania ni waoga sana... sijui kama swala la msituni litatokea
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Huko misituni mnataka kwenda kulina asali ama kutafuta kuni?
   
 17. B

  Boca1 Member

  #17
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Che Nkapa alikuwa ni shareholder katika Mabangu Investiment ambayo ndiyo ilikuwa Prospecting Lincense Holder ya eneo hilo na kuna uwezekano kuwa bado wanahold shares zoa kwenye maning Company iliochukuwa jukumu la uchimbaji. Mabangu Investment inamilikiwa na Prof. Mbilinyi
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hivi Bongo wanasheria wapo??
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahaha sometimes unachekesha Kibunango :)
   
 20. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Acha kudhihaki watu bwana. Umeelewa fika kuwa wanasema nini. Mimi nadhani wewe u mmoja wa watu wanaolinda 'status quo' ya wanaodhalilisha wananchi.
   
Loading...