Kikwete akutana na vipeperushi vya kumkataa Dodoma!

Mh! huu upuuzi..ndani ya CCM kuna mtu wa kumnyooshea RAIS kidole? Nani asiejipenda? Hivi unafikiri kazi ya maafisa wake wa usalama wangekua hawajawachinjia baharini hivyo vitoto vya mafisadi? Tatizo letu hii demokrasia tuliopewa hasa kipindi hiki tunaitumia vibaya sidhani km kila kitu akiingilie RAIS huo utakua udikteta....Hii habari haina ukweli wowote ukizingatia hao waliotajwa kusambaza vipeperushi hawana uwezo huo ata chembe unless mtoa mada ana ajendA ya siri kuwavuruga hao watoto ili yawakute ya ULIMBOKA
 
Nashukuru Mkuu wa ilmu ya Katiba, ila sijawahi kuongea kama mlevi katika kutoa maoni yangu, nadhani kuna nchi jirani yetu(sitaki kuitaja kwasasa) kuna kiongozi baada ya kuchaguliwa akavunja chama chake kutokana na kashfa za rushwa, any way, Katiba yao ni tofauti na yetu inawezekana, Ila haya yote yanawezekana, KATIBA muhimu ni ya nchi na siyo ya vyama.
na mimi hapo nimekuwa nazungumzia katiba ya jamhuri ya muungano ya tanzania ya mwaka 1977 haihusishi chama chochote! "Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa
kodi yoyote ya Serikali.
 
Mi nadhani ni demokrasia imekua ndani ya magamba lakini wanatupa picha gani sisi tunamuona ye mpango kumbe ugambani hakubaliki kwa hiyo walituuzia mbuzi guniani? Mi nitoe ushauri tu kwa vyama vya siasa mwenyekiti asiwe front line awe ni mtu wa kusimamia mikakati na kuimarisha chama mfano uchaguzi wa marekani tangu kampeni wala hajaonekana kimbelembele mwenyekiti wa demo,wala wa repub,na sijaona manguo ya kijani wala makaki mambo mengine kumingle na vijana kwenye mikutano mpaka ya kusutana heshima itatoka wapi
 
kama ilivyotokea kwa Mikhail Gorbachev, aliyekuwa rais wa RUSSIA mwaka 1991.

Mkuu, je URUSI ulikuwa katika hali gani baada ya kumuondoa Mikhail Gorbachev madarakati unceremoniously?? utawala ndani ya Kremlin ukawa unaendeshwa na remote controls za "RUSSIAN OLIGARCHS" tusipokuwa makini na kutumia busara basi Taifa letu litajikuta linaelekea huko huko - mimi sio mtume au nabii ninacho fanya niku-compare na ku-contrast matukio yaliyo wahi kuyakumba mataifa mengine!!!
 
Ni kweli kiongozi nakubaliana na wewe, vipandevipande baada ya M. Gorbachev nikivitaja utashangaa sana....naomba niishie hapo hapo.
 
Na wewe unaamini Lowassa anaweza fanya huu ni upuuzi wa KINA Riz, Nape, Makonda et al, chini ya ushauri wa Cyprian Majura Musiba.. Majura utaiua CCM kwa njaa zenu, Makonda kubalini 3-0, subiri ni NAFASI za kuteuliwa hamchaguliki

Kwani kuna hasara gani Majura kuiua CCM ??? Wewe ni Munafiki unataka CCM isife??? Wacha Majura aiue CCM ni faida Kwa upinzani
 
Ningekuwa mimi JK, wakishanichagua tu, navunja chama naanzisha chama kingine na kuwatosa hao wote, na kukifuta kabisa hicho chma kinachotaka kufanya uhaini ambao hatujawahi kuusikia hapa Tanzania tangu enzi za TAA

Kweli ni bora angewataimu kwa kusubiri achaguliwe kwanza halafu anawamwaga kwa kutumia katiba yao ya CCM bila kuangalia usoni kwao kwani atawaonea huruma ambayo baadaye itakuja mgeukia yeye mwenyewe, au angefutilia mbali uongozi wote uliochaguliwa juzi na kupiga marufuku waliohusika kwa kipindi cha miaka mitano ili 2015 wasitie guu kwenye uchaguzi
 
na mimi hapo nimekuwa nazungumzia katiba ya jamhuri ya muungano ya tanzania ya mwaka 1977 haihusishi chama chochote! "Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa
kodi yoyote ya Serikali.

Mkuu hapo kwenye red Lowassa hapiti kwani kaficha vijisenti Uswiss na havilipii kodi
 
Hapo kwenye red nafikiri panathibitisha ni kwa nini wewe na CCM mko sawa sawa , kaza mwendo jamaa yangu umeshanata masikini hata kujielewa hauwezi kujielewa....!!!!

cHaDeMa.......

enyi mnaojiita wapinzani acheni siasa chafu hizi.

Hivi nani asiyejua kuwa huo nimpango wenu wakuyumbisha chama tawala CCM

USHAULI KWA NYINYI UPINZANI UCHWALA
Shughulikeni na mambo ya chama chenu ambacho kwaundani zaidi ni taasisi tu.
 
Mkuu, fahamu tu kuwa uwepo wa vipepeushi hivyo ni ishara tosha kuwa amekataliwa na wanachama wa CCM, jambo zuri kwake ni kuachia hiyo nafasi ya mwenyekiti wa CCM Taifa, as I believe nothing will change AS he will remain the head of the state
Hivi akikataliwa kweli itakuwaje? Sijui mpaka sasa anajisikiaje? Bado ana nguvu ya kuhutubia mkutano? Je atawaambia tena wahame? Au ni upepo tu utapita?
 
Kwa mara ya kwanza nimesikitishwa sana na baadhi ya wanachama ambao wamepania kumdhalilisha Mh.Jakaya, hili si jambo jema hata kidogo, Raisi wa nchi anapaswa kuheshimiwa, hata kama kuna tatizo lolote kwa nini wasilimalize ndani kwa ndani kuliko kuonyesha dharau zilizo kithili. Kama tatizo ni Uraisi wa 2015, whoever is behind this scum ni mtu wa kuogopwa kama ukoma, hatuhitaji vurugu katika TAIFA letu - mtu ambaye anapania kupata URAISI come rain or shine si binadamu wa KAWAIDA hata kidogo.
umeongea vizuri mkuu.mimi nasema tusipokuwa makini kwa jinsi mambo yanavyoenda kwa ujumla tutajuta mbele ya safari.
 
Mkuu, fahamu tu kuwa uwepo wa vipepeushi hivyo ni ishara tosha kuwa amekataliwa na wanachama wa CCM, jambo zuri kwake ni kuachia hiyo nafasi ya mwenyekiti wa CCM Taifa, as I believe nothing will change AS he will remain the head of the state
hivi mfano wewe unaongoza watu elfu kumi kwenye taasisi.halafu wakatokea watu watano wakaandika vipeperushi kushawishi ukataliwe,ni sahihi ku conclude kwamba wana taasisi hawakutaki kitaalamu?je! kuna mtu anayekubalika kwa watu wote?je! unadhani kikwete angetakiwa akubalike kwa watu wote?
 
Mbona dhaifu anajijua kabisa kuwa hawezi kuongoza na ndo anazidi kuua chama sema anasema hajaona mtu ndani ya ccm anayeweza kuongaza kwa ufanisi kumzidi yeye ndo maana analazimika kugombea tena
 
Back
Top Bottom