Kikwete akiri katiba mpya haitapatikana!

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
13,234
Reaction score
20,589
Akihutubia viongozi wa mkoa wa Morogoro leo, JK amesema katiba mpya haitapatikana endapo viongozi wa kisiasa wataendelea kuvutana!

Aidha amesema yuko tayari kukutana na viongozi wote wa kisiasa ili kutafuta muafaka!

Source: Radio One Stereo.
 
Hivi Mh Rais wetu Kikwete anakua anapoteza kumbukumbu haraka au ni mimi ndio sio simuelewi vema Mh Rais??
Sí majuzi kati tu yeye mwenyewe amesema anaridhishwa na jinsi mchakato unavyoendelea na akatoa baraka kwa Bunge la katiba kuendelea na mchakato ??

Jamani labda mi nazeeka kushindwa kuelewa mambo vema, Hivi si huyu huyu alisema tujiandae kisaikolojia kuwa serikali tatu badae akaja akasema serikali tatu zitasababisha jeshi kuchukua nchi???

Mh Rais labda anazungumzia vitu tofauti tofauti ambavyo mimi navichanganya??? Jamani nisaidie ndugu yenu nimwelewe rais wangu JK (Sio JK Nyerere yeye namwelewa vema tu)
 
Bwahahahahaha.......
Bwaha-ha-ha-haha....... ooh Lord! Umeumiza mbavu zangu mkuu.
 
Hivi Mh Rais wetu Kikwete anakua anapoteza kumbukumbu haraka au ni mimi ndio sio simuelewi vema Mh Rais??
Sí majuzi kati tu yeye mwenyewe amesema anaridhishwa na jinsi mchakato unavyoendelea na akatoa baraka kwa Bunge la katiba kuendelea na mchakato ??

Jamani labda mi nazeeka kushindwa kuelewa mambo vema, Hivi si huyu huyu alisema tujiandae kisaikolojia kuwa serikali tatu badae akaja akasema serikali tatu zitasababisha jeshi kuchukua nchi???

Mh Rais labda anazungumzia vitu tofauti tofauti ambavyo mimi navichanganya??? Jamani nisaidie ndugu yenu nimwelewe rais wangu JK (Sio JK Nyerere yeye namwelewa vema tu)

Hatuna rais nchi hii bali robot! Amekutana na CC yake wiki iliyopita akajiridhisha bunge la katiba linaendelea vema!!

Sasa sijui nani mwingine kamshauri anabadilika ghafla! Kwa hiyo amewaponda wajumbe wenzake wa CC!!
 
Ina maana yeye kama yeye hana mawazo mpaka aambiwe. Duuh kazi tunayo basi.
 
Akihutubia viongozi wa mkoa wa Morogoro leo, JK amesema katiba mpya haitapatikana endapo viongozi wa kisiasa wataendelea kuvutana!

Aidha amesema yuko tayari kukutana na viongozi wote wa kisiasa ili kutafuta muafaka!

Source: Radio One Stereo.

Huyu Maradona wa Si-Hasa za Tanzania sasa anatia wasi wasi; Rais wangu JK; tafadhali sana wananchi wako tunahitaji kuwa na uhakika kuhusu misimamo yako katika mambo mbali mbali; sio asubuhi unasema hili; jioni unasema lile na mtondogoo unasema jingine kuhusu jambo lile lile!! tafadhali sana Rais wangu.

Juzi tu wewe na kamati kuu ya chama chako mmetamka kwamba mnaridhika na maendeleo ya mchakato wa katiba na kwamba mna uhakika katiba mpya itapatikana?! wiki moja baadae unatwambia nini? nini kimekusibu?!
 
Nape utakuja na wimbo gani baada ya mwenyekiti wake kuigeuka CC!
 
Sijawahi kusikia mtu kafa kwa kichefu-chefu.
Nyerere angekuwa bado yu hai, kuchefuliwa na JK kungetosha kumuua.
 
Rais wenu anaweweseka. Hakuna rangi hataiona kwa kubariki mchakato haramu na kusanyiko la maharamia linaloendelea pale Dodoma.
 
Sijawahi kusikia mtu kafa kwa kichefu-chefu.
Nyerere angekuwa bado yu hai, kuchefuliwa na JK kungetosha kumuua.

Hivi hizi jumuiya na vyuo vinavyompa tuzo kebe kebe kila kukicha vinatumia vigezo gani?!
 
Hatuna rais nchi hii bali robot! Amekutana na CC yake wiki iliyopita akajiridhisha bunge la katiba linaendelea vema!!

Sasa sijui nani mwingine kamshauri anabadilika ghafla! Kwa hiyo amewaponda wajumbe wenzake wa CC!!

Nilifikiri mm ndio sio muelewa wa mambo.
Sasa kama Mh Rais hana msimamo wa anachokiamini unategemea nini kwa raia wa kawaida?? Lbda mm ndio sijaelewa kuwa hawamaanishi wanachokisema.
Kama flip flop inaruhusiwa tena kirahisi kama hii, basi kumbe urais sio kazi ngumu hata kidogo. Kila mtu anaweza kuwa rais leo akisema hivi kesho atasema vile , hakuna haja ya kuwa na stand ya unachoamini.

Ngoja tuone hii drama yake itaishia wapi bro.
Du sijui rais ajaye ni nani na atakuaje ila huyu naomba amalize mwaka wake aondoke mimi nimeshindwa kuelwewa falsafa zake za Chalinze
 
Hivi Mh Rais wetu Kikwete anakua anapoteza kumbukumbu haraka au ni mimi ndio sio simuelewi vema Mh Rais??
Sí majuzi kati tu yeye mwenyewe amesema anaridhishwa na jinsi mchakato unavyoendelea na akatoa baraka kwa Bunge la katiba kuendelea na mchakato ??

Jamani labda mi nazeeka kushindwa kuelewa mambo vema, Hivi si huyu huyu alisema tujiandae kisaikolojia kuwa serikali tatu badae akaja akasema serikali tatu zitasababisha jeshi kuchukua nchi???

Mh Rais labda anazungumzia vitu tofauti tofauti ambavyo mimi navichanganya??? Jamani nisaidie ndugu yenu nimwelewe rais wangu JK (Sio JK Nyerere yeye namwelewa vema tu)

..kumbuka kuwa alishapata kusema UKAWA wana MAPEPO hivyo waombewe.

..sasa hao aliodai wana mapepo leo anataka kukutana nao.
 
Ina maana yeye kama yeye hana mawazo mpaka aambiwe. Duuh kazi tunayo basi.
nina mashaka anatumia thermo battery! au Operation system imekufa! sasa jamaa ndo wamaliza ku run set up! wanafanya back up ya mafaili
 
Hivi hizi jumuiya na vyuo vinavyompa tuzo kebe kebe kila kukicha vinatumia vigezo gani?!

Wanamkebehi, nae kwa uzuzu alio nao anadhani anaheshimiwa. Ndio maana kakang'ang'ana na udaktari wake kwa kichina!
 
The dude has no sense of RIGHT TIMING; kwake kila kitu ni kushtukiza tu!! It is a sign of lack of vision.

You are quite right!
1.Alianzisha mchakato wa katiba kwa kustukiza bila hata kushirikisha wenzake!

2. Alitoa ahadi nyingi zisizotekelezeka wakati wa kampeni bila kukihusisha chama chake!

3.Amekua akizusha safari za nje bila kuzingatia bajeti!

.....

Hakika huyu JK ni full matatizo na full hasara!
 
Hivi hizi jumuiya na vyuo vinavyompa tuzo kebe kebe kila kukicha vinatumia vigezo gani?!
mkuu, mtu anaweza kukusifu au kukupa kitu si kwamba anataka kukunufaisha bali anufaike yeye. nilkutana na mkongomani mmoja akaanza kunimwagia sifa kemkem hizi na zile mwisho akaniomba nimpe shs 10,000/-. Kwa hivo ni aghalabu rais kusifiwa sana na walio chini yaka au hata na watu wa nje hasa wazungu kumbe sifa hizo zina bei ndugu.
 
Back
Top Bottom