Kikwete agoma kutoa misaada ya Ambulances; Ikulu yaboronga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete agoma kutoa misaada ya Ambulances; Ikulu yaboronga!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 19, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,429
  Trophy Points: 280
  DAILY NEWS Reporter, 18th January 2010 @ 12:13,

  IN an interesting twist of events, President Jakaya Kikwete failed to hand over two ambulance vehicles today, after controversy ensued over the rightful identity of the targeted receivers.

  The confusion ensued after a representative from Ngorongoro District in Arusha Region turned up instead of an official from Longido, whom documents indicated was supposed to receive the donation.

  The twist happened at the State House grounds before officials and journalists, when the president seemed confused after he discovered it was a representative from Ngorongoro and not from the targeted Longido, who had turned up.

  A representative from Mbozi District in Mbeya Region who was meant to receive the second vehicle on behalf of his district had not yet arrived, prompting the president to hand it over to someone else who was present.

  When he approached the two cars recently donated by CMC Automobiles Limited, Chief Executive Officer, Mr Abdul Haji, President Kikwete was introduced to the receiver as the Executive Director of Ngorongoro District Council, Kayange Jacob when he suddenly stood back.

  “You are….. (as he was being introduced by the State House Comptroller), ahh, you are from Loliondo, this car is not yours, I won’t hand it over to you. It’s not yours. It’s for the people of Longido and not Loliondo.

  Turning to State House officials, he asked: What is this. This is scandalous. Apologise to those you invited to witness this”, said the president.

  “This one car is to cater for the people of Longido, not Loliondo, who sent you here?’

  The Executive Director of Ngorongoro District Council who introduced himself as Kayage, explained to the president that he had been sent by his Regional Commissioner, to come and receive the vehicle as a donation to carry sick people in Ngorongoro.

  But the president explained that records show that one of the two cars was supposed to go to Engarinaibo Village in Longido District, following his promise to them when he toured Arusha last year.

  “I personally promised the villagers I would give them an ambulance, when I receive a donation of vehicles after witnessing their difficulty in transporting their sick people to hospital. Now what is this? This is scandalous,” he repeated.

  Efforts by the State House officials to explain to the president that he hands over the car to the Ngorongoro Director, as there was no other were in vain as he (president) walked back to his office.

  After the drama that lasted for approximately 20 minutes, the Assistant Director of Communications at the State House, Premy Kibanga, told journalists that there was negligence on the part of some officials who had verified the documents, subsequently messing up issues.

  “There has been a problem of communication here at State House, as all documents including the letter to presiding secretary in Arusha, show that those entitled to the donation is Engarinaiko village in Longido and not Loliondo,”said Kibanga.

  Ms Kibanga attributed the anomaly to negligence on the part of the State House official, who was supposed to verify the documents of the director before the handing over, also blaming it on the late arrival of the two officials by ten minutes and that of Mbozi by 20 minutes.

  She said the letter from State House to the presiding secretary in Arusha, dispatched at the end of last year, was clear that that the donation was for Engarinaiko village in Longido and had asked the official to release a municipal driver, to get a short course on how to use the facility at CMC.

  However, it is not clear to this evening as to whether it was the driver of Longido or Ngorongoro who had received the short training prior to yesterday’s event.

  The director of Ngorongoro told journalists that he had been sent by the Regional Commissioner to receive the donation, after a phone call came from the State House asking them to send a representative to receive it.

  Efforts to reach the Arusha Regional Commissioner, Isidori Shirima, were futile as his phone went unanswered.

  But information sent by the Communication Directorate of State House, said the president handed over one vehicle to the Director of Mbozi District, Levison Chilewa, to cater for citizens of Kamsamba as ambulance.

  It was part of the president’s pledge to the area when he visited last year. Earlier, Mr Chilewa told journalists that it would support 26 wards in Mbozi with special target at Kamsamba, Ivuna, Chilulumo, Chitete and Msangano wards.

  The two vehicles - Land Rover Defender 110 Hard Top - worth 108,000 US dollars (about 130m/-), were donated by CMC in honour of the manager’s wife, who lived in the country for 30 years before passing away.
   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  RAIS Jakaya Kikwete jana aligoma kukabidhi gari la msaada wa kubeba wagonjwa, tukio hilo lililotokea katika viwanja vya Ikulu mbele ya maofisa wa Ikulu wakati Rais Kikwete alipoonesha kusita kulikabidhi baada ya utambulisho uliomfanya agundue kuwa aliyefika kukabidhiwa gari ni wa Ngorongoro badala ya Longido.

  Gari hilo lililotolewa msaada na Kampuni ya CMC Automobiles Limited, lilipaswa kupewa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Arusha, lakini kwa mshangao wake, jana alifika mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Kayange Jacob.

  “Wewe ni nani... ahaa, umetokea Loliondo, ahaa hii gari si ya kwako bwana, sikupi….si yako…hii ni ya watu wa Longido si Loliondo,” wewe ni nani kakutuma?” Kayange alimueleza Rais Kikwete kuwa ametumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdori Shirima. Rais Kikwete aliwageukia maofisa wa Ikulu, “Hii ni nini? Hii ni kashfa, waombeni radhi hawa mliowaalika bwana.”

  “Mimi mwenyewe nilifika katika kijiji hicho nikiwa katika ziara na moja ya ahadi zangu kwao baada ya kukuta hali walionayo katika kubeba wagonjwa kijijini hapo, niliwaahidi nikipata msaada wa gari, nitawapelekea na si hawa wa Loliondo, hii ni nini, hii ni kashfa,” alirudia kusema Rais Kikwete.

  Hata hivyo, juhudi za Maofisa wa Ikulu, kumfafanulia rais Kikwete aligoma na kuondoka kurudi ofisini (ndani) na kuendelea na kikao kingine kilichokuwa kikimsubiri. Kayange hakuamini macho yake alipoachwa peke yake baada ya rais kutokomea ofisini huku akilalamika what is this....bwana.


  WanaJF mnatoa maoni gani kuhusu hili sakata kwa rais wetu............
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,429
  Trophy Points: 280
  At last! Where have you been all these days to admit this major problem from in that office!?
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,544
  Likes Received: 18,185
  Trophy Points: 280
  BAK, miss communication is normal event, na ikulu yetu is no exception kama inatokea hata White House, itakuwa sisi?.
  Ila issue kubwa hapa kwa maoni yangu, ni deal ya RC kuipora gari ya Longido kuipeleka Loliondo!.
  Kumbe Brigedia hajatoa gari la wagonjwa!. Yeye ni ni kuvuna tuu?.
  Tatizo sio kwa watu wa Ikulu, maadam wito ulipelekwa kwa RC Shirima, Then RC anauwezo wa kumtuma yoyote kwenda kuipokea gari in good faith.

  Kama aliyetumwa haijalishi ni nani na wa wapi, kama hatimaye hilo gari lilikuwa likabidhiwe kwa wahusika Longido, then, its fine, pale ikula was juss a mess, sio scandal, ila kama ndio ilikuwa deal ya kulipora toka Longido kulipeleka loliondo, this is the real scandal!.
   
 5. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  The president is disorganized so is his office
   
 6. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Yah niliona kwenye habari ya jana mkuu,muungwana alionekana kuchukia,lakini mpaka sasa sielewi kuwa mpaka rais anatoka ofisini hakujua anaenda kumpa nani gari?,je huyo mkurugenzi aliyenyimwa hilo gari halihitaji(na maana kwake hakuna uhaba wa magari ya kubeba wagonjwa?).Anyway tuwaachie wenyewe bwana na protocal zao
   
 7. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,891
  Likes Received: 1,644
  Trophy Points: 280
  AYA MAJAMAA YANAYO FANYA KAZ NA RAIS KILA SIKU TUNASEMA YANA AKILI FUPI, MAZOEA NA UVIVU WAKUSOMA ALAFU MNATEGEMEA TAIFA LIENDELEE? FACK OFF PUMBAVU TAIFA LINATEKETEA KWA MAJINGA KAMA HAYA FUKUZA TUPA MGAMBO WAKAPIGE KWATA, WHERE I WE GOING? NALAANI UJINGA HUU. MUNGU LIBARIKI HL TAIFA NA WATU WAKE. Amen
   
 8. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Tatizo la JK anaaibisha Ikulu yetu. Kutaka publicity sana kuna mgharimu. Tumechoshwa kusikia failures zinazoihusu ikulu hata kwa masuala madodo madogo kama haya.

  vitu vingine vidogo vidogo kama hivi angelikuwa anawaachia wasaidizi wake wahusike navyo. Anajaribu kujiaibisha na intelligence yake/yetu bureeee!!. Wakati fulani, hata kama kuna udhaifu kwenye nyumba, mama au baba hujaribu kujistiri kidogo!

  JK hajifunzi tu? Juzi juzi tu hapa katuacha hoi na ile hotel ya Arusha, hatujakaa sawa mkenge na CMC.

  Uozo wa CMC tunaufahamu. Wahindi hawa, wanadhurumu mali ya wa TZ kwa kukwepa kodi, halafu wanatumia pesa walizokwepa kodi nk, kujifanya wanatoa misaada. Huu ni uhuni!

  Kwa JK
  Mh Rais unatuaibisha. Kwa nini kujihusisha husisha na uzinduzi wa vitu vidogo vidogo ambavyo hata havijawekwa sawa??. Kama, ndiyo njia ya kutaka mass support, poa! Ngoja nimalizie kajumba kangu, nami nianze kuwasiliana na wakuu wa itofaki; wakulete uje ukazindue. Huku utashangiliwa sana!

  Ila ujapo uje na majibu ya swali hili: Wewe hauoni unatuaibisha kwa kujihusisha husisha na uzinduzi wa shughuli ndogo ndogo ambazo zingefanywa na wasaidizi wako wakiwemo wakuu wa wilaya?????
   
 9. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Aisee jana ilikuwa aibu sana,yaani rais ametoka mpaka anakaribia kugawa gari kumbe ameletwa mtu mwingine? Kwanini watu wa Longido hawakuja?
   
 10. T

  TANURU Senior Member

  #10
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni aibu kwa kweli yaliyotokea ikulu hiyo jana. Swali la Hassani ni la msingi sana.
   
 11. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lakini angalau JK ameamka. Sio alivyofanywa vibaya Arusha. Hata kajumba ka Sisimizi ataenda tu maadam kamera za ITV na TBC1 zitaalikwa pia. Mmmmm! JK, kikulacho ki nguoni mwako baba. Unasafisha miguu kabla ya kunawa uso? Usikaushe maji ya singo kwa taulo wakati bado hujaosha kichwa.

  Leka
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,644
  Likes Received: 21,855
  Trophy Points: 280
  Hizi ni dalili tosha kuwa kuna uoza wa kiutendaji na mambo ya hovyo hovyo yanayofanyika katika ofisi ile ni bahati mbaya tuu kuwa hatuyafahamu.
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hata pale Uwanja wa Taifa na kombe la dunia aibu nyingine iljitokeza pale alipotaka kumkabidhi mkewe kombe lile aliguse. Lipo tatizo kwa wasaidizi wake hasa mtu anayeitwa Fyataga.
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu ameanza kupraktisi maamuzi magumu!!!!!!!!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  kwani kulikuwa na ulazima gani wa yeye kwenda kutoa hiyo misaada ya magari mawili? Inakuwaje Rais anatoka Ofisini kwake kwenye kwenye hafla ambapo wanaotakiwa kuwepo walikuwa hawapo!? something is wrong..

  Yaani, hadi Rais anatoka ofisini na kwenda pale yuko tayari kutoa misaada hakuna aliyegundua tatizo. Ndiyo maana tukasema mambo ya mpira awaachie kina Bendera, ya kutoa misaada awaachie kina Mnakulu Mkuu ?? au Katibu Mkuu.. afanye mambo ya msingi.. siku nyingine atatembea nje usiku wa manane huku walinzi wakimsindikiza tu kumbe mwenzao anaota!
   
 16. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #16
  Jan 19, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  naamini JK SASA analielewa somo kuwa wasaidizi aliowateua ni vimeo, uteuzi wake unamgharimu, wanashidwa kumsaidia na kumuokoa kutoka kwenye aibu kama hizo, walitakiwa wao kugundua makosa kabla ya JK.

  kUMBUKENI MKASA WA JK kwenda kuzzindua kivuko daraja hewa kule mto Ruvuma miaka miwili nyuma, kumbuka mkasa wa JK kuzindua Hotel yenye matatizo ya kujengwa kwenye hifadhi ya barabara kule Arusha, ni milolongo hadi kufikia JK kupigwa mawe MBEYA, hana wasaidizi makini kwa sababu hakuwa na uteuzi makini.
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mnajidai mnashtuka sasa hivi madudu mangapi yanafumbiwa macho zaidi ya hilo la kukabidhi gari? Kwani Longido ipo mkoa gani na hii Loliondo ipo mkoa gani naomba ufafanuzi na huyo Mtendaji kasema ametumwa na mkuu wa Mkoa Arusha.
   
 18. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kwa kweli tukio la mkulu kung'aka ni kusikitisha na hii inaonyesha ni jinsi gani asivyopenda kudelegate minor issues kama hii. Aidha ilipaswa awe well informed na wasaiduzi wake kabla ya kwenye hiyo hafla. It is ridiculous..!
   
 19. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Walitaka kumuuzia mbuzi kwenye gunia. Alishtukia ishu, yeye kataka longido nyie Loliondo wakati kule kuna maharamia wanaendelea kujivunia mali ya wadanganyka! Akasema "Sidanganyiki!"
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  halafu kwanini anafikiri hii ni 'kashfa' sidhani kama ni kashfa tu the extent ya majumba ya Benki Kuu, Meremeta, n.k hayo yote hajawahi kuita ni kashfa! mweh.. Inawezekana kweli kuwa kulitokea mchanganyo kidogo lakini siyo kashfa kubwa hivyo kiasi cha kufukuzisha watu kazi..

  Katika orodha ya kashfa zinazokabili taifa letu hii wala siyo kashfa! Tukikubali tutashangilia akiwafukuza watu au kuwawajibisha hawa watu huku zile kashfa zenyewe watu wake wakiendelea kupeta
   
Loading...