Kikwete agoma kutoa misaada ya Ambulances; Ikulu yaboronga!

Wadanganyika tunauwezo mkubwa sana wa kusahau haraka.... Tumeshasahau kwamba muungwana alishawahi kupewa cheque ambayo tarakimu zake zinatofautiana sana na fedha halisi zilizotakiwa kuandikwa kwenye cheque!!

ongezea kwenye orodha ya fedheha za rais na siyo kusema watu wanasahau.
 
kwani kulikuwa na ulazima gani wa yeye kwenda kutoa hiyo misaada ya magari mawili? Inakuwaje Rais anatoka Ofisini kwake kwenye kwenye hafla ambapo wanaotakiwa kuwepo walikuwa hawapo!? something is wrong..

Yaani, hadi Rais anatoka ofisini na kwenda pale yuko tayari kutoa misaada hakuna aliyegundua tatizo. Ndiyo maana tukasema mambo ya mpira awaachie kina Bendera, ya kutoa misaada awaachie kina Mnakulu Mkuu ?? au Katibu Mkuu.. afanye mambo ya msingi.. siku nyingine atatembea nje usiku wa manane huku walinzi wakimsindikiza tu kumbe mwenzao anaota!

tatizo hapa ni je hawa watakaoachiwa haya majukumu watayafanya kama Mh. Rais anavyotaka? maana kama hapa wanachanganyana mbele ya Rais itakuwaje kwa hawa wadogo?

sisi wabongo wengi huwa hatuwi serious ndiyo maana kuna matatizo katika nyanja nyingi hebu angalia kwenye
1. mpira hususani wa miguu (TFF) virabu na timu ya taifa
2. mamiss kwa lundenga
3. riadha (ikangaa)
4. ngumi (kuna watu walikamatwa na madawa ya kulevya)
5. filamu (akina Ray na Kanumba)
6. nk nk nk
7. EWURA?????????
8. SUMMATRA
9. NK, NK, nk, nk

kama tungekuwa serious hata kidogo basi lazima tungefanikiwa katika maeneo fulani fulani ambayo hayahitaji government interventions.
 
jk na wasaidizi wake walikuwa wanafanya ZE COMEDY SHOW ili kupata headlines kwenye vyombo vya habari kuwa naye anaweza kuwa mkali...anashindwa kuwa mkali kwenye mambo ya msingi...

ni ze comedi kwa kuwa rais kabla hajanyanyuka kwenye kiti kwenda mahali anapewa briefing ya tukio analoenda kufanya ..kwa mapanda ....na afisa anayempa briefing anafanya uhakiki wa maandishi na physical .......na kama ni kukosea angejuwa akiwa ofisini kuwa wamekosea.....na waala hapakuwa na haja ya kufanya ze comedy...

afteral ni kupoteza muda wa rais ...kwani ingetosha siku alipopokea haya magari toka kwa Haji yule wakala wa cmc[wanaoiuzia serikali magari] ....angeweza kuagiza pale pale kuwa wapewe nani ............sasa kulikuwa na haja gani ya kuwasafirisha wakurugenzi waje kupokea vigari viwili.....hatuoni tunapoteza muda wa kufanya kazi?? maafisa ugavi wanafanya nini..kama rais anafanya kazi yao.....mbona wizara ya afya inapokea magari kila siku na anayepokea mara nyingi ni mkurugenzi wa tiba au kinga.....na anayatuma kwa maafisa ugavi wanayapeleka wilaya kusudiwa ....

rais ana muda wa mchezo huyu...si bora cheo cha state house comproller kiondolewe.....au comproller kazi yake ni kugawa mbuzi na maharage wakati wa sherehe ...lakini kupokea misaada ya wafanyabiashara ni lazima awe rais.......unamruka comproller,msaidizi maalum wa rais ,katibu mkuu,katibu mkuu kiongozi ,mawaziri wa nchi ofisi ya rais.....hadi kumlazimu rais mwenyewe ainuke?
 
Wadau

Nimeona wengi mmetoa michango mizuri sana juu ya umuhimu wa rais kutojiingiza kufanya kila jambo na kumsababishia fedheha. Nakubaliana nanyi kwa asilimia 100%.

Lakini, katika tukio hili tunatakiwa kuwa na mtazamo wa upande wa pili. Wachache sana wamejaribu kuhoji nia halisi ya uongozi wa mkoa wa Arusha. pamoja na 'makosa ya kiutendaji' pale ikulu kushindwa kutofautisha Longido na Loliondo, ni vizuri tukapata ufafanizi wa lengo la RC/RAS kuamua kuhamisha ahadi ya rais kwa watu wa Longidi.

Kisiasi, rais alikuwa na sababu ya kusita kuendelea na zoezi lile, kwani anazo kumbukumbu za ahadi aliyotoa kwa watu wa Longido. Lakini, jambo jingine ni kwamba hata angeamua kufumba macho na kuendelea na mgao, bado hiyo ingeendelea kuwa habari. Kama gari lingekwenda Loliondo badala ya Longido, ni dhahiri habari zingevuja. Na kama wangefanya utaratibu wa siri baada ya hapo na kulipeleka Longido, nayo ingekuwa habari.

Hii inaweza kuwa kiashiria cha jinsi mambo mengi yanavyoweza kubadilishwa na watendaji na mwisho wa siku yasiwafikie wahusika.
 
RAIS Jakaya Kikwete jana aligoma kukabidhi gari la msaada wa kubeba wagonjwa, tukio hilo lililotokea katika viwanja vya Ikulu mbele ya maofisa wa Ikulu wakati Rais Kikwete alipoonesha kusita kulikabidhi baada ya utambulisho uliomfanya agundue kuwa aliyefika kukabidhiwa gari ni wa Ngorongoro badala ya Longido.

Gari hilo lililotolewa msaada na Kampuni ya CMC Automobiles Limited, lilipaswa kupewa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Arusha, lakini kwa mshangao wake, jana alifika mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Kayange Jacob.

"Wewe ni nani... ahaa, umetokea Loliondo, ahaa hii gari si ya kwako bwana, sikupi….si yako…hii ni ya watu wa Longido si Loliondo," wewe ni nani kakutuma?" Kayange alimueleza Rais Kikwete kuwa ametumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdori Shirima. Rais Kikwete aliwageukia maofisa wa Ikulu, "Hii ni nini? Hii ni kashfa, waombeni radhi hawa mliowaalika bwana."

"Mimi mwenyewe nilifika katika kijiji hicho nikiwa katika ziara na moja ya ahadi zangu kwao baada ya kukuta hali walionayo katika kubeba wagonjwa kijijini hapo, niliwaahidi nikipata msaada wa gari, nitawapelekea na si hawa wa Loliondo, hii ni nini, hii ni kashfa," alirudia kusema Rais Kikwete.

Hata hivyo, juhudi za Maofisa wa Ikulu, kumfafanulia rais Kikwete aligoma na kuondoka kurudi ofisini (ndani) na kuendelea na kikao kingine kilichokuwa kikimsubiri. Kayange hakuamini macho yake alipoachwa peke yake baada ya rais kutokomea ofisini huku akilalamika what is this....bwana.

WanaJF mnatoa maoni gani kuhusu hili sakata kwa rais wetu............

Kinachoonekana hapa ni drama isiyo na sababu. Ambacho angeliweza kufanya Rais ni kukabidhi gari na kutoa angalizo kwa wasaidizi wake kwamba gari lile si la Loliondo bali ni la Longido. Wakati huo huo angemuagiza huyo Kayange afikishe ujumbe kwa Mkuu wa Mkoa kwamba anataka gari hilo liende Longido ambako ndiko lilikodhamiriwa na aletewe taarifa kwamba gari lile limefika Longido. Rais kulalamika na kususa hadharani kwa jambo dogo kama hilo haileti picha nzuri. Hii inaitwa creating a mountain out of a mole hill!
 
jk na wasaidizi wake walikuwa wanafanya ZE COMEDY SHOW ili kupata headlines kwenye vyombo vya habari kuwa naye anaweza kuwa mkali...anashindwa kuwa mkali kwenye mambo ya msingi...

ni ze comedi kwa kuwa rais kabla hajanyanyuka kwenye kiti kwenda mahali anapewa briefing ya tukio analoenda kufanya ..kwa mapanda ....na afisa anayempa briefing anafanya uhakiki wa maandishi na physical .......na kama ni kukosea angejuwa akiwa ofisini kuwa wamekosea.....na waala hapakuwa na haja ya kufanya ze comedy...

afteral ni kupoteza muda wa rais ...kwani ingetosha siku alipopokea haya magari toka kwa Haji yule wakala wa cmc[wanaoiuzia serikali magari] ....angeweza kuagiza pale pale kuwa wapewe nani ............sasa kulikuwa na haja gani ya kuwasafirisha wakurugenzi waje kupokea vigari viwili.....hatuoni tunapoteza muda wa kufanya kazi?? maafisa ugavi wanafanya nini..kama rais anafanya kazi yao.....mbona wizara ya afya inapokea magari kila siku na anayepokea mara nyingi ni mkurugenzi wa tiba au kinga.....na anayatuma kwa maafisa ugavi wanayapeleka wilaya kusudiwa ....

rais ana muda wa mchezo huyu...si bora cheo cha state house comproller kiondolewe.....au comproller kazi yake ni kugawa mbuzi na maharage wakati wa sherehe ...lakini kupokea misaada ya wafanyabiashara ni lazima awe rais.......unamruka comproller,msaidizi maalum wa rais ,katibu mkuu,katibu mkuu kiongozi ,mawaziri wa nchi ofisi ya rais.....hadi kumlazimu rais mwenyewe ainuke?

Hapo kwenye RED ndipo panapoweza kueleweka kichwani mwangu. Vinginevyo napata kizungu zungu.:confused:

Hata hivyo tukumbuke kuwa kwenye kila kazi kuna specialization. Former Kenyan Presida, D A Moi alijiita profesa wa siasa. Nadhani hapa tumetegeneza profesa wa kucheza na media! Vinginevyo sina maelezo mengine ninayoweza kuyaelewa; ukizingatia akili yangu tayari ime-jam linapokuja suala la JK na mstakabali wa TZ/Bongo!!
 
Aliyakataa mapanki ya Mwanza, akaambiwa pia kuwa ile kampuni, BAE, iliyotuuzia rada ni mali ya serikali ya Uingereza, Rais wetu wasaidizi anao!

Hivi huyu rais wetu alipewa orientation ya kutosha? Ipo haja ya kumkumbusha kwamba yy ni rais wa Tanzania huenda itamfanya aache kutudhalilisha kiasi hiki. Nakumbuka kuna siku alikuwa anajibiza na watunza magari wa bandarini nikajiuliza tofauti ya levels toka kwa rais mpaka wao nikakosa jibu. Rais gani huyu kila siku yuko busy na micro issues na kuacha issues za msingi hazifanyiwi kazi? Mr. President tumechoka hiyo taasisi ya urais ni ya watanzania tafadhali usiendelee kutudhalilisha kiasi hicho.
 
Hizi ni dalili tosha kuwa kuna uoza wa kiutendaji na mambo ya hovyo hovyo yanayofanyika katika ofisi ile ni bahati mbaya tuu kuwa hatuyafahamu.

Hao ndio wanaMtandao at their best!! Hawa jamaa sio serious na mambo yao wamejaa usanii tu!
 
Viongozi wa Arusha wana Matatizo na Uongozi/ Maamuzi ya JK...!!

Kuna dharau iliyopitiliza kutoka Arusha.
 
Ubabaishaji kila mahali serikalini.

Hili tumelijua, je mangapi yamefanyika hatujui?????

Sasa kama Kikwete kweli uko serious, basi fukuza kazi mara moja wale wote waliokuwa wanataka kukuingiza kwenye kashfa hiyo.
 
Ubabaishaji kila mahali serikalini.

Hili tumilijua, je mangapi yamefanyika hatujui?????

Kila siku scholaship za wakulima wanapewa watoto wa vigogo...promotion za wengine makazini wanapewa wengine wasiostahili, safari za nje kwenye mafunzo badala ya kwenda watendaji wanakwenda mabosi.... the list goes on and on...sasa mchezo umezoeleka hadi wamemfikishia rais ikulu.

Iko siku atagombea na kushinda uraisi Juma, mtakuja kushuhudia anaapishwa Shomari...nyie subirini. hawana sura ya aibu hata kidogo hao watu...!!
 
RAIS Jakaya Kikwete jana aligoma kukabidhi gari la msaada wa kubeba wagonjwa, tukio hilo lililotokea katika viwanja vya Ikulu mbele ya maofisa wa Ikulu wakati Rais Kikwete alipoonesha kusita kulikabidhi baada ya utambulisho uliomfanya agundue kuwa aliyefika kukabidhiwa gari ni wa Ngorongoro badala ya Longido.

Gari hilo lililotolewa msaada na Kampuni ya CMC Automobiles Limited, lilipaswa kupewa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Arusha, lakini kwa mshangao wake, jana alifika mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Kayange Jacob.

“Wewe ni nani... ahaa, umetokea Loliondo, ahaa hii gari si ya kwako bwana, sikupi….si yako…hii ni ya watu wa Longido si Loliondo,” wewe ni nani kakutuma?” Kayange alimueleza Rais Kikwete kuwa ametumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdori Shirima. Rais Kikwete aliwageukia maofisa wa Ikulu, “Hii ni nini? Hii ni kashfa, waombeni radhi hawa mliowaalika bwana.”

“Mimi mwenyewe nilifika katika kijiji hicho nikiwa katika ziara na moja ya ahadi zangu kwao baada ya kukuta hali walionayo katika kubeba wagonjwa kijijini hapo, niliwaahidi nikipata msaada wa gari, nitawapelekea na si hawa wa Loliondo, hii ni nini, hii ni kashfa,” alirudia kusema Rais Kikwete.

Hata hivyo, juhudi za Maofisa wa Ikulu, kumfafanulia rais Kikwete aligoma na kuondoka kurudi ofisini (ndani) na kuendelea na kikao kingine kilichokuwa kikimsubiri. Kayange hakuamini macho yake alipoachwa peke yake baada ya rais kutokomea ofisini huku akilalamika what is this....bwana.

WanaJF mnatoa maoni gani kuhusu hili sakata kwa rais wetu............

Hivi kumbe bado anakumbuka ahadi zake?? Si kuna siku alizikana akidai hiyo ilani ya CCM hakuiandika yeye??

Anayway, kwa maoni yangu JK naye kachemsha kuna haja gani ya kuonyesha ubabe mbele ya wageni na hao journalist??? Kwa mtaji huu sijui tutegemee nini akipata awamu ya pili?? Nafikiri ubabe utazidi kipimo. Au ndiyo hayo maamuzi magumu???!!!
 
Hii ndiyo faida ya kuajiri watoto wa mjomba kwenye issue sensitive. Watakuja kukubadilishia mpaka mke shauri yako.....

Hivi wewe hujui wanaofaa secret service ni watu wa namna gani? Jk..jk..jk..jk.. Utakuja pigwa kokoto la macho wewe!!!!!!!!
 
mi nazani kuna tatizo kubwa katika haya yote....huenda raisi n mbishi na anataka kufanya anavyotaka yeye au wasaidizi wke wanamfanyia kitu kibaya au ni uozo uliopo kwa hiyo kila mtu anaona bora liende, hakuna wakumshika mwingine,hivi mbona ile aibu ya hotel ya arusha ilikuwa mbaya sana,ni wakati raisi afanye ya muhimu...naaza kuhisi hawa wasaidizi wakati mwininge wana ajenda ya siri,kumharibia JK

Wengi walioingia kufanyakazi Ikulu na Jakaya ni wale walioteuliwa kwa mapendekezo ya Rostam[ Salva Rweyemamu et al]' kwahiyo royalty yao haiko kwa Jakaya bali kwa Rostam/Lowassa kwahiyo kazi wanayoifanya pale ni kuhakikisha kuwa Jakaya anaonekana anapwaya!! I hope by now amekwisha gundua hilo na kama bado soon he will be in serious trouble!! Wakina Salva wapo hapo kukusanya materials za kuja kumuandika Jakaya na urais wake vibaya baadae!!
 
Yeah. Lakini sio wote. Baada ya ile barua ya Salva kwa Rostam kuanikwa jamvini, imemshushia hadhi mno! Ambitions za kutaka kufika juu sio mbaya lakini utekelezaji wa hizo ambitions zako to the expense of your integrity ndio dhambi isiyokosheka.
 
JK ameonyesha kuwa ahadi zake anazozitoa anazikumbuka kuliko hata hao wasaidizi wake na hao anaoambatana nao kwenye misafara mirefu ya gharama kubwa kumbe hata hawatilii maanani anachokiongea huko. Hongera JK, la MAISHA BORA kwa kila MTZ limekaaje? 2010 hii!

Inawezekana kweli hili ni dili kuonyesha kuwa mbali ya shughuli nyingi alizonazo rais si msahaulifu akisema kitu lazima akifuatilie, lakini je vipi lile la Maisha bora kwa kila mtanzania bado analikumbuka?
 
Hivi kuna taarifa kwamba kuna watu wamefukuzwa kazi? Mwenye taarifa atueleze. Au ni yale yale tu kama ya EPA, Richmonduli, Dowans et al?
 
Back
Top Bottom