Kikwete abatilisha adhabu za vifo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
RAIS Jakaya Kikwete amesema, hivi karibuni alibatilisha hukumu 75 za vifo kuwa vifungo vya maisha.

Mbali na kubatilisha huko amesema licha ya Tanzania kuwa na sheria ya Kunyonga katika vitabu vya nchini, kwa muda mrefu haijanyonga mtu.

Rais Kikwete alisema hayo juzi wakati wa chakula cha usiku katika makao makuu ya Jumuiya ya Kilei ya Kanisa Katoliki Duniani la Mtakatifu Eggidio, mjini Rome, Italia.

Ujumbe huo wa Mtakatifu Eggidio uliongozwa na mwanzilishi wa Jumuia hiyo, profesa wa historia katika chuo kikuu cha Rome, Profesa Andrea Riccardi na msaidizi wake wa kiroho, Padre Matteo Zuppi.

“Hili ni jambo lililoulizwa na Kamati ya Jaji Nyalali. Watu walikataa kufutwa kwa adhabu ya kifo. Majuzi nilibatilisha kiasi cha hukumu 75 za vifo kuwa vifungo vya maisha. Lakini bado waliohukumiwa kifo kwenye magereza yetu ni wengi, pengine kufikia watu 200, hata kama sijahesabu.”

Rais Kikwete alisema hapa nchini bado idadi kubwa ya watu wanapinga kufutwa kwa adhabu ya kifo na wanataka adhabu hiyo iendelea kuwapo katika vitabu vya sheria.

Akizungumzia mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino, alisema mbali na kuonekana mauaji ya kusikitisha lakini ni mauaji ya kijinga kutokea katika dunia ya leo ya sayansi na teknolojia ambayo yameliaibisha taifa la Tanzania.

“Kwamba watu wanaweza kuwa wajinga kuamini kuwa ukipata kidole cha albino utatajirika ni jambo gumu sana kuamini katika dunia ya leo ya sayansi na teknolojia. Lakini napenda kuwahakikisheni kuwa sasa Serikali imeyathibiti mauaji haya,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Tuliendesha kura ya maoni. Watu wengi wametiwa mbaroni na wengine wako mahakamani. Kati yao wengine wamehukumiwa kunyongwa,”
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=4448
 
JK kaanza kampeni mapema sana,tume ya uchaguzi tafadhali toeni kauli walau ya kumkaripia asubiri wakati ukifakia atueleze blah blah kama kawaida yake safari hata akishinda hawezi kupata zile asilimia 80 za mwaka 2005.
 
Mbali na kubatilisha huko amesema licha ya Tanzania kuwa na sheria ya Kunyonga katika vitabu vya nchini, kwa muda mrefu haijanyonga mtu.

Ni mtu asiyeelewa concept ya "rule of law" tu, au yule ambaye anaielewa lakini hawezi ku resists self congratulation hata pale ambapo haiwezekani, anayeweza kusema hayo.

Tatizo la wanaopinga adhabu ya kifo si tu idadi ya watu wangapi wananyongwa, bali pia kwamba sheria inaruhusu kunyonga.

Katika nchi inayofuata utawala wa sheria, huwezi kujitapa kwamba "ingawa hatuna sheria za kuzuia ubadhirifu, hatuna tatizo la ubadhirifu" kwani sheria zitakuwa zinaruhusu ubadhirifu.

Yaani wanaomuandalia cha kusema bure, yeye mwenyewe bure.

Sasa kama una sheria ya kunyonga watu halafu huitumii hiyo sheria ya kazi gani? Si uifute tu?

Amua moja, sisi tuna sheria ya kunyonga na tunanyonga watu, au hatuamini katika kunyonga watu hivyo tunaifutilia mbali hii sheria.Huu uvuguvugu hata kwenye vitabu ulikatazwa.
 
Haelewi anatoka wapi wala anaelekea wapi Rais wetu..! Hata swali hilo linakuwa gumu kujibu ?

Namfananisha na jamaa yangu mmoja katoka Bongo kaenda nje kutafuta kazi..Alipo ulizwa kazi gani anaweza kufanya ? aka jibu kazi yoyote ili mradi apate mshahara.

Sasa unategemea mtu huyo kweli atapata kazi kwa maisha ya sasa.
 
Inasikitisha kuona jinsi tunavyofikiri na kuamua mambo ya nchi. Utani utani tuu nothing is done seriously! Unadhubutu kusema kama unajikomba kwa watu wakati unawakilisha nchi. Inaonyesha wazi jinsi ambavyo hawataki kubadilisha mambo mengi yaliyopitwa na wakati. Wanavyoogopa kuyafanyia kazi, maana akiulizwa ni wakina nani hao waliokataa atakutajia watu anaowafahamu yeye tu, waliokaribu naye, wana ccm. Wangeangalia jinsi wenzetu wanavyojadili kwa nguvu za hoja nzito kuhusu "health care" huko Marekani. Haieleweki ni majukwaa yepi yanayotumika kujadili haya mambo muhimu ya kitaifa hapa kwetu. Hivi ndivyo ufisadi ulivyozaliwa maana wapo watu wachache sana huenda hawazidi hata mia moja wanaoliamulia mwelekeo taifa la watu milioni 40. Inawezekana nilipitwa na hili lakini sijawahi kusikia swala la kufuta adhabu ya kifo limejadiliwa bungeni. Niombe msaada wenu wana-JF
 
Back
Top Bottom