Kikwete Aahidi Bajaj 400 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Aahidi Bajaj 400

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sn2139, Aug 31, 2010.

 1. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mgombea wa CCM JM Kikwete jana alitoa ahadi ya kutoa bajaj 400 kwa wajawazito huko Chunya ili ziwasaidie kuwawahisha hospitalini mara tu atakapoingia madarakani. Source: Radio Maria
  Sungura
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,330
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Aagize na bajaj nyingine kwa ajuili ya kutembelea mawaziri wake kwenye mizunguko yao ya hapa mjini.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nijuavyo Bajaji rough road hazifui dafu,amalize kwanza rami ambayo kwa sasa imesimama kisa mkandarasi hajapewa mkwanja,labda kwa kuwa yuko mbeya mkwanja unaweza ukawekwa sawa
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Jakaya Kikwete ameahidi kutoa pikipiki za miguu mitatu(Bajaj) 400 za wagonjwa(ambulance) kwa nchi nzima na gari moja la Wagonjwa kwaajili ya kituo cha afya cha Mkwajuni ili kuwasafirisha wajawazito katika Wilaya ya Chunya.

  Akizungumza na Wakazi wa Mkwajuni Wilayani hapa wakati wa mkutano wake wa kampeni,Kikwete alisema ahadi hiyo ataitekeleza pindi atakapochaguliwa kurejea kwenye kiti alichonacho hivi sasa.


  Chanzo:Tanzania Daima.

  Mwandishi: Irene Mark.Mbeya.

  My take.

  Bajaj na wajawazito hii kali hata kipindi cha zama za mawe hii isingekubalika.Bado sijamuelewa ana maanisha nini!!1 kazi ipo.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,330
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Kazidisha sana ahadi, mwisho tutamsikia akiwaahidi wananchi wa dodoma usafiri wa meli
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  bajaj kwa ajili ya wajawazito? hiko kioja cha mwaka
   
 7. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #7
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM, amesema kuwa chama chake kimebuni mkakati mzito wa kuwasaidia kina mama wajawazito wanapoenda clinic au kwenda kujifungua. Akihutubia mamia ya wananchi mkoani Mbeya, JK alijitapa kuwa tatizo la usafiri kwa akina mama limefika mwisho kwani atahakikisha kama atachaguliwa tena serikali yake itaagiza pikipiki za miguu mitatu maarufu kama bajaji, 300 (mia tatu) ambazo atazisambaza nchi nzima kwa ajili ya kuhakikisha hakuna mama mjamzito atakayepata shida ya usafiri. JK pia aliahidi kununua gari moja la wagonjwa (ambulance) ambayo ataizawadia hospitali moja huko mbeya ili kusaidia bajaji zitakazokuwa huko.

  Source; Tanzania Daima ya leo...
   
 8. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani wewe ni leo tu ndo hujamwelewa ? Mbona mwenzio sijawahi kumwelewa na siku hizi nemeamua kunyamaza tu.
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  nGoja nikatafute mtu anipige mimba nifaidi
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu Mkulu mwaka 2005 alifanyaga kampeini? Alizungumziaga nini tena? Sijui nilikuwa wapi kuzingatia aliyokuwa akiyasema kwenye kampeni zile za mwaka ule maana..... naanza kupatwa na mashaka!!
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Angewapa Mawaziri,MaRC,nk hizo Bajaj...:becky:
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mie najiuliza hivi mwaka 2005 alifanyaga kampaini? alikuwa anaongea nini na imekuwaje sasa hivi naona kama anachemka tu? Bajaj kwa wanawake wajawazito?? Mkuu... (Sijui mwaka ule nilikuwa nashangaa sura na tabasamu) ah.
   
 13. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamani hivi ni kweli au? mimi naona anaona makazi ya wananchi wengi yapo mbali na hospitali, for that case anataka kurahisisha procees ya kujifungua, mama mjamzito akirushwa na bajaji dk.2 tu kajifungua, manake he cnt be seriouz inakuwaje umpandishe mama mjamzito bajaji.
   
 14. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #14
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Yani wajawazito wanunuliwe bajaji mia tatu, wakati mashangingi ya viongozi yanaagizwa zaidi ya 300 kila mwaka!
   
 15. R

  RACKY Member

  #15
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Sio vibaya kwa yeye kutoa ahadi hiyo ila tatizo ni kwamba ikiwa yeye ni kiongozi ambaye yuko madarakani anaomba aongezewe muda wa kuwa madarakani. kama alisha ona kuwa kuna tatizo hilo la upungufu wa viombo vya usafiri kwa wagonjwa hasa mama wajawazito, na akaliwekea ukimia ili kana kwamba atumie tatizo hilo kwa masilahi binafsi, si sahii.
  Mh uwezo unao nguvu unayo tuna omba wezesha sasa ili WATANZANIA wazida kuwa na imani na ahadi
   
 16. b

  bobishimkali Member

  #16
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unashangaa nini? hujui kwamba yapo maeneo ya vijijini wajawazito wanasafirishwa kwa baiskeli.Huoni kwamba bajaji zinaweza zikawasaidia zaidi wajawazito hao kushinda baiskeli wanazotumia? bajaji ni usafiri mzuri na unakubalika kulingana na maeneo husika .
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  "Aisee"
   
 18. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hilo nalo ni la kushangaa!!
  kawaida ya mkuu anapokuwa jukwaani macho yake yanakuwa mbelee.
  sasa wakati alipokuwa jukwaani chunya, ghafla bajaji kwa mbaali ikapita ndipo hiyo ahadi ikaja ghafla nayo.
  Hata ingepita treni kwa muda ule angeahidi treni.
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tokea ameanza kampeni kuna idadi ya ahadi kama 25 hivi kama sio 30 kujenga viwanja vya ndege, kununua meli, umeme na nyingine nyingi ataweza kweli huyu mkulu
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  :becky::becky::becky::becky: hiyo kali kweli
   
Loading...