Kikundi cha 'Mungu ndie msaada wetu' kipigwe marufuku haraka

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
298,978
751,639
Kikundi kimoja cha kidini mkoani Rukwa kimepiga marufuku waumini wake wa kike wajawazito kuhudhuria kliniki huku watoto wakikatazwa kupokea chanjo yoyote kwa maelezo kuwa ni kinyume na mafundisho ya Mungu
Na waunini wengine wote wamekuwa wakizuiliwa kutumia tiba yoyote ya hospital
Baada ya habari hii kujulikana kiongozi wao alikimbilia kusikojulikana na kuzima simu zake zote
 
Wanapataje usajili hawa watu? Na kama hawakuwa wamesajiliwa, inakuwaje wafanye kazi zao bila kuwa na kibali?

Ahsante kwa taarifa mshana jr naamini wahusika watachukua hatua stahiki
 
Umenikumbusha Mashaidi wa Yehova Masalia, watu sijui wanakuwaga wamelishwa dawa hawaambiliki wala hawaelewi kitu.
Page+3.JPG

Polisi yatoa onyo la mwisho kwa Wasabato Masalia

KUNDI la waumini wa Dhehebu la Waadventista Wasabato Masalia, kwa mara ya tatu limesambaratishwa na askari wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kurudi tena uwanjani hapo huku wakiwa wameongezeka idadi yao kutoka 17 hadi kufikia 51.

Wasabato hao masalia, walifika katika uwanja huo mnamo saa 2:00 asubuhi huku wakiwa na mabegi yao tayari kwa safari wakisema: "Bwana alikuwa amewaambia tena kuwa jana ilikuwa ndio siku ya kuondoka na kuelekea nchi za Ulaya kuhubiri injili."
Na Furaha Kijingo
 
Mkuu mshana jr umenikumbusha Wasabato Masalia. Religion is an opium. Kwanini watu hutapeliwa kirahisi kupitia dini? Huwa nashindwa kupata jibu.
Yaani wakili wangu msomi, hata mie huwa najiuliza sipati jibu. Kwa mfano miaka ya nyuma huko wilayani Ukerewe - kata ya Namagondo iliibuka dini ambayo ilikuwa haieleweki. katika mtiririko wake wa ibada kulikuwa na kipindi kinaitwa "KIPINDI CHA UUMBAJI" yaani ikifika muda huo taa zina zimwa halafu waumini kila mmoja ana mdaka mwanamke/mwanamme anayempenda "kuumba" naye, hivyo wanafanya sex. eti kipindi cha uumbaji!!!. Nashukuru baadae DC aliipiga marufuku.
 
dini ni ulevi wa hovyo sana, washirika mnazidi kuwa maskini huku viongozi waki neemeka

alafu wala hawashtuki na ukiwashtua wanaliamsha dude kukushambulia.
 
Page+3.JPG

Polisi yatoa onyo la mwisho kwa Wasabato Masalia

KUNDI la waumini wa Dhehebu la Waadventista Wasabato Masalia, kwa mara ya tatu limesambaratishwa na askari wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kurudi tena uwanjani hapo huku wakiwa wameongezeka idadi yao kutoka 17 hadi kufikia 51.

Wasabato hao masalia, walifika katika uwanja huo mnamo saa 2:00 asubuhi huku wakiwa na mabegi yao tayari kwa safari wakisema: "Bwana alikuwa amewaambia tena kuwa jana ilikuwa ndio siku ya kuondoka na kuelekea nchi za Ulaya kuhubiri injili."
Na Furaha Kijingo
Asante kwa kumbukumbu mujarabu Miss Natafuta . Nami nimewakumbuka hawa baada ya Mkuu mshana jr kuleta bandiko lake. Kwenye dini kuna vituko sana. Ndiyo maana dini kwasasa inapoteza mvuto. Ni utapeli na vituko kwa kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom