Elimu kuhusu dini

Elimu kuhusu dini

THE SPIRIT THINKER

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2019
Posts
419
Reaction score
654
KAMA NITAKUKWAZA WEWE UNAYE SOMA UZI HUU NAOMBA UNISAMEHE MAANA NAKWENDA KUONGELEA ELIMU YA KWELI KUHUSU DINI NA CHANZO CHAKE.

Tutazungumza kwa urefu zaidi jinsi dini fulani fulani zilivyoanza na kusitawi. Utakuta inanurisha si kujua tu jinsi kila dini ilivyo tofauti na nyinginezo bali pia jinsi inavyofanana nazo. Pia utaweza kujua jinsi kila dini inavyoingia katika mpangilio wa wakati wa historia ya kibinadamu na historia ya dini, jinsi kitabu au maandishi yayo matakatifu yanavyohusiana na mengine, jinsi mwanzilishi au kiongozi wayo alivyovutwa na mawazo mengine ya kidini, na jinsi imekuwa na uvutano juu ya mwenendo na historia ya ainabinadamu. Ukizingatia mambo haya akilini, kujifunza juu ya jitihada ya ainabinadamu ya kutafuta Mungu ambayo imechukua muda mrefu Mungu kutakusaidia uone kwa uwazi zaidi ukweli juu ya dini na mafundisho ya kidini.

SITOPENDELEA DINI YEYOTE NITAJITAHIDI KUELEZEA KWA MAPANA KILA DINI NA KUFICHUA MAMBO YA SIRINI KABISA YA KILA DINI.HATA DINI ZA ASILI NITAZIELEZEA KWA KIWANGO CHA KAWAIDA SITOZAMA NDANI.KUMBUKA SITOAIBISHA DINI BALI NITAIELEZEA KAMA ILIVYO.

LAKINI YEYOTE ANARUHUSIWA KUNIKOSOA NA KUPANUA MADA HII MAANA INA MASWALI NA MAJIBU KWA AJIRI YA KUSHIRIKI MAJADILIANO.HII NI ELIMU YA WAZI KWA WOTE HIVYO UNARUHUSIWA KUTOA HOJA ZAKO LAKINI ZIWE NA UDHIBITISHO MAANA NAMI NITAONGEA KWA KUNUKUU VITABU VILIVYO TOA HOJA HIZI ZOTE KUHUSU ELIMU YA KWELI KUHUSU DINI NA IMANI.
Sura 1

Kwa Nini Kupendezwa na Dini Nyingine?1-7.

Ni nini baadhi ya madhihirisho ya dini mbalimbali za ulimwengu?BILA kujali waishi wapi, bila shaka umejionea mwenyewe jinsi dini inavyoongoza maisha za mamilioni ya watu, labda na yako pia. Katika nchi ambazo Uhindu unazoewa, mara nyingi utawaona watu wakifanya puja—sherehe ambayo yaweza kuhusisha kutoa sadaka kwa vijimungu vyao, kwa namna ya nazi, maua, na matofaa. Kuhani anapaka rangi nyekundu au ya manjano, yaani tilak, kwenye vipaji vya nyuso za waumini. Mamilioni pia humiminika kila mwaka kwenye mto Ganges watakaswe na maji yao.Katika nchi za Katoliki, utaona watu wakisali katika makanisa na makathedro huku wameshika kisalaba au tasbihi. Shanga za tasbihi zinatumiwa kuhesabia sala zinazotolewa kwa ujitoaji wao kwa Mariamu. Na si vigumu kutambua watawa wa kike na makasisi, wanaotofautishwa na kanzu zao nyeusi. Katika mabara ya Kiprotestanti, vikanisa na makanisa ni tele, na siku ya Jumapili wafuasi kwa kawaida huvaa nguo zao bora na kukusanyika waimbe nyimbo za dini na kusikia mahubiri.

Mara nyingi makasisi wao huvaa mavazi meusi na kola ya kikasisi yenye kuwatofautisha.Katika nchi za Kiislamu, unaweza kusikia sauti za waadhini, wapiga mbiu Waislamu wakiipiga kwenye vinara vya misikiti mara tano kila siku, kuwaita waamini kwenye s̩alãt, au sala ya sherehe. Wao huiona Qurani Tukufu kuwa kitabu cha Kiislamu cha maandiko matakatifu. Kulingana na imani ya Kiislamu, kilifunuliwa na Mungu akapewa nabii Muhammad na malaika Gabrieli katika karne ya saba W.K.Kwenye barabara za mabara mengi ya Kibuddha, watawa wa Dini ya Buddha, kwa kawaida wakiwa wamevaa majoho ya dhahabu-nyekundu, meusi, au mekundu, huonekana kuwa ishara ya mtu kuwa wa dini.

Mahekalu ya kale yanayoonyesha Buddha mtulivu ni uthibitisho wa zamani za kale wa imani ya Kibuddha. Dini ya Shinto ikiwa inazoewa katika Japan, inahusu maisha za kila siku kukiwa na vihekalu vya familia na matambiko kwa wazazi wa kale waliokufa. Wajapan huhisi huru kusali kwa ajili ya mambo ya kimwili kabisa, hata juu ya kufaulu katika mitihani ya shuleni.

Utendaji mwingine wa kidini unaojulikana ulimwenguni pote ni ule wa watu wanaoenda nyumba kwa nyumba na kusimama kwenye barabara wakiwa na Biblia na vitabu vya Biblia. Magazeti Mnara wa Mlinzi na Amkeni! yakionekana wazi, karibu kila mtu anawatambua watu hao kuwa Mashahidi wa Yehova.8. Historia ya ujitoaji kidini inaonyesha nini?Unamna-namna huu mkubwa wa ujitoaji wa kidini ulimwenguni pote waonyesha nini? Kwamba kwa maelfu ya miaka ainabinadamu wamekuwa na uhitaji na tamaa ya kiroho. Binadamu ameishi na majaribu na mizigo, tashwishi na maswali yake, kutia ndani kitendawili cha kifo. Hisia za kidini zimeonyeshwa katika njia nyingi kwa watu kugeukia Mungu au vijimungu vyao, wakitafuta baraka na utulizo. Dini pia hujaribu kushughulikia maswali makubwa: Kwa nini sisi tupo hapa? Tuishije? Wakati ujao una nini kwa ajili ya ainabinadamu?9. Ni katika njia gani watu walio wengi wana namna zao za ujitoaji kidini maishani mwao?Kwa upande mwingine, kuna mamilioni ya watu wasiodai kuwa na dini yoyote wala imani yoyote katika kijimungu chochote. Wao ni waatheisti. Wengine, waagnosti, huamini kwamba Mungu hajulikani na yaelekea hawezi kujulikana. Hata hivyo, hilo kwa wazi halimaanishi kwamba wao ni watu wasio na kanuni wala maadili, kama ambavyo kudai kuwa na dini kusivyomaanisha kwamba mtu anazo. Hata hivyo, mtu akikubali dini kuwa “ujitoaji kwa kanuni fulani; utumainifu imara au uaminifu; udhamiriaji; shauku ya kufuata dini au ufungamano,” basi watu walio wengi, kutia waatheisti na waagnosti, wana namna fulani ya ujitoaji wa kidini maishani mwao.—The Shorter Oxford English Dictionary.10. Je! dini ina mshindo juu ya ulimwengu wa kisasa? Toa kielezi.Kwa kuwa kuna dini nyingi mno katika ulimwengu unaozidi kuwa mdogo zaidi na zaidi kwa sababu ya usafiri na uwasiliano wa kasi zaidi, mshindo wa imani mbalimbali huhisiwa ulimwenguni pote, tutake-tusitake. Kasirani iliyotokea mnamo 1989 kuhusu kitabu The Satanic Verses, kilichoandikwa na mtu ambaye watu wengine walimtaja kuwa ‘Mwislamu kafiri,’ ni uthibitisho ulio wazi wa jinsi fikira ya kidini yaweza kujidhihirisha kwa kiwango cha duniani pote. Kulikuwako wito kutoka viongozi wa Kiislamu kuwa kitabu hicho kipigwe marufuku na hata mtungaji wacho auawe. Ni nini kinachofanya watu wamenyuke vikali sana katika mambo ya dini?11. Kwa nini si kosa kuchunguza imani nyingine?Ili kujibu hilo, tunahitaji kujua jambo fulani juu ya chanzo cha dini za ulimwengu. Ni kama Geoffrey Parrinder anavyotoa taarifa katika World Religions—From Ancient History to the Present: “Kuchunguza dini tofauti-tofauti kwa lazima hakumaanishi mtu anakosa uaminifu kwa imani yake mwenyewe, bali huenda ikazidishwa kwa kuona jinsi watu wengine wametafuta uhalisi wa mambo na wakathawabishwa sana na jitihada yao ya kutafuta.” Maarifa huongoza kwenye kupata kuelewa, na kuelewa kwenye uvumilio wa watu wenye maoni tofauti.Kwa Nini Kuchunguza?12. Ni mambo gani ambayo kwa kawaida huamua dini ya mtu?Je! wewe umepata kufikiri au ukasema, ‘Mimi nina dini yangu mwenyewe. Hilo ni jambo la kibinafsi kabisa.

Mimi siizungumzi pamoja na wengine’? Ni kweli dini ni jambo la kibinafsi kabisa—karibu tangu kuzaliwa mawazo ya kidini au ya kiadili yanapandikizwa katika akili yetu na wazazi na watu wa ukoo. Tokeo ni kwamba, kwa kawaida sisi hufuata mafikira ya kidini ya wazazi wetu na ya wazazi wa wazazi wetu. Kwa ujumla dini imekuwa utamaduni wa familia. Matokeo ya hatua hiyo yamekuwa nini? Kwamba katika visa vingi wengine wametuchagulia sisi dini yetu. Karibu imetegemea mahali na wakati tulipozaliwa. Au, kama mwanahistoria Arnold Toynbee alivyoonyesha, kuambatana kwa mtu na imani fulani mara nyingi huamuliwa na “tukio la kijiografia la mahali alipozaliwa.”13, 14. Kwa nini si jambo la akili kuwaza kwamba dini aliyozaliwa nayo mtu ni yenye kuidhinishwa na Mungu moja kwa moja?Je! ni jambo la akili kudhania kwamba dini ambayo ilipandikizwa wakati wa mtu kuzaliwa kwa lazima ndio ukweli mzima?

Kama ulizaliwa Italia au Amerika Kusini, basi, bila ya uchaguzi wowote, yaelekea ulilelewa ukiwa Mkatoliki. Kama ulizaliwa katika India, basi yaelekea moja kwa moja ulikuwa Mhindu au, kama unatoka Punjabi, labda wewe ni wa Dini ya Sikh. Kama wazazi wako walitoka Pakistan, basi kwa wazi ungekuwa Mwislamu. Na kama ulizaliwa katika nchi ya Siasa za Kijamaa katika makumi machache ya miaka yaliyopita, huenda ikawa hukuwa na uchaguzi wowote bali kulelewa ukiwa mwaatheisti.—Wagalatia 1:13, 14; Matendo 23:6.

Kwa hiyo, je! dini aliyozaliwa nayo mtu inakuwa moja kwa moja ndiyo ya kweli, yenye kuidhinishwa na Mungu? Kama wazo hilo ndilo lingefuatwa kwa maelfu ya miaka iliyopita, wengi kati ya ainabinadamu wangekuwa wangali wanazoea ushamani wa kikale na ibada za nguvu za uzazi za kale, kwa msingi wa kwamba ‘kilichokuwa kizuri vya kuwatosha wazazi wangu wa kale waliokufa ni kizuri vya kunitosha.’
 
15, 16. Kuna manufaa gani katika kuchunguza dini nyingine?Kwa sababu ya unamna mpana wa wonyesho wa kidini ambao umesitawi kuuzunguka ulimwengu kwa miaka 6,000 iliyopita, angalau ni jambo lenye kuelimisha na kupanua akili kuelewa mambo ambayo wengine husadiki na jinsi itikadi zao zilivyoanza. Na kwaweza pia kufungua mataraja ya tumaini lililo imara zaidi la wakati wako ujao.Katika nchi nyingi sasa, kwa sababu ya uhamiaji na kusonga-songa kwa watu, watu wa dini tofauti-tofauti hushiriki ujirani mmoja. Kwa hiyo, kuelewa maoni ya mmoja na mwenzake kwaweza kuongoza kwenye uwasiliano na mazungumzo yenye maana kati ya watu wa imani tofauti-tofauti. Labda, pia, kwaweza kuondoa ulimwenguni chuki fulani ambayo msingi ni tofauti za kidini. Ni kweli, watu wanaweza kutokubaliana sana kuhusu itikadi zao za kidini, lakini hakuna msingi wa kuchukia mtu mwingine kwa sababu tu yeye hushikilia maoni tofauti.—1 Petro 3:15; 1 Yohana 4:20, 21; Ufunuo 2:6.17. Kwa nini hatupaswi kuwachukia wale ambao kuwaza kwao kidini hutofautiana na kwetu?Sheria ya kale ya Kiyahudi ilitoa taarifa hii: “Wewe hutamchukia mtu wa jamaa yako katika moyo wako. Karipia mtu wa jamaa yako lakini usipate hatia yoyote kwa sababu yake. Wewe hutalipa kisasi wala kuwa na kinyongo juu ya watu wa nchi yako. Mpende mwenzako kama wewe mwenyewe: Mimi ndimi BWANA [Yehova].” (Mambo ya Walawi 19:17, 18, Ta) Mwanzilishi wa Ukristo alitoa taarifa hii: “Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wanawachukia ninyi, . . . na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.” (Luka 6:27, 35) Chini ya kichwa “Mwanamke Ambaye Ni wa Kufanyiwa Mtihani,” Qurani hutoa taarifa juu ya kanuni kama hiyo (surah 60:7): “Asaa Mwenyezi Mungu atatia mapenzi baina yenu na hao maadui zenu, na Mwenyezi Mungu ni Muweza. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.”18. Ni jinsi gani yale anayoamini mtu hufanya tofauti?Hata hivyo, ingawa uvumilio na uelewevu vyahitajiwa, hilo halimaanishi kwamba haifanyi tofauti mtu huamini nini. Kama mwanahistoria Geoffrey Parrinder alivyotoa taarifa hii: “Nyakati nyingine husemwa kwamba dini zote zina mradi ule ule, au hizo ni njia zinazolingana za kuongoza kwenye ukweli, au hata kwamba zote zinafunza mafundisho yale yale . . . Lakini Waazteki wa kale, walionyanyua kuelekea jua mioyo yenye kudunda ya wahanga wao, kwa hakika hawakuwa na dini nzuri kama ile ya Wabuddha wapenda amani.” Kuongezea hayo, inapohusu ibada, je! Mungu mwenyewe siye anayepaswa kuamua kinachokubalika na kisichokubalika?—Mika 6:8.Dini Ipimweje?19. Dini yapasa kuathirije mwenendo wa mtu?Ingawa dini zilizo nyingi zina fungu la itikadi au mafundisho, mara nyingi zinatokeza theolojia yenye kutatanisha sana, asiyoweza kuelewa kabwela. Hata hivyo kanuni ya kisababishi na matokeo hutumika katika kila kisa. Mafundisho ya dini yapasa kuongoza utu na mwenendo wa kila siku wa kila mwumini. Hivyo, mwenendo wa kila mtu kwa kawaida utakuwa ni mwakisho, kwa kadiri kubwa au ndogo, wa msingi wa kidini wa mtu huyo. Dini yako ina matokeo gani juu yako? Je! dini yako inatokeza mtu mfadhili zaidi? Mkarimu, mnyoofu, mnyenyekevu, mvumiliaji, na mhurumiaji zaidi? Hayo ni maswali ya kufikiri kuzuri, kwa maana kama mwalimu mmoja mkuu wa kidini, Yesu Kristo alivyotoa taarifa hii: “Kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.”—Mathayo 7:17-20.20. Ni maswali gani yanayotokea kwa habari ya dini na historia?Bila shaka historia ya kilimwengu lazima itufanye tutue na kutufanya tutake kujua dini imekuwa na jukumu gani katika vita vingi ambavyo vimetatiza ainabinadamu na kusababisha taabu isiyo na kifani. Ni kwa nini watu wengi mno wameua na kuuawa katika jina la dini? Zile Krusedi (vita vitakatifu), Mahakama za Kuhukumia Wazushi wa Kidini, mapambano katika Mashariki ya Kati na Ireland Kaskazini, machinjo kati ya Iraq na Iran (1979-87), migongano ya Wahindu na wafuasi wa Dini ya Sikh katika India—matukio hayo yote kwa hakika yanawafanya watu wanaofikiri watokeze maswali juu ya itikadi na maadili ya kidini.—Ona kisanduku chini.21. Ni nini baadhi ya vielelezo vya matunda ya Jumuiya ya Wakristo?Makao ya Jumuiya ya Wakristo yametokeza sana kwa ajili ya unafiki wayo katika uwanja huu. Katika vita vya ulimwengu viwili, Mkatoliki ameua Mkatoliki na Mprotestanti ameua Mprotestanti kwa kuchochewa na viongozi wao wa kisiasa “Wakristo.” Hata hivyo, Biblia inatofautisha matendo ya mwili na matunda ya roho. Kwa habari ya matendo ya mwili, inatoa taarifa hii: “Ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo; katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” Hata hivyo waitwao Wakristo wamezoea mambo hayo kwa karne nyingi, na mwenendo wao mara nyingi umeachiliwa na makasisi wao.—Wagalatia 5:19-21.22, 23. Kinyume cha hayo, dini ya kweli yapasa kuzaa matunda gani?Kinyume cha hayo, matunda ya roho yaliyo mazuri yanasimuliwa kama: “upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” Dini zote zapasa kuwa zikizaa matunda ya aina hii yenye amani. Lakini zinafanya hivyo? Je! ile yako inafanya hivyo?—Wagalatia 5:22, 23.Kwa hiyo, uchunguzi wa kitabu hiki juu ya jitihada ya ainabinadamu ya kutafuta Mungu kupitia dini za ulimwengu yapasa kutumika kujibu baadhi ya maswali yetu. Lakini dini yapasa kuhukumiwa kwa viwango gani? Kwa viwango vya nani?‘Dini Yangu Ni Nzuri vya Kunitosha’24, 25. Ni tatizo gani analotokezewa kila mtu kwa habari ya dini yake?Watu wengi wanapuuza mazungumzo ya kidini kwa kusema, ‘Dini yangu ni nzuri vya kunitosha. Mimi simdhuru mtu mwingineye yote, nami husaidia niwezapo.’ Lakini hayo yatosha? Je! viwango vyetu vya kibinafsi kuhusu dini vyatosha?Ikiwa dini ni “wonyesho wa imani ya mtu na heshima kubwa kwa uwezo unaozidi nguvu za kibinadamu unaotambuliwa kuwa muumba na msimamizi wa ulimwengu wote,” kama ambavyo kamusi moja inavyotoa taarifa, basi bila shaka swali lapasa kuwa hili, Je! dini yangu ni nzuri kumtosha muumba na msimamizi wa ulimwengu wote mzima? Pia, katika kisa hicho, Muumba angekuwa na haki ya kuamua ni nini mwenendo, ibada, na fundisho vyenye kukubalika au visivyokubalika. Ili kufanya hivyo, ni lazima yeye afunue mapenzi yake kwa ainabinadamu, na ufunuo huo lazima uwe unapatikana na kufikiwa kwa urahisi na wote. Kuongezea hayo, ufunuo wake, hata ingawa ulitolewa muda wa karne nyingi tofauti-tofauti, sikuzote wapasa kuwa wenye kukubaliana na kupatana. Hilo linatokeza tatizo kwa kila mtu—kuchunguza uthibitisho na mtu kujithibitishia ni nini mapenzi ya Mungu yanayokubalika.26. Ni kitabu gani kitakatifu kinachopaswa kutumika kuwa kipimio cha ibada ya kweli? Na kwa nini?Kimoja cha vitabu vya kale zaidi kinachodai kuwa na pumzi ya Mungu ni Biblia. Pia ndicho kitabu kilichoenezwa zaidi na kutafsiriwa zaidi katika historia yote. Karibu miaka elfu mbili iliyopita, mmoja wa waandikaji wacho alitoa taarifa hii: “Msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” (Warumi 12:2) Chanzo cha uthibitisho huo kingekuwa nini? Mwandikaji uyo huyo alitoa taarifa hii: “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” Kwa hiyo, Biblia iliyopuliziwa na Mungu yapasa kutumika kuwa kipimio chenye kutegemeka cha ibada ya kweli na yenye kukubalika.—2 Timotheo 3:16, 17.27. (a) Baadhi ya maandishi matakatifu ya dini fulani za kilimwengu ni yapi? (b) Mafundisho yayo yapaswa kulinganaje na yale ya Biblia?Kisehemu cha kale zaidi cha Biblia ni cha tarehe ya mapema zaidi ya maandishi mengineyo yote ya kidini. Tora, au vitabu vitano vya kwanza vya Biblia, Sheria iliyoandikwa na Musa akiwa na pumzi ya Mungu, ni ya tarehe ya kurudi nyuma kwenye karne za 15 na 16 K.W.K. Kwa kulinganisha, maandishi ya Hindu ya Rig-Veda (mkusanyo wa nyimbo za dini) yalikamilishwa yapata 900 K.W.K. wala hayadai yana pumzi ya kimungu. “Kanuni ya Vikapu Vitatu” ya Kibuddha ni vya tarehe inayorudi nyuma kwenye karne ya tano K.W.K. Qurani, inayodaiwa kuwa ilipokewa kutoka kwa Mungu kupitia malaika Gabrieli, ilitokezwa katika karne ya saba W.K. Kitabu cha Mormon, kinachoripotiwa kuwa alipewa Joseph Smith katika United States na malaika aitwaye Moroni, kilitokezwa karne ya 19. Ikiwa baadhi ya vitabu hivi vimepuliziwa kimungu kama wanavyodai wengine, basi mambo ambayo vinatoa kwa habari ya mwongozo wa kidini hayapasi kupingana na mafundisho ya Biblia, kwani ndiyo chanzo cha awali kilichopuliziwa na Mungu. Pia vinapasa kujibu baadhi ya maswali ambayo ainabinadamu wanataka sana kujua.
 
Sura 2

Dini Ilianzaje?

















1, 2. Ni nini kimeonwa kwa habari ya ukale na unamna-namna mkubwa wa dini?HISTORIA ya dini ni ya tangu kuwapo kwa binadamu mwenyewe. Ndivyo watuambiavyo waakiolojia na waanthropolojia. Hata kati ya walio “wa kikale” zaidi, yaani, staarabu zisizostawika, kunapatikana uthibitisho wa ibada ya namna fulani. Kwa kweli The Encyclopædia Britannica chasema kwamba “kadiri ambayo wasomi wamevumbua, hakujapata kuwako watu, popote, wakati wowote ule, ambao hawakuwa wa kidini katika maana fulani.”Zaidi ya ukale wake, dini pia hupatikana ikiwa yenye unamna-namna mkubwa. Wawinda vichwa katika mapori ya Borneo, Waeskimo katika Aktiki yenye barafu, wahamaji katika Jangwa Sahara, wakaaji wa mjini katika majiji makubwa ya ulimwengu—kila kikundi cha watu na kila taifa duniani lina kijimungu au vijimungu vyao na njia yao ya kuabudu. Utofautiano katika dini kwa kweli ni mkubwa ajabu.3. Ni maswali gani kuhusu dini za ulimwengu yanayopasa kufikiriwa?Kwa kufikiri kuzuri maswali yanakuja akilini. Dini hizi zote zilitoka wapi? Kwa kuwa kuna tofauti kubwa na ufanani kati yazo, je! zilianza kila moja ki-vyake, au zaweza kuwa zilisitawi kutoka chanzo kimoja? Kwa kweli huenda tukauliza: Hasa kwa nini dini ikaanza? Na jinsi gani? Majibu ya maswali hayo ni yenye umaana mkubwa kwa wote wanaopendezwa na kujua ukweli juu ya dini na imani za kidini.Suala Juu ya Asili4. Twajua nini juu ya waanzilishi wa dini nyingi?Inapohusu suala la asili, watu wa dini tofauti-tofauti hufikiria majina kama Muhammad, Buddha, Confucius, na Yesu. Karibu katika kila dini, kuna mhusika mkuu ambaye hupewa sifa ya kuanzisha ‘imani ya kweli.’ Baadhi ya hao walikuwa ni wapinduzi wa kidini wachukiao sanamu. Wengine walikuwa ni wanafalsafa wa kiadili. Na bado wengine walikuwa ni mashujaa wa taifa wasio na ubinafsi. Wengi wao wameacha maandishi au semi ambazo zilifanyiza msingi wa dini mpya. Baada ya muda kupita mambo waliyosema na kufanya yalifafanuliwa, yakatiwa madoido, na kufanywa kuwa ya kifumbo. Baadhi ya viongozi wao hata walifanywa kuwa viabudiwa.5, 6. Dini nyingi zilianzaje?Hata ingawa watu hao mmoja mmoja walionwa kuwa waanzilishi wa dini zile kubwa-kubwa ambazo tumezizoelea, yapasa kuangaliwa kwamba wao hawakuanzisha dini hasa. Katika visa vilivyo vingi, mafundisho yao yalitokana na mawazo ya kidini yaliyokuwapo tayari, hata ingawa wengi wa waanzilishi hawa walidai upulizio wa kimungu kuwa chanzo chayo. Au walibadili na wakarekebisha upya mifumo ya kidini iliyokuwapo ambayo ilikuwa imekuwa isiyoridhisha katika njia hii au hii.Kielelezo, kwa usahihi ambao historia inaweza kutuambia, Buddha alikuwa mwana-mfalme aliyeudhiwa sana na mateso na hali zenye kusikitisha alizokuta zinamzunguka katika jamii iliyotawalwa na Uhindu. Dini ya Buddha ilisababishwa na jitihada yake ya kutafuta suluhisho la matatizo ya maisha yenye kuumiza. Hali moja na hiyo, Muhammadi alihangaishwa sana na ibada ya sanamu na ukosefu wa adili alioona katika mazoea ya kidini yaliyomzunguka. Baadaye yeye alidai alipokea wahyi (mafunuo maalumu) mbalimbali kutoka kwa Mungu, ambayo yakawa ndiyo Kurani na kuwa msingi wa chama kipya cha kidini, Uislamu. Uprotestanti ulikuwa chipukizi la Ukatoliki ukiwa tokeo la Mapinduzi Makubwa ya Kidini yaliyoanza mapema katika karne ya 16, wakati Martin Lutheri alipopinga kanisa Katoliki kuuza hati za rehema.7. Ni swali gani kuhusu dini ambalo lingali lahitaji kujibiwa?Basi, kwa habari ya dini zilizopo sasa, hakuna ukosefu wa habari kuhusu asili yazo na usitawi wazo, waanzilishi, maandishi yazo matakatifu, na kadhalika. Lakini namna gani juu ya dini zilizokuwapo kabla yazo? Na zile za hata kabla ya hizo? Tukirudi nyuma vya kutosha katika historia, muda si muda tutakabiliwa na swali hili: Dini ilianzaje? Kwa wazi, ili kupata jibu la swali hilo, ni lazima tuangalie mbali zaidi ya mipaka ya dini moja moja.Nadharia Nyingi8. Kwa karne nyingi, ni nini mtazamo wa watu kuelekea dini?Funzo la asili na usitawi wa dini ni uwanja mpya kwa kulinganisha. Kwa karne nyingi, kwa ujumla watu walikubali pokeo la dini ambamo katika hilo walizaliwa na ambamo katika hilo walilelewa. Wengi wao waliridhika na maelezo waliyopokezwa na mababu zao, wakihisi kwamba dini yao ilikuwa ndio ukweli. Ni mara chache kulipokuwako sababu ya kuwa na tashwishi ya lolote, au uhitaji wa kuchunguza jinsi, lini, au kwa nini mambo yakaanza. Kwa kweli, kwa karne nyingi, kukiwapo uchache wa njia za usafiri na uwasiliano, hata ni watu wachache waliojua kuna mifumo mingine ya kidini.9. Tangu karne ya 19, ni majaribio gani yamefanywa kuvumbua jinsi na kwa nini dini ilianza?Hata hivyo, wakati wa karne ya 19, picha hiyo ilianza kubadilika. Nadharia ya mageuzi ilikuwa ikisambaa kati ya wenye elimu kubwa. Jambo hilo, pamoja na kuwadia kwa utafiti wa kisayansi, vilisababisha wengi wawe na tashwishi ya mifumo iliyoimarishwa, kutia na dini. Wakitambua vizuizi vya kutafuta vidokezi ndani ya dini iliyokuwapo, wasomi fulani waligeukia masalio ya staarabu za mapema au kwenye ncha za mbali za ulimwengu ambako watu walikuwa wangali wakiishi katika jumuiya za kikale. Walijaribu hayo kwa kutumia mbinu za saikolojia, sosholojia, anthropolojia, na kadhalika, wakitumaini kuvumbua dokezi juu ya jinsi dini ilivyoanza na kwa nini.10. Kukawa nini kwa sababu ya machunguzo ya asili ya dini?Kukawa nini? Ghafula, kukatokea nadharia nyingi—nyingi kama hesabu ya wachunguzi wenyewe—kila mchunguzi akipinganisha za mwenzake, na kila mmoja akijitahidi kumshinda yule mwingine katika kuthubutu na uvumbuzi. Baadhi ya watafiti hao walifikia mikataa ya maana; kazi ya wengine imefanya kusahauliwa tu. Sisi tunapotupia macho matokeo ya utafiti huo tunaelimika na kunurishwa. Itatusaidia tupate uelewevu bora zaidi wa mitazamo ya kidini kati ya watu tunaokuta.11. Fafanua nadharia ya animism.Nadharia ambayo kwa kawaida inaitwa animism (ibada ya maumbile), ilipendekezwa na mwanthropolojia Mwingereza Edward Tylor (1832-1917). Yeye alidokeza kwamba mambo kama vile ndoto, njozi, chechele, na maiti kutokuwa na uhai yalisababisha watu wa kikale wakate maneno kwamba mwili ni makao ya nafsi (Kilatini, anima). Kulingana na nadharia hiyo, kwa kuwa mara nyingi waliota juu ya wapendwa wao waliokufa, walidhani kwamba nafsi iliendelea kuishi baada ya kifo, kwamba iliuacha mwili na kukaa katika miti, miamba, mito, na kadhalika. Hatimaye, wafu na vitu ambavyo ilisemekana nafsi inakaa ndani yavyo vikaja kuabudiwa kuwa vijimungu. Na hivyo, asema Tylor, dini ikazaliwa.12. Fafanua nadharia ya animatism.Mwanthropolojia mwingine, R. R. Marett (1866-1943), alipendekeza animism inolewe zaidi, akaiita animatism. Baada ya kuchunguza imani za Wamelanesia wa visiwa vya Pasifiki na wenyeji wa Afrika na Amerika, Marett alikata maneno kwamba badala ya kuwa na wazo la nafsi ya kibinafsi, watu wa kikale waliamini kuna kani isiyo na utu au nguvu fulani zinazozidi zile za kibinadamu zilizohuisha kila kitu; imani hiyo ilitokeza hisia-moyo zenye kutisha na kutia hofu binadamu, hayo yakawa msingi wa dini hii ya kikale. Kwa Marett, dini kwa sehemu kubwa ilikuwa itikio la hisia-moyoni la binadamu kwa yale yasiyojulikana. Taarifa yake aliyopenda zaidi ilikuwa kwamba dini “haikuwa imefikiriwa sana kwa kiasi ambacho ilifuatwa.”13. Ni nadharia gani ya dini aliyopendekeza James Frazer?Mwaka 1890 mtaalamu wa Scotland wa masimulizi ya wenyeji, James Frazer (1854-1941), alichapisha kitabu chenye uvutano The Golden Bough, ambamo alitoa hoja kwamba dini ilitokana na mizungu. Kulingana na Frazer, binadamu kwanza alijaribu kuongoza uhai wake mwenyewe na mazingira yake kwa kuiga aliyoona yanatukia katika maumbile ya asili. Kwa kielelezo, aliwaza kwamba angeweza kuita mvua inye kwa kunyunyiza maji kwenye ardhi kwa kuambatana na midundo ya ngoma yenye kusikika kama radi au kwamba angeweza kumdhuru adui yake kwa kudunga pini kisanamu fulani. Jambo hilo liliongoza kwenye matumizi ya sherehe, ulozi, na vidude vya uchawi katika sehemu nyingi za maisha. Viliposhindwa kufanya yaliyotazamiwa, ndipo alipogeukia kutambika na kusihi msaada wa nguvu zinazozidi zile za kibinadamu, badala ya kujaribu kuziongoza. Sherehe na maneno ya kunuizia uchawi yakawa dhabihu na sala, na kwa njia hiyo dini ikaanza. Kwa maneno ya Frazer, dini ni “upatanisho au usuluhisho wa nguvu zinazozidi binadamu.”14. Sigmund Freud alifafanuaje asili ya dini?Hata yule Mwaustria mchanganua akili maarufu Sigmund Freud (1856-1939), katika kitabu chake Totem and Taboo, alijaribu kueleza asili ya dini. Kwa kupatana na kazi yake, Freud alieleza kwamba dini ya mapema kabisa ilikuwa chipukizi la kile alichoita hamaniko lisababishwalo kwa kuhofu umbo-baba. Yeye alitoa nadharia kwamba, kama ilivyo na farasi-mwitu na ng’ombe, katika jumuiya ya kikale baba alitawala jamii. Wana, ambao walimchukia baba na pia kumstaajabia, waliasi na wakamwua huyo baba. Ili wajipatie uwezo wa baba, akadai Freud, ‘washenzi hao wala-watu walimla waliyemwua.’ Baadaye, kwa sababu ya kusikitika, wakabuni desturi za kufunika kitendo chao. Kulingana na nadharia yake Freud, umbo hilo la baba likawa Mungu, sherehe hizo zikawa dini ya mapema kabisa, na kuliwa kwa baba aliyechinjwa kukawa lile pokeo la kula kishirika linalozoewa katika dini nyingi.15. Nadharia nyingi zilizopendekezwa kuhusu asili ya dini zimepatwa na nini?Nadharia nyingine nyingi ambazo ni majaribio ya kufafanua asili ya dini zingeweza kutajwa. Hata hivyo, nyingi za hizo zimekwisha sahauliwa, na hakuna yoyote ya hizo ambayo imetokeza kuwa yenye kuthibitika zaidi au kukubaliwa zaidi ya zile nyingine. Kwa nini? Kwa sababu tu hakujapata kuwapo ushuhuda au uthibitisho wowote wa kihistoria kwamba nadharia hizo zilikuwa za kweli. Zilikuwa mazao tu ya kuwaza au dhana ya mchunguzi fulani, ambazo upesi mahali pazo pakachukuliwa na ile nyingine iliyofuata.Msingi Wenye Kosa16. Ni kwa nini miaka mingi ya uchunguzi imeshindwa kutokeza ufafanuzi juu ya jinsi dini ilivyoanza?Baada ya miaka mingi ya kung’ang’ana na suala hilo, wengi sasa wamefikia mkataa kwamba haielekei sana kwamba kutakuwako fanikio lolote la kupata jibu la swali la jinsi dini ilivyoanza. Kwanza, hii ni kwa sababu mifupa na masalio ya watu wa kale havituambii jinsi watu hao walivyofikiri, walichohofu, au ni kwa nini wao waliabudu. Mikataa yoyote inayofikiwa kutokana na vitu hivyo vya kale ni makisio yenye msingi wa kielimu. Pili, mazoea ya kidini ya wanaoitwa leo washenzi, kama vile Waaborijini wa Kiaustralia, kwa lazima si kipimio chenye kutegemeka cha kupima mambo ambayo watu wa nyakati za kale walifanya au kuwaza. Hakuna anayejua kwa uhakika kama au jinsi utamaduni wao ulivyobadilika wakati wa karne nyingi zilizopita.17. (a) Wanahistoria wa dini wa ki-siku-hizi wanajua nini? (b) Ni nini linaloonekana kuwa hangaikio kuu wakati wa kuchanganua dini?Kwa sababu ya yote hayo yasiyo ya hakika, kitabu World Religions—From Ancient History to the Present kinakata maneno kwamba “mwanahistoria wa ki-siku-hizi wa dini anajua kwamba haiwezekani kuzifikia asili za dini.” Hata hivyo, kwa habari ya jitihada za wanahistoria, kitabu hicho chaonelea hivi: “Wakati uliopita wananadharia wengi walihangaikia si kusimulia au kufafanua tu dini bali kutoa ufafanuzi wa kuibatilisha, wakihisi kwamba kama namna za zamani zingeonyeshwa zilitegemea udhanifu basi dini za baadaye na za hali ya juu zaidi huenda zikazoroteshwa.”18. (a) Ni kwa nini wachunguzi wengi wamekosa kufaulu kufafanua asili ya dini? (b) Yaonekana kuwa ni nini yaliyokuwa madhumuni ya wachunguza dini wa “kisayansi”?Katika maelezo hayo ya mwisho mna kidokezi cha ni kwa nini wachunguzi mbalimbali wa “kisayansi” wa asili ya dini hawajatokeza ufafanuzi wowote wenye kuthibitika. Kufikiri vizuri hutuambia kwamba mkataa sahihi waweza kufikiwa kutokana tu na dhana sahihi. Mtu akianza na dhana yenye kosa, haielekei yeye atafikia mkataa timamu. Kushindwa tena na tena kwa wachunguzi wa “kisayansi” kutokeza ufafanuzi wa kiakili kwatokeza tashwishi kubwa zilizo juu ya dhana ambayo walitegemeza maoni yao. Kwa kufuata wazo lao lililofikiriwa kimbele, katika jitihada zao za ‘ufafanuzi wa kuibatilisha dini’ wamejaribia kutoa ufafanuzi wa kupuuza kuwapo kwa Mungu.19. Ni nini iliyo kanuni ya msingi yenye kuongoza machunguzo ya kisayansi yenye kufanikiwa? Tafadhali toa kielezi.Hali hiyo yaweza kulinganishwa na zile njia nyingi ambazo wataalamu wa nyota na anga kabla ya karne ya 16 walijaribu kufafnua mwendo wa sayari. Kulikuwako nadharia nyingi, lakini hakuna yoyote ya hizo iliyokuwa yenye kuridhisha kweli kweli. Kwa nini? Kwa sababu zilitegemea udhanifu wa kwamba dunia ilikuwa ndicho kitovu cha ulimwengu wote mzima ambacho nyota na sayari zilizunguka. Maendeleo halisi hayakufanywa mpaka wanasayansi—na Kanisa Katoliki—walipokuwa na nia ya kukubali uhakika wa kwamba dunia haikuwa kitovu cha ulimwengu wote mzima bali ilizunguka jua, kitovu cha mfumo wa jua. Kushindwa kwa nadharia hizo nyingi kufafanua mambo ya hakika kulisukuma watu mmoja mmoja wenye akili zilizo wazi, wasijaribu kutokeza nadharia mpya, bali kuchunguza tena msingi wa machunguzo yao. Na hilo likaongoza kwenye kufanikiwa.20. (a) Ni nini uliokuwa msingi wa dhana yenye makosa ya uchunguzi wa “kisayansi” juu ya asili ya dini? (b) Voltaire alirejeza kwenye uhitaji gani wa msingi?Kanuni iyo hiyo yaweza kutumiwa kuhusu uchunguzi wa asili ya dini. Kwa sababu ya ongezeko la uatheisti (kutodai kuwa na dini yoyote) na kuenea kwa ukubali wa nadharia ya mageuzi, watu wengi wamesadiki ki-vivi hivi tu kwamba Mungu hayupo. Kwa kutegemea udhanifu huo, wanahisi kwamba ufafanuzi wa kuwapo kwa dini wapaswa upatikane tu kwa binadamu mwenyewe—katika hatua zake za kufikiri, mahitaji yake, hofu zake, “mahamaniko” yake. Voltaire alitoa taarifa hii, “Kama Mungu hayupo, ingekuwa lazima kumbuni yeye”; kwa hiyo wao hutoa hoja kwamba binadamu amebuni Mungu.—Ona kisanduku, ukurasa 28.21. Twaweza kufikia mkataa gani wa kufikiri kuzuri kutokana na kushindwa kwa nadharia hizo nyingi juu ya asili ya dini?Kwa kuwa nadharia hizo nyingi zimeshindwa kutoa jibu lenye kuridhisha kikweli, je! sasa huu sio wakati wa kuchunguza tena dhana ambayo juu yayo machunguzo haya yametegemezwa? Badala ya kumenyeka bila ya matokeo katika kawaida ile ile, je! lisingekuwa jambo la akili kutafuta jibu kwingine? Ikiwa tuna nia ya kuwa na akili iliyo wazi, tutakubali kwamba kufanya hivyo ni jambo la akili na la kisayansi. Na hasa tuna kielelezo kimoja cha kutuonyesha tuone fikira nzuri ya kuchukua mwendo huo.Ulizio la Kale22. Nadharia nyingi za Waathene juu ya vijimungu vyao ziliathirije njia yao ya kuabudu?Katika karne ya kwanza ya Wakati wa Kawaida wetu, Athene, Ugiriki, lilikuwa kitovu maarufu cha usomi. Hata hivyo, kati ya Waathene kulikuwako vikundi vingi vyenye mawazo tofauti, kama vile Waepikureo na Wastoiki, kila kimoja kikiwa na wazo lacho chenyewe juu ya vijimungu. Kwa kutegemea mawazo hayo mbalimbali, viabudiwa vingi viliheshimiwa sana, na njia tofauti za ibada zikasitawi. Matokeo ni kwamba, jiji hilo lilijaa sanamu na mahekalu yaliyofanyizwa na watu.—Matendo 17:16.23. Mtume Paulo aliwatolea Waathene maoni gani yaliyo tofauti kabisa juu ya Mungu?Wapata mwaka 50 W.K., mtume Mkristo Paulo alizuru Athene na kuwatolea Waathene maoni tofauti kabisa. Yeye aliwaambia: “Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono; wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.”—Matendo 17:24, 25.24. Hasa Paulo alikuwa akiwaambia nini Waathene juu ya ibada ya kweli?Kwa maneno mengine, Paulo alikuwa akiwaambia Waathene kwamba Mungu wa kweli, “aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo,” si ubuni wa kuwaza kwa mtu, wala yeye hatumikiwi kwa njia ambazo mtu huenda akatunga. Dini ya kweli si jitihada ya upande mmoja ya mtu kujaribu kujazia uhitaji fulani wa kisaikolojia au kutuliza hofu fulani. Tofauti na hilo, kwa kuwa Mungu wa kweli ndiye Muumba, ambaye alimpa mtu uwezo wa kufikiri na nguvu za kusababu, ni jambo la akili kwamba Yeye angempa mtu njia ya kuja katika uhusiano wenye kuridhisha pamoja Naye. Hilo, kulingana na Paulo, ndilo Mungu alifanya hasa. “Alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika [mtu] mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, . . . ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.”—Matendo 17:26, 27.25. Fafanua jambo kuu la hoja ya Paulo juu ya asili ya ainabinadamu?Angalia hoja kuu ya Paulo: Mungu “alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika [mtu] mmoja.” Hata ingawa leo kuna mataifa mengi ya watu, wanaoishi duniani pote, wanasayansi wanajua kwamba, kwa hakika, ainabinadamu yote ni ya asili ile ile. Fikira hiyo ni yenye umaana mkubwa kwa sababu tunaposema juu ya ainabinadamu yote kuwa ya asili ile ile, inamaanisha mengi zaidi ya wao kuwa na uhusiano wa kiuzaliwa na kiurithi tu. Wana uhusiano katika maeneo mengine pia.26. Ni nini kinachojulikana juu ya lugha kinachounga mkono hoja kuu ya Paulo?Kwa mfano, angalia yanayosemwa na kitabu Story of the World’s Worship juu ya lugha ya binadamu. “Wale ambao wamefanya uchunguzi wa lugha za ulimwengu na kuzilinganisha wana jambo la kusema, nalo ndilo hili: Lugha zote zaweza kuwekwa katika vikundi vya familia za usemi, na familia hizi zote zaonwa kuwa zilianza kutokana na chanzo kile kile.” Kwa maneno mengine, lugha za ulimwengu hazikuanza zikiwa tofauti-tofauti na kwa kujitegemea, kama ambavyo wanamageuzi wangetuaminisha. Wao hutoa nadharia ya kwamba watu wenye kuishi ndani ya mapango katika Afrika, Ulaya, na Asia walianza kwa mikoromo na miguno na hatimaye wakasitawisha lugha zao wenyewe. Sivyo ilivyokuwa. Uthibitisho ni kwamba “zilianza kutokana na chanzo kimoja.”27. Kwa nini ni kufikiri kuzuri kwamba mawazo ya mtu juu ya Mungu na dini yalianza kutokana na chanzo kimoja?Ikiwa ndivyo ilivyo kwa kitu cha kibinafsi na cha kutokeza sana kama ilivyo lugha ya kibinadamu, basi je! lisingekuwa jambo la akili kufikiri kwamba mawazo ya mtu juu ya Mungu na dini yapasa pia kuwa yalianza kutokana na chanzo kimoja? Na ilivyo, dini inahusiana na kufikiri, na kufikiri kunahusiana na uwezo wa mtu kutumia lugha. Si kwamba dini zote kwa kweli zilikua kutokana na dini moja, bali mawazo na mafikira yapasa kufuatiwa mpaka kwenye asili ile ile au dimbwi moja la mawazo ya kidini. Je! kuna uthibitisho wa kuunga mkono hilo? Na ikiwa, kwa kweli, dini za watu zilitokana na chanzo kimoja, ni nini hicho? Twaweza kujuaje?Tofauti Lakini Zafanana28. Twaweza kujuaje kama kuna asili moja ya dini za ulimwengu?Twaweza kupata jibu katika njia ile ile ambayo wataalamu wa lugha walipata majibu yao juu ya asili ya lugha. Kwa kuzilinganisha lugha na kuona ufanani wazo, mtaalamu wa etimolojia (elimu ya kuchunguza asili ya maneno) aweza kufuatisha lugha mbalimbali kurudi mpaka kwenye chanzo chazo. Hali moja na hiyo, kwa kulinganisha dini, twaweza kuchunguza mafundisho yazo, hekaya, sherehe za ibada, sherehe za heshima, desturi, na kadhalika, na kuona kama kuna uzi wowote wa msingi wenye utambulishi mmoja na, ikiwa ndivyo, uzi huo unatuongoza kwenye nini.29. Ni nini inayoweza kuwa sababu ya tofauti nyingi kati ya dini?Kijuu-juu, dini nyingi zilizopo leo zaonekana kuwa zenye kutofautiana sana. Hata hivyo, tukizivua mambo ambayo ni madoido tu na ambayo ni nyongeza ya baadaye, au tukiondoa zile tofauti ambazo ni tokeo la hali za hewa, lugha, hali za kipekee-pekee za nchi yao ya kuzaliwa, na mambo mengine, inastaajabisha jinsi nyingi za dini hizo zinavyoonekana zinafanana.30. Wewe waona ufanani gani kati ya Ukatoliki wa Roma na Dini ya Buddha?Kwa kielelezo, watu walio wengi wangefikiri kwamba hakungeweza kuwako dini nyingine mbili zozote zinazotofautiana zaidi ya Kanisa Katoliki la Roma la nchi za Magharibi na Dini ya Buddha ya nchi za Mashariki.
 
Tutazungumza kwa urefu zaidi jinsi dini fulani fulani zilivyoanza na kusitawi. Utakuta inanurisha si kujua tu jinsi kila dini ilivyo tofauti na nyinginezo bali pia jinsi inavyofanana nazo. Pia utaweza kujua jinsi kila dini inavyoingia katika mpangilio wa wakati wa historia ya kibinadamu na historia ya dini, jinsi kitabu au maandishi yayo matakatifu yanavyohusiana na mengine, jinsi mwanzilishi au kiongozi wayo alivyovutwa na mawazo mengine ya kidini, na jinsi imekuwa na uvutano juu ya mwenendo na historia ya ainabinadamu. Ukizingatia mambo haya akilini, kujifunza juu ya jitihada ya ainabinadamu ya kutafuta Mungu ambayo imechukua muda mrefu Mungu kutakusaidia uone kwa uwazi zaidi ukweli juu ya dini na mafundisho ya kidini.



USIKOSE KUSOMA SURA YA TATU........................................................................................
 
bila summary hapa, utapoteza wasomaji naona unataka utushushie kitabu kizima 😅
Naupokea ushauri bwana Surya.Kama nikiandika kwa ufupi nitapendelea baadhi ya dini maana zina story fupi sana.Acha nishushe nondo zote hadi pale zitakapo tosha maana siandiki kwa ajiri ya kushinda.Hii story challenge.
 
Bro, weka hata Paragraph, utatusaidia wengi
Pia unapo bold habari nzima ambayo haina hata Paragraph ndio unatuchanganya kabisa

Mada ni nzuri Mno.

Japo bado sijajua mtazamo wako kuhusu Dini, ila nimeelewa bandiko lako kwa kiasi Fulani

Post namba 1, umeeleza kivipi chagua la mtu kuhusu ipi ni dini sahihi linategemea kwa kiasi kikubwa Wapi amezaliwa

Observation ambayo ni sahihi kwa 99%

Na kivipi, ukweli kuhusu dini yako, utegemee wapi ulipo?

Kwanini watu wasichague dini kulingana na akili zao, na sio kuchaguliwa na mazingira
 
Sura 3

Nyuzi Zile Zile Katika Ngano



KWA nini tuchunguze ngano?

Je! hizo si ubuni wa wakati mrefu uliopita tu? Ingawa ni kweli kwamba nyingi zazo hutegemea ubuni, nyingine zategemea jambo la hakika. Kielelezo ni ngano na hekaya zinazopatikana ulimwenguni pote ambazo hutegemea uhakika wa Gharika ya ulimwengu, au Furiko, ambalo Biblia husimulia.

Sababu moja ya kuchunguza ngano ni kwamba ndizo msingi wa imani na desturi ambazo zingali zapatikana katika dini leo. Kwa kielelezo, imani katika nafsi isiyoweza kufa yaweza kufuatishwa mpaka kwenye ngano za Waashuri-Wababuloni wa kale kupitia ngano za Kimisri, Kigiriki, na Kiroma mpaka kwenye Jumuiya ya Wakristo, ambako zimekuwa itikadi iliyo na msingi katika theolojia yake.


Ngano ni uthibitisho wa kwamba mtu wa kale alifanya jitihada ya kutafuta vijimungu, na pia maana ya uzima. Katika sura hii tutazungumza kifupi baadhi ya habari za kawaida zinazotokana na ngano za tamaduni kubwa-kubwa za ulimwengu. Tupitiapo ngano hizo, tutaona jinsi uumbaji, Furiko, vijimungu vya bandia na vijimungu-nusu, nafsi isiyoweza kufa, na ibada ya jua zinavyojitokeza kwa ukawaida kuwa nyuzi zile zile katika visehemu-sehemu vya ngano. Lakini kwa nini iwe hivyo?Pindi nyingi sana kuna kiini cha uhakika wa kihistoria, mtu fulani, au tukio fulani ambalo baadaye limetiwa chumvi au likapotolewa ili kufanya iwe ngano hiyo. Moja la mambo hakika hayo ya kihistoria ni maandishi ya Biblia ya uumbaji.
 
Uhakika na Hadithi ya Kubuni Juu ya Uumbaji


Ni zipi zilizokuwa baadhi ya itikadi za ngano za Kigiriki?

Ngano juu ya uumbaji ni tele, lakini hakuna yoyote inayoeleza kwa njia rahisi ya kiakili kama maandishi ya Biblia juu ya uumbaji. (Mwanzo, sura 1, 2) Kwa kielelezo, simulizi litolewalo katika ngano za Kigiriki lasikika kuwa la kishenzi. Mgiriki wa kwanza kuandika ngano katika njia ya utaratibu alikuwa Hesiod, aliyeandika Theogony chake katika karne ya nane K.W.K. Yeye afafanua jinsi vijimungu na ulimwengu vilivyoanza. Aanza na Gaea, au Gaia (Dunia), anayemzaa Zohari (Mbingu).

Mambo yanayofuatwa yamefafanuliwa na msomi Jasper Griffin katika The Oxford History of the Classical World:“Hesiod asimulia hadithi, inayojulikana na Homer, juu ya mfuatano wa vijimungu vya anga. Kwanza Zohari ndiye mkuu zaidi, lakini alikandamiza watoto wake, na Gaia alimtia moyo mwana wake Kronosi amhasi. Kronosi naye akawala watoto wake mwenyewe, mpaka Rhea mke wake akampa jiwe ale badala ya Zeu; mtoto Zeu alilelewa Krete, akamlazimisha baba yake atapike ndugu zake, akiwa pamoja nao na msaada mwingine wakamshinda Kronosi na Matitani wake na kuwatupa chini ndani ya Tartaro.”



Kulingana na Jasper Griffin, ni nini kinachoelekea kuwa ndicho chanzo cha ngano nyingi za Kigiriki?Wagiriki walipata kutoka chanzo gani ngano hizi za kiajabu?

Mtungaji uyo huyo ajibu: “Asili yazo ya kwanza yaelekea kuwa ilikuwa ya Kisumeri. Katika hadithi hizi za mashariki twaona mfufulizo wa vijimungu, na taswira za kuhasiwa, za kumeza, na za jiwe moja likirudi katika njia ambazo, ijapokuwa zenye kutofautiana, zaonyesha kwamba ufanani na Hesiod si sadifu tu.” Tunalazimika kuangalia Mesopotamia na Babuloni za kale kuwa ndizo chanzo cha ngano nyingi zilizoenea katika tamaduni nyinginezo.

{a} Kwa nini si rahisi kupata habari juu ya ngano za kale za Uchina?

(b) Ngano moja ya Kichina yafafanuaje uumbaji wa dunia na binadamu? (Linganisha Mwanzo 1:27; 2:7.)

Ngano za kale za dini ya wenyeji Wachina si rahisi nyakati zote kufafanua, kwani maandishi mengi ya kale yaliharibiwa katika kipindi cha 213-191 K.W.K.

Hata hivyo, ngano fulani zimesalia, kama ile inayosimulia jinsi dunia ilivyofanyizwa. Profesa mmoja wa sanaa ya Mashariki, Anthony Christie, aandika hivi: “Twajifunza Kaosi alikuwa kama yai la kuku. Wala Mbingu wala Dunia havikuwapo. Kutoka kwa yai P’an-ku akazaliwa, kutoka kwa elementi zalo nzito Dunia ikafanyizwa na Anga kutoka kwa elementi nyepesi. P’an-ku huwakilishwa na mbilikimo, aliyevaa ngozi ya dubu au shela ya majani. Kwa miaka 18,000 umbali kati ya Dunia na Anga uliongezeka kila siku kwa futi
10, na P’an-ku akakua kwa kimo icho hicho hivi kwamba mwili wake ukajaza pengo hilo. Alipokufa, sehemu tofauti-tofauti za mwili wake zikawa elementi mbalimbali za asili. . . . Viroboto vya mwili wake vikawa ndiyo jamii ya kibinadamu.”

Kulingana na ngano za Wainka, lugha zilitokeaje?

Kutoka Amerika ya Kusini hekaya ya Inka yafafanua jinsi muumba anayesimuliwa katika ngano alivyolipa kila taifa usemi. “Yeye alilipa kila taifa lugha ambayo lingeisema . . . Yeye alimpa kila mmoja mwili na pia wanaume na wanawake hali ya kuwapo na nafsi, akaliamuru kila taifa lizame chini ya dunia. Basi kila taifa likapita chini ya ardhi na likatokea katika sehemu ambazo yeye aliligawia.” (The Fables and Rites of the Yncas, cha Cristóbal de Molina wa Cuzco, kilichonukuliwa katika South American Mythology) Katika kisa hiki yaonekana kwamba simulizi la Biblia la kuvurugwa kwa lugha kule Babeli ndilo kiini cha uhakika wa ngano hii ya Inka. (Mwanzo 11:1-9) Lakini sasa acheni tugeuze uangalifu kwenye Gharika inayosimuliwa katika Biblia kwenye Mwanzo 7:17-24.
 
Furiko—Jambo la Hakika au Ngano?.

(a) Biblia yatuambia nini juu ya hali duniani kabla ya Furiko?
(b) Nuhu na familia yake walipaswa kufanya nini ili waokolewe kutoka Furiko hilo?

Ikiturudisha nyuma miaka ipatayo 4,500 iliyopita, karibu na 2,500 K.W.K., Biblia hutuambia kwamba wana wa roho wa Mungu walioasi walitwaa miili ya kibinadamu “wakajitwalia wake wo wote waliojichagulia.” Uzazi-mchanganyiko huu usio wa asili ulitokeza Wanefili wenye kufanya jeuri, “waliokuwa watu hodari wa zamani.” Mwenendo wao wa kuhalifu sheria uliathiri ulimwengu wa kabla ya Furiko kufikia hatua ya kwamba Yehova akasema: “Nitamfutilia mbali binadamu niliyemwumba usoni pa nchi . . . kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA .”

Halafu simulizi hilo laendelea kusema juu ya hatua kamili na zenye vitendo ambazo Nuhu alipaswa kuchukua ili ajiokoe mwenyewe na Furiko hilo, na pia familia yake na aina mbalimbali za wanyama.—Mwanzo 6:1-8, 13–8:22; 1 Petro 3:19, 20; 2 Petro 2:4; Yuda 6.10.

Kwa nini simulizi la Biblia juu ya Furiko halipasi kuonwa kuwa ngano?Wahakiki wa ki-siku-hizi husema maandishi ya matukio ya kabla ya Gharika yanayosimuliwa katika Mwanzo ni ngano. Hata hivyo, historia ya Nuhu ilipokewa na kuaminiwa na wanaume waaminifu, kama vile Isaya, Ezekieli, Yesu Kristo, na mitume Petro na Paulo.

Pia inaungwa mkono na uhakika wa kwamba inawakilishwa katika ngano nyingi mno ulimwenguni pote, kutia Utenzi wa Gilgameshi wa kale na pia ngano za China na za Waazteki, Wainka, na Wamaya.

Tukiwa tunazingatia akilini maandishi ya Biblia, acheni sasa tufikirie ngano za Waashuri-Wababuloni na marejezo yazo kwenye furiko fulani.—Isaya 54:9; Ezekieli 14:20; Mathayo 24:37; Waebrania 11:7.
 
Furiko na Gilgameshi Binadamu-Kijimungu {nusu mtu nusu mungu}.


Maarifa yetu juu ya Utenzi wa Gilgameshi yategemea nini?

Tukirudi nyuma katika historia miaka zaidi ya 3,000, twakuta ngano ya Kiakadia iliyo maarufu sana iitwayo Utenzi wa Gilgameshi. Maarifa yetu juu ya hilo yategemea hasa maandishi-awali ya maandishi-kabari yaliyotoka kwenye maktaba ya Ashurbanipali, aliyetawala katika Ninawi la kale.

Gilgameshi alikuwa nani, na kwa nini yeye hakupendwa na wengi? (Linganisha Mwanzo 6:1, 2.)

Hiyo ni hadithi ya matendo hodari ya Gilgameshi, anayesimuliwa kuwa theluthi mbili kijimungu na theluthi moja binadamu, binadamu-kijimungu. Aina moja ya utenzi huo yaeleza hivi: “Katika Uruki alijenga kuta, boma kubwa, na hekalu la mbarikiwa Eanna kwa ajili ya kijimungu Anu cha anga, na kwa ajili ya Ishtari kijimungu-kike cha upendo . . . , bibi yetu wa upendo na vita.” (Ona kisanduku, Nitakiweka kwenye sura za mbele kwa ajili ya orodhesho la vijimungu na vijimungu-vike vya Waashuri-Wababuloni.)

Hata hivyo, Gilgameshi hakuwa hasa kiumbe mzuri kukaribiwa. Wakaaji wa Uruki walilalamikia vijimungu hivi: “Ashiki yake haiachii bikira mpenzi wake, wala binti ya shujaa wala mke wa sharifu.”

(a) Vijimungu vilichukua hatua gani, na Gilgameshi alifanya nini? (b) Utnapishtimu alikuwa nani?

Vijimungu hivyo vilichukua hatua gani kwa kuitikia uteti wa watu? Kijimungu-kike Aruru kiliumba Enkidu awe mshindani binadamu wa Gilgameshi. Hata hivyo, badala ya kuwa maadui, wakawa marafiki wa karibu. Utenzi huo ulipoendelea, Enkidu akafa. Kwa majonzi mengi, Gilgameshi alilia hivi: “Nifapo, je! sitakuwa kama Enkidu? Ole umeingia tumboni mwangu. Kwa kuhofu kifo, natanga-tanga uwandani.” Yeye alitaka siri ya kutokufa basi akafunga safari akamtafute Utnapishtimu, mwokokaji wa gharika aliyekuwa amekabidhiwa na vijimungu hali ya kutoweza kufa.

(a) Utnapishtimu aliambiwa afanye nini? (Linganisha Mwanzo 6:13-16.) (b) Safari ya Gilgameshi inayotajwa na utenzi ikawaje?

Hatimaye Gilgameshi ampata Utnapishtimu, ambaye amsimulia hadithi ya furiko. Kama inavyoonekana katika bamba la Utenzi wa 11, liitwalo Bamba la Furiko, Utnapishtimu amsimulia maagizo aliyopewa kuhusu furiko: “Bomoa nyumba (hii), jenga merikebu! Acha mali, tafuta uhai. . . . Ndani ya merikebu ingiza mbegu yako ya vitu vyote vilivyo hai.” Je! hili halisikiki kidogo kufanana na mrejezo wa Biblia kuhusu Nuhu na Furiko? Lakini Utnapishtimu hawezi kumtuza Gilgameshi hali ya kutoweza kufa. Gilgameshi, akiwa amekata tamaa, arudi nyumbani Uruki. Simulizi lamalizika kwa kifo chake. Jumla ya ujumbe wa utenzi huo ni huzuni na fadhaa ya kifo na maisha ya baadaye. Watu hao wa kale hawakumpata Mungu wa ukweli na tumaini. Hata hivyo, kiunganishi cha utenzi huo na simulizi rahisi la Biblia la muhula kabla ya Furiko ni wazi kabisa. Sasa na tugeukie simulizi la Furiko kama linavyoelezwa na hekaya nyingine.
 
Hekaya ya Furiko katika Tamaduni Nyingine


Kwa nini tupendezwe na hekaya ya Kisumeri juu ya furiko?Hata mapema zaidi ya Utenzi wa Kale wa Gilgameshi ni ngano ya Kisumeri inayotaja “Ziusudra, kifani cha Nuhu wa kibiblia, ambaye anaelezwa kuwa mfalme mwogopa-mungu, mwenye kuhofu kijimungu, daima akitafuta-tafuta ufunuo wa kimungu katika ndoto au tabano.” (Ancient Near Eastern Texts Relating to the Old Testament)

Kulingana na chanzo icho hicho, ngano hii “yatoa ulinganifu wa karibu zaidi na wenye kutokeza zaidi kwa habari ya kibiblia isiyopata kuchimbuliwa bado katika fasihi ya Kisumeri.” Staarabu za Wababuloni na Waashuri, zilizofuata baadaye, ziliathiriwa na ule wa Kisumeri.

Hekaya za Kichina juu ya furiko zingaliweza kuwa zilitokana na chanzo gani?Kitabu China—A History in Art chatuambia kwamba mmoja wa watawala wa kale wa China alikuwa Yü, “mshinda Furiko Kubwa. Yü alielekeza maji ya furiko kwa njia ya mfereji kwenye mito na bahari ili awape makao tena watu wake.”

Mtaalamu wa ngano Joseph Campbell aliandika juu ya “Kipindi cha Wakubwa Kumi” cha Uchina, akisema: “Kwa enzi hii ya maana, inayofikia ukomo katika Gharika, maliki kumi walipewa mgawo katika ngano za mapema za wakati wa Chou.

Kwa sababu hiyo, inaonekana kwamba huenda tunachotazama hapa ni badiliko la kimahali la mfululizo wa orodha ya kale ya mfalme wa Sumeri.” Halafu Campbell alitaja visehemu fulani kutoka hekaya hizi za Kichina zilizoelekea “kukazia ile hoja kwa ajili ya chanzo kuwa cha Kimesopotamia.” Hiyo inaturudisha nyuma kwenye chanzo kile kile kilicho kiini cha ngano nyingi. Hata hivyo, hadithi za Furiko zaonekana pia katika mabara ya Amerika, kwa kielelezi, katika Meksiko wakati wa kipindi cha Waazteki katika karne za na 16 W.K.

Waazteki walikuwa na hekaya gani?

Ngano za Kiazteki zilisema juu ya enzi nne zilizotangulia, wakati wa ile ya kwanza dunia ilikaliwa na majitu. (Hicho ni kikumbusho kingine juu ya Wanefili, majitu wanaorejezewa kwenye Biblia katika Mwanzo 6:4.)

Zilitia ndani hekaya ya zamani za kabla ya furiko ambayo katika hiyo “maji yaliyo juu yaungana na yale yaliyo chini, yakifuta kabisa peo za macho na kufanya kila kitu kuwa bahari isiyo na mwisho ya ulimwengu mzima.” Kijimungu chenye kuongoza mvua na maji kilikuwa Tlaloki. Hata hivyo, mvua yacho haikupatikana kwa bei nafuu bali ilitolewa “kwa kubadilishana na damu ya wahanga waliotolewa dhabihu ambao machozi yao yenye kutiririka yangekuwa kama mvua na kwa hiyo kuchochea mtiririko wa mvua.” (Mythology—An Illustrated Encyclopedia) Hekaya nyingine yaeleza kwamba muhula wa nne ulitawalwa na Chalchiuhtlicue, kijimungu-kike cha maji, ambacho ulimwengu wacho uliangamia katika furiko. Watu waliokolewa kwa kuwa samaki!

Ni masimulizi gani yametapakaa katika ngano za Amerika Kusini? (Linganisha Mwanzo 6:7, 8; 2 Petro 2:5.)

Hali moja na hiyo, Wainka walikuwa na hekaya zao juu ya Furiko. Mwandikaji Mwingereza Harold Osborne aeleza hivi: “Labda sehemu katika ngano za Amerika ya Kusini zilizoenea zaidi kotekote ni zile hadithi za gharika . . . Ngano za gharika zimeenea sana kati ya vikundi vya watu wa nyanda za juu na makabila ya nyanda za chini. Gharika kwa ujumla hukamatanishwa na uumbaji na Epifani [udhihirisho] ya kijimungu-muumba. . . Nyakati nyingine huonwa kuwa adhabu ya kimungu ikifutilia mbali aina ya kibinadamu katika kufanya tayarisho la kutokeza jamii mpya.”

Elezo juu ya hekaya ya Maya inayohusu furiko.Vivyo hivyo, Wamaya katika Meksiko na Amerika ya Kati walikuwa na hekaya yao juu ya Furiko iliyohusisha gharika ya ulimwengu wote, au haiyococab, maana yake “maji juu ya uso wa dunia.” Askofu Mkatoliki Las Casas aliandika kwamba Wahindi Waguatemala waliiita Butic, ambalo ndilo neno linalomaanisha furiko la maji mengi na humaanisha hukumu ya mwisho, na kwa hiyo wao waamini kwamba Butic nyingine iko karibu, ambayo ni furiko na hukumu nyingine, si la maji, bali la moto.” Hekaya nyingine nyingi kuhusu furiko zipo ulimwenguni pote, lakini zile chache zilizokwisha kunukuliwa zathibitisha kiini cha hekaya hiyo, lile tukio la kihistoria linalosimuliwa katika kitabu cha Mwanzo.
 
Back
Top Bottom