Kikundi cha kilimo

nitaluv

Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
27
Reaction score
19
Habari wapendwa....

Mimi nipo morogoro, ni Dada mwenye uchungu sana na maisha na nahitaji maendeleo kwa njia yoyote iliyo halali! na moja ya njia hizo ni kilimo! nimeshawahi kujishughulisha Sana na kilimo cha umwagiliaji kwa zao la nyanya, hoho na matikiti... kwakweli ingawa haikunilipa Sana lakin niliweza kurudisha gharama za uzalishaji na kupata faida kidogo!

ila kwa mwaka 2014 wote sikuweza kurudi shambani kutokana na matatizo ya kifamilia yaliyonifanya kutumia mtaji wote!sasa nahitaji kurudi shamban mwaka huu lakin nimeona changamoto kubwa kwenye kilimo ni ufuatiliaji!

Mimi kwa nature ya kazi yangu ni mtu Wa kusafiri safiri! hivyo nimefikiria nikipata watu amabo wako interested na kilimo Kama Mimi tuanzishe kikundi cha kilimo nadhani itakuwa poa Sana na pia tunaweza kufaidika na opportunity zilizopo kwenye halmashauri Kama hela za vijana wenye miradi mbalimbali hasa hii miradi ya kilimo!

Kama upo morogoro na kweli hili wazo limekugusa tiririka hapa chini tuone tunaanzia wapi..... wazo langu ni kuja kuwa na kampuni inayozalisha, inayouza na kununua mazao... please naomba wenye nia ya kweli waje hapa tukamate hii fursa!.. kikundi kiwe na watu 3 hadi Wa 5 ili tuweze kumanage vizuri..

wote tunajua panya wengi hawachimbi shimo!

Asanten.
 
Kilimo kinacholengwa hapa ni kipi? Mtaji kiasi gani? Preferred Location ni wapi?

Naomba majibu please wakati ukinifikiria tuwe pamoja!!
 
Kuna wakati fulani nilikwenda mtumbani kuchagua viatu, nilipata kiatu kizuri sana na nikajaribu kikanitosha vizuri (habari njema) nikauliza bei, nikatajiwa ile ninayoimudu (habari njema sana hii) nilipomwambia muuzaji anitafutie chenzie alikipata (oh! Maisha burudaaani kabisa).

Lakini nikagundua vyote ni vya mguu wa kushoto na mimi nina mguu mmoja tu wa kushoto, mwingine ni wa kulia (habari mbaya katikati ya habari njema).

Namaanisha: mimi nimelipenda sana wazo lako na ningependa kua miongoni mwa hao wabia tufanye uwekezaji katika kilimo (na tungefanya na ufugaji maana nina kautaalam kiasi) lakini lakini lakini, "habari mbaya katikati ya habari njema" ni kwamba niko mbali mno toka morogoro na kwa namna yoyote kwa sasa siwezi kuwapo huko.

Nikupongeze tu na kukutia moyo, naamini utawapata wadau na mkitia nia na juhudi mtafanikiwa. Always mimi ni mwenzenu.

Ahsante.

(wacha nipeleke yeboyebo zangu kwa fundi akashone, nitarejea)
 
Dah...how I wish ungekuwa uko Moro!anyways..tutakutumia hata kwa maon na ushauri!Kama nlivyosema hapo juu lengo ni kuja kuwa na kampun inayozalisha, kuuza na kununua mazao...

ila pia ufugaji uko humo ndani yake!napenda pia ufugaji hasa wa kuku Wa kienyeji na ng'ombe Wa maziwa!nitakutumia kwenye ufugaji kaka...na Jana nimepata info nzuri Sana toka kwa "gazeti" through thread yake ya ufugaji Wa kuku Wa kienyeji!thanks
 
Kilimo kinacholengwa hapa ni kipi?
Mtaji kiasi gani?
Preferred Location ni wapi?
Naomba majibu please wakati ukinifikiria tuwe pamoja!!

My dia ni kilimo cha matunda (kama matikiti,nanasi.pasion nk)na mboga mboga... (Kama nyanya,hoho,vitunguu,pilipili )…. operation cost Mimi wakati nalima nlitumia Kama m2 manake nlikuwa natumia drip system!so gharama za mafuta zilikuwa kubwa!ila sahiv nimeshajifunza na nimeona furrow ni nzuri zaid na haina gharama Sana! so operation cost itapungua Sana..

ukiwa na m1 unalima kwa furrow eka moja!hapo nimeweka gharama za mbegu,mbolea,madawa.... ila Kutakuwa na kulipa vibarua na kukodisha shamba!(nikifika kwa job nitakaa niainishe hizi gharama vizuri then ntakuja na taarifa iloyokamilika)... preferred location ni maeneo ya kasanga,mlali na kilosa pia ni pazuri ila ni mbali na Moro mjin so usimamiaji utasumbua! asante kwa kuonyesha nia!
 

usijali
 
Nimeipenda hii kitu, nasubiri mchamganuo.
 
Kitu kizuri hiki..ila lazma kuwe na limit ya watu ambao wana wajibika.

Ila naona mazao ya biashara kama alizet na ufuta vinalipa sana
 
Kitu kizuri hiki..ila lazma kuwe na limit ya watu ambao wana wajibika.

Ila naona mazao ya biashara kama alizet na ufuta vinalipa sana

Yap alizet na ufuta ni mazao mengine poa Sana kwa biashara!ila mi sina utaalamu nayo Sana....Nina uzoefu na mazao ya bustani(matunda na mbogamboga)...so maybe members watakaopatikana tukiungana tunaeza kuja na mawazo mazuri jinsi ya kudeal na mazao ya aina zote hizi!na kuhusu limit number of people ni jambo muhimu Sana ndo maana niatangulia kusema 5 people will be enough!....na kwa mnaosubiri mchanganuo Wa gharama msijali nalifanyia kazi..nitalileta kwenu kabla ya siku kuisha!
 
Binafsi nimelipenda wazo ila sasa naomba mtoa mada uwe wazi ili nione kama naweza kujiunga na kikundi hicho cha kilimo. Tatizo sio umbali; naamini wanakikundi wanaweza kuwa mbali lakini wakawawezesha wakaaji wa hapo Moro wazo likafanyiwa kazi na wanakikundi wakapewa mgao wao kama kawaida. Toa contact zako tuongee zaidi
 

Nimekuelewa mkuu...na mwanzon hata Mimi nlifikiria inawezekana kufanya jambo hili kwa kutumia hela yako tu...ila kumbuka Kama lengo ni kuwa Kama kikundi then lazima tufate zile nguzo tano za kikundi mojawapo ni uwepo Wa vikao at least once in a month Kama kikundi kikiwa bado kichanga na baadae hata ikiwa Mara moja kwa miez mitatu ni poa...

ila mwanzon kukutana Mara kwa Mara ili kuimarisha kikundi kutahitajika na nahofia umbali Wa wanachama unaeza ukazuia hili!naongea kwa kutumia uzoefu kaka as nlishahamasisha watu tukaunga kikundi cha namna hii kwa watsapp but hakikufika mbali na ikanibid kuwarudishia watu pesa zao!..my number 0713002081...kwa aliye serious na swala hili!
 
Binafsi niko serious ila kwa kuwa sijapewa uwazi kuhusu linalotarajiwa kufanyika ndo maana nasema nitakupigia tuongee zaidi
 
nitaluv

Niko serious, naomba kazi ya kusimamia shamba lenu po pote pale mtakapopata ndani ya Tz.
 
Last edited by a moderator:
Okey guys nimejitahid Kuchanganua gharama za hiki kilimo na haya ndo majibu nlokuja nayo..

1- kukodi shamba ni 250,000/= kwa mwaka!(shamba lililo karibu na chanzo cha maji kisichokauka kwa mwaka mzima)

2- kuandaa shamba
*kulima kwa tractor 50,000/=
*kupiga halo 50,000/=
*kuinulia matuta (matuta 35*tsh 4000 each) =14000

3-kuandaa kitalu 100,00/=

4- Mbegu kwa ekali moja
*tikitimaji pact 3@55,000=165,000/=
*nyanya pact 2@180,000=360,000/=
*vitunguu kg1.5 =468,000/=
*viaz mbatata gunia 5@50,000= 500,000/=
*cabbage pacts 2@68,000= 136,000/=
*nanasi miche 18000 = 2700,000/=
*pilipili mbuzi miche 5200 = 25,000/=
*matango =17,000/=

5- Mbolea (gharama ni makadilio). = 500,000/=

6- Madawa (gharama ni makadilio) = 250,000/=

7- mafuta( umwagiliaji) Lita 2 kwa siku 90= 450,000/=

8-miti na kamba (kwa nyanya na hoho)= 250,000/=

9- vibarua wawil ( 60,000*2=120,000) kwa miez 4=480,000/=

10- kununua water pump (ya 3'). = 280,000/= hadi 300,000/=

Kama kuna nlichokisahau then ntakijibu kupitia maswali yenu!thanks....
 
Binafsi niko serious ila kwa kuwa sijapewa uwazi kuhusu linalotarajiwa kufanyika ndo maana nasema nitakupigia tuongee zaidi

Poa kaka tutaongea vizuri badae kwa cm!ngoja tufanye majukumu ya watu kwanza mida hii!
 
Mm ni mtaalam wa kilimo cha hayo mazao yaan nahitimi dip ya horticulture mwez wa nne mwaka huu,ningekua karibu niko Morogoro ningeshirikiana bahati mbaya niko Arusha dah
 
Mm ni mtaalam wa kilimo cha hayo mazao yaan nahitimi dip ya horticulture mwez wa nne mwaka huu,ningekua karibu niko Morogoro ningeshirikiana bahati mbaya niko Arusha dah

Dah tena ingekuwa poa Sana ungekuwa ni mmoja Wa wanachama..tungekuwa na uhakika Wa technical assistance bureeee kabisa!too bad...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…