Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,821
- 6,122
RIWAYA ; KIKOSI CHA PILI.
Season 2.
Na; BAHATI MWAMBA.
SIMU;0758573660.
Soma hivi……..
GATUMBA BURUNDI.
Kiasi cha kilomita kumi na tano kutoka Bunjumbura na, kilomita tano kutoka mashariki ya Congo, kulikuwa na kundi la watu wanne wakijongea kwenye makazi ya watu yaliokuwa kati ya mpaka wa Burundi na Congo. Watu wale walikuwa wamevalia kijeshi, walivaa kofia ngumu zilizokuwa na kurunzi kwa mbele, walivaa buti ngumu na mikononi walishika silaha mpya na za kisasa kutoka Canada.
Viunoni mwao walikuwa na mikanda ilioshika vyema suruali zao, huku kukiwa na kibeti cha kuhifadhia kisu na kisu chake. Vifuani mwao kulining’inia mabomu ya kurusha kwa mkono. Mikono yao ilivikwa glavu maalumu zilizokuwa zimekatwa vidoleni.
Bunduki zao zilikuwa na viwambo vya kuzuia sauti.
Hadi wanaingia katikati ya kijiji kile kilichoko mkoani Bujumbura , wilaya ya Gatumba. Walikuwa wametembea umbali wa kilomita moja na nusu na walitokea kwenye msitu wa Kamori ,ulioko nchini Congo, kilomita moja tu, kufika Gatumba Bujumbura.
Makazi ya watu, yalitawaliwa na ukimya wa kutisha, huku sauti zikiwa ni za wadudu wapendao usiku, mara chache walisikia sauti za mbu karibu na masikio yao lakini hazikuwa na madhara kwa kuwa walikuwa wamejipaka mafuta maalumu kwa wadudu wa aina ile.
Watu wale ambao walivaa kijeshi, walikuwa wanatumia ramani, na ramani ilikuwa imewafikisha hadi karibu na nyumba moja, iliokuwa inaukubwa kuliko nyumba zingine pale kijijini.
Taarifa waliokuwa nayo juu ya nyumba ile, iliwafanya wasimame kwa muda ili kujipa maelekezo ni nini cha kufanya ili wawe ndani ya muda na bila kuleta kelele ama madhara kwa watu waliokuwa wamepumzika vyumbani mwao.
“Ndani tutaingia wawili, nje bakini wawili!” Mmoja aliongea na ndie alikuwa kiongozi wa kikundi kile cha watu wanne, ambapo kijeshi huitwa fire.
Baada ya makubaliano yao waligawanyika; ambapo wawili waliizunguka ile nyumba na wawili walianza kusogea karibu na mlango wa ile nyumba. Wakati wanaukaribia mlango, kiongozi alinyosha mkono wake wa kushoto na kuupunga juu mara mbili, hali ile ilisababisha aliekuwa nyuma kusimama na kutulia kimya huku kichwa chake kikizunguka kwa kasi kubwa kila pande.
“ Kuna watu nane katika nyumba hii, watu hao wanasilaha kila mmoja na kuna milango mitatu ndani ya nyumba hii, hivyo kasi yetu ndio itakayotuwezesha kuufikia mlango tulioukusudia.” Kiongozi alimwambia mwenzake aliekuwa nae.
“Hakika kamanda” alijibu yule bwana, akiwa bado kasimama kimya na macho yake makali, yakiona vingi katikati ya giza zito lililokuwa limeikumbatia anga ya Gatumba.
Kwa mbali walisikia sauti za watu wakicheka na kupiga miluzi, sauti zilitoka kwenye ile nyumba waliotarajia kuingia muda mfupi uliofuata.
Haraka kiongozi akanyoosha tena mkono wake na kupunga vidole vyake viwili kuelekea mbele. Ilikuwa ni ishara ya kusonga mbele, huku aliekuwa nyuma yake, akitangulia mbele na yeye akigeuka nyuma ili kumlinda wa mbele yake.
Licha ya kujongea kwa kasi na kulindana kila walipopiga hatua nne, lakini vishindo vyao havikuwastua watu wa nyumba za jirani, wala wale waliokuwa wanacheka.
Nyumba ile ina dirisha upande wa mbele, hivyo walipofika usawa wa dirisha, kiongozi alipunga mkono wake hewani mara moja, haraka jamaa aliekuwa nyuma yake, alinyata na kwenda mlangoni na kujibanza akingoja hatua iliofuata.
Kiongozi wa Kikosi hiki, alikuwa anasikiliza sauti za watu waliokuwa wanacheka, aligundua wanacheza karata na walikuwa zaidi ya wanne. Aliitizama saa yake, ilimuonesha zimesalia dakika tano kabla muda waliopanga kuanza tukio lilowaweka pale.
Taratibu alianza kugusa dirisha kwa mtindo wa kutelezesha vidole, kutoka upande wa kushoto wa dirisha, kwenda upande wa kulia. Alirudia tukio lile mara mbili na kutulia. Masikio yake hayakusikia zile kelele za vicheko, ni dhahiri waliokuwa ndani walisikia alichokifanya na walingoja afanye tena. Lakini yeye hakutaka kurudia, bali aliwaacha watafakari wanavyoweza kuhusu walichosikia.
Aliachana na dirisha, haraka alienda mlangoni ambapo alikuwawepo mtu mwingine, alipofika aligonga mlango mara moja na kisha alimtizama jamaa aliekuwa pembeni yake na kumpa ishara fulani kwa kupandisha kichwa juu chini, kisha aliondoka na kuelekea dirishani tena.
Alipofika dirishani, alirudia kufanya kile alichokuwa amekifanya hapo mwanzo na kutulia, huku akiweka sawa silaha yake, mana alijua matokeo ya alichokifanya.
Alivuta hisia na kuisikia mijengeo ya watu watatu wakisogea pale dirishani na mmoja akielekea ulipo mlango.
Alingoja hadi dirisha lilipofunguliwa, nae haraka aliwasha kurunzi iliokuwa kwenye kofia yake na kitendo kile hakikutegemewa na aliefungua dirisha, hivyo aliinama ili kuupisha mwanga ule, lakini hakujua kufanya vile ilikuwa ni kucheza na maisha ya wenzake, ambao walikuwa nyuma yake, ambao walijikuta wakirushwa juu na kutupwa chini kwa nguvu, walikuwa wamekutana na risasi za bunduki ya mkanada.
Yule aliefungua dirisha na kuinama,alinyuka ili atizame wenzake aliowasikia wakilia kwa uchungu, lakini hakufanikiwa kuwaona, kisu cha shingo kilitamatisha uhai wake.
Baada ya shambulizi lile, komando yule aliruka hatua moja kubwa na kuelekea mlangoni palipokuwa na komando mwingine. Alikuta nae kamaliza kazi ya watu wawili waliokuwa wameenda kuufungua mlango.
“Clear?” Aliuliza komando kiongozi.
“Yeah” alijibu komando aliekuwa mlangoni.
“Wamebaki watatu hapa ndani, hivyo tuna dakika sita pekee.” Aliongea komando kiongozi.
“Copi tha…” alijibu komando aliekuwa mlangoni, kisha walipeana ishara na kuanza kunyata kuingia ndani ya nyumba ile, ambayo ilijengwa ikiwa na vyumba vitatu vilivyoelekeana.
Ndani ya nyumba ile, kulikuwa na taa zinawaka hivyo kuleta mwangaza na kuwawezesha makomando wale kuona vyema
*****
WALE MLIOPENDA KUONA NAANDIKA KITABU (HARD COPY), HABARI NI NJEMA..
KITABU CHA JASUSI, KOMANDO(based on a true story), sasa kipo hatua za mwisho kukamilika.
Ukipenda kukiweka maktaba kwako, bei ni Tsh 10000'/=. Mikoani utatumiwa..
Lakini kwa wakazi wa Dodoma na Dar, nitawaletea mlipo..
Japo hali yangu kiafya haijawa sawa sana, baada ya kutoka chumba cha upasuaji wiki mbili nyuma... Naamini nitakuwa sawa, japo kupiga mazoez na kukufikia ulipo.
Hivyo wasiliana nami kwa kuweka oda yako mapema...
Hakikisha unapoweka oda, unauhakika wa kulipia.
Wasiliana nami kwa namba 0758573660.
Whatsapp tu, tumia 0658564341.