Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 166
- 182
Kikongwe wa miaka 90 arejeshewa Ardhi yake
Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Mwanza, limefanikiwa kumrejeshea eneo lake kikongwe wa miaka 90 Anastazia Ndazi.
Baraza hilo limemrejeshea eneo lake lenye ukubwa wa mita 60 (urefu) na upana wa mita 30 lililopo Bwiru Ziwani Ilemela mkoani Mwanza.
Kesi hiyo namba 179 ya mwaka 2012 ilikuwa baina ya mpeleka maombi Yohana Magayane na mjibu maombi Anastazia Ndazi.
Kesi hiyo ilikuwa chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Mwanza Mayeye Sigiti Magambo ambaye ametoa uamzi wa kesi hiyo leo asubuhi.
Mwenyekiti huyo akitoa uamuzi wa kesi hiyo iliyoanza mwaka 2012, ambapo Leo bibi huyo amepewa ushindi huo baada ya ushahidi wa pande zote mbili kupitiwa.
Mwenyekiti wa baraza, amesema mleta maombi anadai ardhi hiyo alipewa na baba yake mdogo mwaka 1986 na aliishi hapo bila shida yoyote mpaka pale baba yake huyo mdogo alipofariki, shangazi yake ambaye ni mjibu maombi alipoanza kuamru aondoke.
Baada ya mvutano huo kuendelea, alifungua kesi katika Baraza la kata ya pasiansi wilaya ya Ilemela ambako alishinda na baadae mjibu maombi (Anastazia Ndazi) kukata rufaa Baraza la wilaya ambako pia alishinda.
Mleta maombi baada ya kushinda Baraza la wilaya, shangazi yake ambaye ni mjibu maombi alikata rufaa mahakama kuu kisha mahakama kuu ikaamuru irejeshe Baraza la wilaya kwa kusikilizwa upya.
Mwenyekiti alidai baada ha kesi kuanza kusikilizwa upya, mleta maombi mleta alisema eneo hilo alipewa mbele ya kikao cha familia na barua ilitolewa ambayo aliiwasilisha kwenye baraza.
Kwa upande wa mjibu maombi eneo hilo aliinunua na alikaa kwenye eneo hilo kwa miaka 15 na akaeleza kwamba ana nyaraka zote za kulipa kodi za Serikali.
Amesema mjibu maombi aliwasilisha risiti za kulipa kodi ya ardhi na kodi ya jengo.
"Mjibu maombi huyo katika risiti tano za kodi ya ardhi na aliwasilisha risiti nyingi tano za kodi ya jengo risiti na risiti zote hizo zilichukuliwa kama vielelezo.
"Mjibu maombi aliendelea kuiomba baraza kwamba katika eneo hilo alikuwa amejenga nyumba ya vyumba vitatu na sebule ambayo ilibomolewa na mleta maombi.
"Mjibu maombi aliiomba baraza hilo itamke wazi yeye ndio mmiliki wa eneo hilo lenye mgogoro," amesema Mwenyekiti wa Baraza.
Mwenyekiti huyo baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili amedai baraza limeona mleta maombi kielelezo chake kilipitishwa na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha chatya wilaya ya kyera mkoani Kagera wakati eneo linalolamikiwa lipo Bwiru Mwanza.
Mwenyekiti huyo alidai kuwa baada ya kielelezo hicho kimeonesha kina mapungufu huku mjibu maombi yeye ameonesha namna alivyokuwa analipa Kodi za Serikali kwa kipindi chote.
"Hivyo basi natamka wazi mjibu maombi Anastazia Ndazi kama mmiliki halali wa eneo hilo kwa kuwa ameweza kuidhibitishia mahakama namna alivyokuwa analipa Serikali kodi, pia mleta maombi unalazimika kulipa fidia," alisema Mwenyekiti wa baraza.
Nje ya mahakma
Anastazia Ndazi ameishukru Serikali kupitia baraza la Ardhi wilaya ya Mwanza kutenda haki kwa kurejeshewa eneo lake ambalo alikuwa amedhurumiwa na Yohana Magayane.
Pia amelishukuru Shirika la Kutetea Haki za wanawake na wasichana la KIVULINI jijini Mwanza chini ya Mkurugenzi mtendaji Yassin Ally kwa kusimamia na kufuatilia kesi hiyo kwa kila hatua mpaka leo hii.
Kwa upande wake, Yohane Magayane amedai kuwa uamzi uliotolewa na baraza hilo yeye hakubaliani nao na kuongeza kwamba atakata rufaa makama kuu.
Amesema katika eneo hilo yeye ana viwanja viwili na kwamba bibi kikongwe huyo hana eneo lolote huku akidai kwamba ameonewa.
"Baba yangu mdogo alinipa eneo hilo tukiwa msibani mkoani Kagera kwa hivyo alinikabidhi kwa kuwa ndugu zangu wote walikuwepo na hivyo isingewezekana kuja mpaka Mwanza," amesema Magayane.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea Haki za Wanawake Nina wasichana, Yassin Ally amesema haki ya bibi huyo, imetendeka ameweza kupata haki yake huku akiomba utekelezaji wa hukumu uende kwa Kasi.
Amesema Bibi huyo mwenye umri wa zaidi ya miaka 90 hakuwahi kufanikiwa kupata mtoto na kwamba kuna wajanja wachache wenye pesa kupitia mleta maombi (Magayane) kutaka kumdhurumu Bibi huyo.
Yassin amewaomba watu kuwa na utamaduni wa kutunza vielelezo kama alivyofanya bibi huyo kwa kutunza nyaraka zake za miaka 30 iliyopita.
MWISHO