Kikombe cha babu kilinitenganisha na mpenzi wangu

Kikombe cha babu kilinitenganisha na mpenzi wangu

ma jery

Senior Member
Joined
Jun 15, 2011
Posts
171
Reaction score
65
Nakumbuka mwaka 2011 nilianza mahusiano na kijana mmoja hapa dsm.
tukaanza kutembea kimwili kwani nilimuamini na nilimpenda alinitambulisha kwa wazazi ,marafiki zake na ndugu zake wote.
tukiwa katika dimbwi la mapenzi taarifa zikazagaa kama mnavojua kwamba kuna mzee loliondo anatibu magonjwa yote hadi ukimwi.
Siku moja mpenzi wangu akaja usiku kuniaga kwamba anakwenda loliondo...mimi sikuwa nafahamu kama ana tatizo lolote .nikamuuliza kwani mwenzagu una ugonjwa gani ? akaniambia yeye anaenda tu kuna watu anawapeleka.pia akasema hayanihusu.huyoooooo akaondoka.
Baada ya siku nne akarudi.ila akaniambia mimi nimeshatibiwa sitaki tena mahusiano na wewe.nikamuuliza kwanini mwenzanguu?....
akaniambia wewe cha kufanya tafuta hela uende loliondo ...utapona ugonjwa wako.
akaniambia mimi bwana kuna siku nimetembea na changudoa na sikutumia condom..kwa hiyo sijui kama nipo mzima.ila mimi nimeshatumia kikombe cha babu sina HIV tena.....LOH JAMANI MIMI NILIONA DUNIA INAZUNGUKA. USIKU SILALI NIKILALA NAOTA TU NINA HIV MARA NINAZIKWA....NDANI YA SIKU MBILI NILIZEEKA.
NIKASEMA CHA KUFANYA NITAFUTE TU HELA NIENDE LOLIONDO................Bahati mbaya sikupata hela na nyumbani sikuweza kuomba hela kwasababu najulikana sina tatizo lolote la ugonjwa...nikaanza kuishi kwa matumaini mpenzi nae akanimwaga.
Basi nimeishi kwa matumaini toka hiyo 2011 hadi mwaka jana mwishoni nilipoamua kupima.Mungu ni mwema nimepima hadi hapa nairobi sina ukimwi wala malaria..nikamwambia yule barazuli akasema hata yeye hana..kumbe yule changudoa hakumwambukiza na anataka turudiane.
 
Kumbe babu aliacha madhara hivi........
 
enh!........ haya hadithi njooo!!!!!!!!!!
 
Siku hizi tumechoka kusoma vitu vya namna hii, huo muda wa kuingia na kutoka hatuna tena.
 
Hizi stori za wadada za groups za fb nahisi hazifai jf. Napita..
 
ma jery nakuaminia kwa story zako za mazombi,si we juz ulileta ile ya mkaka asiokua na kifanyio wa unicef siju au???

Haya malizia nipo standby mimiii
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom