Kikojozi

Kikojozi

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2010
Posts
2,696
Reaction score
740
Baba mmoja alikuwa kikojozi. Tabia hiyo ilikuwa kero kwa mkewe kiasi cha kutaka kuachika. Hata hivyo mama akaenda kwa siri kwa mganga Kingalu ili apate dawa ya kumponya mmewe ugonjwa wake. Mganga kisha kumwambia mama kuwa ugonjwa wa mmewe ulisababishwa na jini, akampa dawa na maelekezo ya kuitumia kwa kuchanganya kwenye maji ya kuoga, bila kumjulisha mmewe.

Siku mme aliyotumia dawa akafanya mambo ya ajabu zaidi; akajisaidia haja kubwa kitandani. Mke akamuuliza mme imekuwaje?

Mme akasimulia:

Niliota wewe umeenda kwa mganga ili upate dawa ya kutibu nisikojoe kitandani. Mganga alikwambia kuwa jini ndilo husababisha nikojoe kitandani na akakupa dawa uichanganye katika maji yangu ya kuoga. Kisha ukaniambia nikilala usiku nisisinzie kwa kuwa jini hilo litakuja dirishani kwetu. Ukaniambia nikilisikia nifungue mlango nilifukuze mpaka litakapoingia kwenye shimo la choo. Kisha likishaingia chooni nilinyee, na ndio utakuwa mwisho wangu wa kukojoa kitandani. Akamalizia kusema: "Nasikitika niliposhituka kutoka usingizini nikakuta nimeharibu. Mke wangu hii ndoto ni mbaya sana. Itabidi kesho niende kwa mganga Kingalu, ambaye nasikia ni maarufu eneo hili, ili nitafute tiba"

Mkewe baa ya kusikia yote akamjibu mmewe. "Usinde kwa mganga, heri uendelee kukojoa kitandani"!
 
Back
Top Bottom