Kikiwete: Afrika inaweza kuhimili ushindani iwapo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikiwete: Afrika inaweza kuhimili ushindani iwapo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, May 7, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete.  [FONT=ArialMT, sans-serif]Rais Jakaya Kikwete amesema ushirikiano wa kimataifa na kuondolewa kwa vikwazo vya biashara dhidi ya nchi zinazoendelea, vitasaidia kukuza uchumi wa bara la Afrika ili uhimili ushindani duniani.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Pia Rais Kikwete amesema mazingira rafiki yatakayowezesha bidhaa za nchi zinazoendelea kulifikia soko la mataifa yaliyoendelea, ni miongoni mwa nyenzo zinazohitajika katika ukuaji wa uchumi wa bara hilo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Rais Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwasilisha hoja katika mdahalo uliofanyika wakati Kongamano la Kimataifa la Uchumi Duniani (WEF), unaofanyika jijini Dar es Salaam ukizilenga nchi za Afrika.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema ushirikiano huo unapaswa kuwepo katika sekta za umma na binafsi, ili kuwezesha matumizi ya rasilimali zilizopo barani Afrika zinufaishe mataifa ya kiafrika.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mdahalo huo ulioongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa WEF, Klaus Schwab, uliwajumuisha pia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT), Anna Tibaijuka.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wengine ni wenyeviti wenza wa WEF, Ajai Chowdhry (India), Joergen Ole Haslestad (Norway) na Pat Davies na Kuseni Dlamin (Afrika Kusini).[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Watu wengine mashuhuri walioshiriki kwenye mkutano huo ni Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tshavangirai, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Rais wa Zambia Rupiah Banda na Rais wa Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Kanayo Nwanze.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Rais Kikwete alisema Afrika ina rasilimali nyingi ambazo hazijatumika ipasavyo, na kwamba miongoni mwa changamoto zilizopo ni kwa kiasi gani (rasilimali) zinazotumika zimelinufaisha bara hilo kwa maendeleo yake.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema licha ya kuwepo rasilimali hizo, Afrika inakabiliwa na upungufu wa mahitaji kama vile ujuzi, teknolojia na mtaji wa fedha, hali inayojenga mazingira ya kuhitaji ushirikiano hususani na mataifa yaliyoendelea.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Rais Kikwete alisema viongozi wa Afrika wamefanikiwa kuweka sera bora za kiuchumi zenye lengo la kukuza uchumi wa mataifa yao, na kwamba jitihada hizo zitafanikiwa zaidi kupitia ushirikiano.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, Rais Kikwete alisema ushirikiano huo unapaswa kufanyika katika hali ya kila upande kunufaika.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Ikiwa utafanya uwekezaji unaotoa taswira ya umiliki wa mataifa wa nje pasipokuwa na kiashiria cha wamiliki wa ndani, hilo halitakuwa jambo jema,” alisema.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Rais alisema nchi zilizoendelea zinapaswa kuondoa vikwazo vinavyozuia bidhaa kutoka mataifa yanayoendelea zikiwemo za kiafrika.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Tunahitaji kuwa na uhakika wa kufanya biashara, uhakika na kunufaika na masoko makubwa katika nchi zilizoendelea,” alisema.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, mshiriki mmoja kutoka Ghana alipendekeza majadiliano ya ushirikiano yahusu maeneo yaliyo nje ya uwezo wa Waafrika.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Lakini akijibu hoja hiyo, Rais Kikwete, alisema kinachohitajika katika majadiliano ni kuwateuwa wataalamu nguli kutoka sekta husika.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Pia Rais Kikwete alielezea umuhimu wa kuwandaa vijana katika nyanja tofauti za kijamii, hasa kwa kuwapa elimu bora, ujuzi na stadi zitakazowawezesha kubuni, kusimamia na kuendeleza uchumi wan chi zao.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Naye Tibaijuka alisema mtaji wa uhakika ni suala la msingi katika kufanikisha matumizi ya rasilimali yenye tija kwa Afrika.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Pia Tibaijuka alisema wanawake ambao ni asilimia 51 ya Waafrika wote, wanahitaji kuwekewa mazingira yatakayowawezesha kuchangia na kunufaika na ukuaji wa uchumi barani humo. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa upande wake, Davies alielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha mfumo wa kufanya biashara miongoni mwao, kama sehemu ya kufanikisha jitihda za kukuza uchumi wa bara hilo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Naye Chowdhry alisema pamoja na mambo mengine, utayari wa viongozi barani Afrika una nafasi kubwa katika kukuza uchumi wa mataifa yao.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati huo huo, Tanzania imebainika kupoteza Dola milioni 240 (takribani Sh. Bilioni 336) kutoka katika pato la Taifa (GDP) kila mwaka kutokana na ugonjwa wa malaria.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati hali ikiwa hivyo nchini, bara la Afrika linapoteza kiasi cha Dola bilioni 40 kila mwaka kutokana na ugonjwa huo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji wa Standard Bank Group ya Afrika Kusini, Clive Tasker, alisema takwimu hizo zilitokana na utafiti uliofanyika na ambao ulionyesha pia kuwa gharama zinazotokana na malaria kwa kampuni yake zinafikia Dola milioni sita.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Tasker alisema hayo kwenye mkutano huo uliohudhuriwa pia na Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa Viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria (ALMA).[/FONT]  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...