Kikazi zaidi

Kikazi zaidi

Walikuwa washenzi sana halafu watoto wakiumizana wanawafundisha kusema uongo kuficha maovu yao
Kuna moja sitoisahau.

Tulichonganishwa na mtu alietuzidi umri sie tulikuwa wawili yeye peke yake, walahi kilichofuata siri yako. Tulipigwa sana.

Ila mimi yalikuwa hayakuisha yule jamaa tuliomchangia mande alikuwa na mdogo wake makamo yangu kwa kweli nilimchapa sana kulipiza kisasi hadi ikafikia mambo ya vikao, tukasuluhishwa. Kumbe kwa yule Kaka mtu hayakuisha. Kaka mtu akakutana na mimi tena baada ya kusuluhishwa kwa kweli alinipa kipigo kufikia hadi kufikia kutoka manundu. Maza anaonana na mimi jioni ananiuliza kulikoni? Mimi nikamdanganya Maza nimeumia mpirani huwezi amini.

Ila na mimi yalikuwa hayajaisha nikawa bado nimemmandi kwa kipigo kitakatifu alichonipa kwa kweli nitakuchosa kusoma nikisema nielezee kwa urefu.

Ngoja nifupishe kidogo yule jamaa aliingia cha kike na mwenzake wakawa wanaenda Msikitini na kwa kawaida lazima wapite kwetu njia ya mkato, kwa kweli nilitupa mawe mengi sana ambayo nilikuwa nimeyajaza kwenye kisalfeti nilikuwa nayakusanya nayapandisha juu ya bati kidogo kidogo mpaka yakawa mengi mchanganyiko na mawe ya kokoto humo humo, nilipeleka mawe hiyo siku mpaka jamaa anapiga mayowe "nakufa" nilipoona kelele zimezidi ikabidi niingie mitini kuua soo kwanza.

Huwezi amini yule jamaa baada ya siku ya tukio ikawa heshima na adabu, tulikutana na yeye mtu mbili tu na akufanya lolote tulipishana kwa usalama
 
Hahahahaaaa hahahahaaaa hahahahaaaa nimecheka mpaka machozi wallah! Visasi vya utotoni acha tu, kuna zile Nguni za mtaa kwa mtaa sisi tuliwafuata jamaa kuwachapa huko huko kwao baada ya tambo za muda mrefu

Sasa kufika kwao inabidi tuvuke mto ambao daraja lake ni magogo makubwa mawili, tukavuka tukaingia mtaani kwao full mziki tukawachapa mpaka mwisho wa mtaa huku wengine wakitokomea kusikojulikana

Kumbe washenzi wale walikuwa wameandaa upu.pu wa kutosha pale darajani na wale walitokomea kumbe walienda kuyaondoa yale magogo ya daraja na kutusubiri

Hamadi tunafika pale daraja halipo kugeuka tukakutana na vumbi la kufa mtu la ----- hatuna pa kukimbilia zaidi ya kujitosa majini sitakaa nisahau
 
Ya kwako kali sana.

Unaoga bila kupenda na nguo zako mwilini
 
Halafu maji yenyewe yalikuwa meusii waste product toka kiwanda cha kutengeneza kiwi, hivyo yalikuwa hayafai hata kuoga na yalikuwa yanaharibu nguo kwahiyo tulipata adhabu mara mbili nguo kuharibika na Upu.pu
 
Ilikuwa kasheshe si mchezo.

Ila ujue wazazi wanajua kuchunguza mambo kama huamini angalia mfano mtoto yoyote yule kama anasema jambo la uongo unaona kabisa hapa naongopewa ila unanyamaza, na kwa mfano huu ile siku Maza aliamua anyamaze tu wewe mpira gani utoke manundu usoni! labda ingekuwa mpira(cha ndimu) kilichofumwa kwa kokoto yale malailoni yakianza kuchoka kokoto zinaanza kuchomoza.

Maza alistukia mchezo sema alipotezea tu, na hili nimekuja kugundua baadae nilipoanza kukua na kupata akili ya kikubwa nikajiambia kimoyo moyo Maza uongo wangu aliustukia ile siku sema aliamua kunyamaza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom