Kikao cha wanawake 11 kuchambua waume zao 'Chambu Chambu'

Kisai

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
27,981
28,098
Hii ni habari iliyonukuliwa toka katika kinywa twahara, ikielezea kikao kilicho kaliwa na wanawake 11, wanawake ambao walijumuika kwa ajili ya kuwaelezea waume zao kinaga ubaga, yaani nje ndani,na kuwekeana sharti la kuwa,kila mmoja kati yao asifiche kitu chochote kuhusu mume wake.

Mada hii nimeileta kwenu hasa kwa ajili yetu sisi wanaume na kwa ujumla na wanawake pia. Kwani kuna mengi ya kujifunza juu ya habari hii.

Nitakuwa naweka maneno ya mwanamke mmoja au zaidi mpaka watakapo fika wote 11. Ila sitaweka wote kwa ujumla ili nisiwachoshe.

Lengo au malengo ya kuwawekea kikao hiki

1. Kuwaonyesha Wanawake namna nzuri ya kuwazungumzia waume zao pindi wakiwa wenyewe,peke yao katika vikao vyao (Hili tunajua fika huwa mnatuzungumzia sana). Sababu husemwa mara nyingi wanawake wakiwa peke yao zaidi ya asilimia hamsini katika mzungumzo yao huwazungumzia Wanaume.

2. Kuwakumbusha matumizi mazuri ya lugha ya staha na uchaguzi mzuri wa maneno. Yaani kutumia mafumbo ikinidi, mafumbo ambayo ndiyo uwazi wenyewe,yaani unaweza kuta mwanamke anakuelezea kwa mafumbo na anakuwa amekuweka wazi mno ila kwa uchaguzi mzuri wa maneno kama tutakavyo ona katika kikao hiki.

3. Kutukumbusha sisi wanaume kuwafanyia wema wake zetu na kuwa na tabia nzuri kwao, kwa sababu nyingi,kwanza wema hauozi, hata ikitokea tukaachana na wake zetu basi watuelezee kwa wema,lakini kadhalika utu na kuyafanyia kazi maamrisho ya dini.

Tanbihi

Kwa kuchunga nidhamu na adabu za unukuzi habari. Kuna vitu sitaviweka wazi mpaka nitakapo maliza kuweka kikao hiki,kisha nitaweka marejeo ya kurejea kwa ajili ya faida zaidi.

Naanzia hapa....

Anasimulia msimuliaji :

Walikaa wanawake kumi na moja siku moja,wakaafikiana juu ya kuwaelezea waume zao pasi na kuficha kitu chochote.

Mwanamke wa Kwanza

"Mume wangu mimi ni kama nyama ya ngamia iliyo ngumu kabisa. Ambayo iko juu ya kilele cha Mlima,mlima ambao unateleza. Mlima huo siyo mlima mwepesi kuupanda,ili kwenda kuchukua nyama hiyo,wala nyama yenyewe si mnofu ambao unaweza kuuchukua kwenda kuupeleka nyumbani."

Mwanamke huyu alikuwa akimaanisha ya kuwa mumewe ana tabia mbaya mno,yaani hachukuliki wala haingiliki.

Mwanamke huyu akawa ameishia hapo.

Mwanamke wa Pili

"Mume wangu mimi ni kama usiku wa sehemu za tambarare (Usiku ambao hauna baridi wala hauna joto). Ukikaa nae huwezi kuogopa wala huchoki (Yaani ukikaa pembezoni mwake una pata amani wala hupati khofu yoyote,yaani humchoki).Yaani si wa joto wala si wabaridi na wala si MPUMBAVU, yupo kati na kati."

Hapa Mwanamke huyu alimsifia mume wake kwa sifa nzuri sana.

Mwanamke wa Tatu

"Mume wangu ni jitu kuubwaaa (mwili mkubwa) lisilo na akili(Yaani mwili mkubwa lakini akili kisoda,kama tusemavyo sisi Waswahili). Mimi nikisema tu ataniacha. Nikinyamaza nakuwa kama sina mume hivi,yaani nipo nipo tu.

Yaani mume wake hataki kumsikiliza mkewe,yaani akisema tu basi talaka.

Mwanamke wa Nne

" Mimi mume wangu sitataja habari zake, kwani nikumuelezea zitaacha kitu kumuhusu,yaani nitaweka bayana dhahiri yake na undani wake (kwa lugha zetu ni sawa na kusema "A to Z"),na kama akijua ataniacha."

Mwanamke huyu akapita kimya.

Itaendelea ....

Ni mimi Zurri, ndiye Jurjani na sasa ndiye Mubarridi. Nawaenzi wakubwa wangu.
 
Mods anuani ya uzi wangu mmeiharibu,mngeiacha vile vile kama nilivyo iandika.

Isomeke : Kikao cha Wanawake 11 wakiwachambua waume zao "chambu chambu"

Si kama mlivyo weka sasa.

Shukrani.
 
Back
Top Bottom