Kikao cha wanaume

Hakuna aliyehukumu,na kwa kutumia ID fake haiondoi uhalisia wa mwanamke au mwanaume,uhuru upo na kwa mtazamo wako kama mwanaume uhuru huu unatakiwa kuwa hivi? karibu

vyovyote mana hujui anachokifikiria wewe unataka uwe vipi?
 
Labda wengine wanajiadhari na Ban lakini vipi kuhusu hawa wanatumia za kike?

sawa, wengine Ni kwa ajili ya hizi ban lakini kwani ukipigea ban huwezi kutulia mpaka ufunguliwe? Kwani humu Ni oxygen usipoipata hutaishi?? Pili, hao wenye IDs zaidi ya moja, wengi hutumia uhusika tofauti, ID moja aonekane mtu WA busara Sana, nyingine aandike -----...sielewi, kwa nini hatuwezi kuwa sisi? Mfano, humu Kuna wanaonifahamu kiuhalisia, lakini sijawahi kuogopa kuandika chochote, hata masihara nafanya bila kuogopa mtu...

Hao wanaojifanya wanawake, sina komenti aisee...kuna walakini Sana mwanaume kujifanya yeye jike!!!!
 
karibu sana miss, Mimi napenda kande za maziwa mtindi..ushawahi?

Godfather bwana.

Could it be unanisaidia because it is the only food am eating with relish?

Nimepika jana leo nikamalizia kiporo,za chumvi lakini.

And what is this about mtindi?
 
Dah kumbe huyo Mwanaume?
 
I think the same way too Karucee that's why women who act like men are more appreciated by men themselves they are considered as unique,but men who act like women they are considered as strange creatures and they are neither admired nor welcomed by most of the people who understands themselves excpt for those few who sin to them is something to enjoy!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Dah kumbe huyo Mwanaume?

Kabisa,hadi amekorofishana na watu humu walipomuumbua. Fuatilia post zake kule jukwaa la siasa,katiba mpya na hoja mchanganyiko,anaporomosha matusi ambayo kwa akili ya kawaida mwanamke hawezi kuyatamka. Dume zima kabisa [ila sio la mbegu]
 
Godfather bwana.

Could it be unanisaidia because it is the only food am eating with relish?

Nimepika jana leo nikamalizia kiporo,za chumvi lakini.

And what is this about mtindi?

Mtindi ni maziwa mgando
 
Wewe kwa mtazamo wako unalionaje,inakuaje utakapojkuta unawasiliana na mtu PM ukidhani wa kike kumbe wa kiume,utafikiria nini kuhusu huyo mwanaume?

Well, ndo maana huwa sivamiagi watu au vitu hovyo hovyo. Niko mwangalifu sana maishani. Nimeshasema mara nyingi sana kuwa JF ni msitu, tena ulio mnene.

Kwa sababu hiyo, kwanza , sina sana mazoea ya kuwasiliana na watu humu kwa njia ya PM. Pili, hata nikifanya hivyo nakuwa niko mwangalifu sana kuhusu mambo ninayowasiliana.

Amini usiamini watu huwa wananitumia PM kuniomba mambo mbalimbali yakiwemo kuwafundisha Kiingereza, kuwanunulia vi-gadgets ili kama narudi Tanzania niwaletee, kuwafanyia proof readings za kazi au assignments zao za shuleni au kazini, na mengineyo mengi tu.Kawaida yangu huwa nazipotezea tu PMs kama hizo.

Tatu, huwa nina machale sana. Unapowasiliana na mtu kuna mambo ambayo mtu unaweza kuyang'amua endapo utakuwa mhalisia. Kuna mambo huwa haya-make sense hata kidogo. Sasa uwezo kama huu haufundishiki. Ni wa kuzaliwa nao pamoja na tajiriba yako ya kimaisha.

Nikiona mtu haeleweki eleweki napotezea au namchukulia hivyo hivyo tu. Hakutakuwa na seriousness yoyote ile. Sasa itokee kuwa huyo ninayewasiliana naye kuwa ni wa kiume ilhali anajiwasilisha ki-kike, nitampotezea tu kwa kunipotezea muda wangu.

Maana sababu za yeye kujifanya hivyo anazijua mwenyewe na kwa kweli haitanistahili mimi kupoteza muda wangu kuanza kuwaza na kuwazua kulikoni huyo mtu yuko hivyo. To each his own.
After all, JF ni msitu hivyo kutegemea visivyotegemewa ni hali ya kawaida. Dawa ni kuwa mhalisia tu, basi.
 
Kuna mengi ya ajabu ajabu humu,kuna wengne ni 'ME' na 'ID' zao ni za kiume lakini siku nyingine unashangaa wanaandika mwandiko wa KIKE kabisa!.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…