Kikao cha gafla jumba la Malkia UK

Kikao cha gafla jumba la Malkia UK

Uingereza kwa sasa haina Archduke, nchi kama Austria na Prussia enzi zile walikuwa na hii title.. na mara nyingi ilikuwa inashikiliwa na Heir apparent (Mrithi wa kiti). Na Archduke simply ni head of all dukes... Refer Archbishop.

Pia title ya Duke ni equivalent na Prince, ingawa Prince ni wale waliotoka kwenye Royal family tu.. ndio maana Uingereza Princes wote pia ni Dukes.

Duke ambaye siyo Prince anaitwa Peer, na anatoka katika Noble family (familia ya kiheshima).. sio Royal family.

noble families zinahold titles nyingi.. kwa uingereza zinakuwa chini ya familia ya kifalme na zinaitwa peerage families..

Ranks zao ni..

1. Dukes and Duchesses
2. Marquess and Marchioness
3. Earl/Count and Countess
4. Viscount and Viscountess
5. Baron and Baroness

Hao hapo juu ni wale ambao wanarithi hizo title (hereditary peerage), nikimaanisha ikiwa baba ana title ya Duke, akifariki mtoto anairithi na hii huendelea kwenye familia vizazi na vizazi.

Kuna wale wanaopewa heshima na Malkia au Mfalme lakini hairuhusiwi kurithisha title yao kwa watoto.. na wengi wanakuwa na title ya LORD au LADY na vilevile BARON au BARONESS.. refer Margareth Thatcher alipewa title ya Baroness.. so jina lake lilikuwa Baroness Thatcher.

Kuna pia hawa Knights, hawa hupewa heshima ya Maisha na Malkia au Mfalme lakini hawapo kwenye hili kundi la Peers.. Knights huwa na title ya SIR na baadhi ya watu maarufu kama Elton John na Richard Branson wanayo hii title.

Kama una swali lolote uliza..
Mkuu asante kwa ufafanuzi.

Kuna house, mfano ukifatilia hii story utaskia house Fulani wanataja, hizi house zinahusikaje katika utawala?. Mosi

Pili, Naomba nielezee warithi wa queen elizabeth kuanzia atakaye mfuatia saivi mpk yule mtoto wa juzi Charlotte.

Tatu, kuna tetesi kuwa princess Diana aliuwawa sababu ya kutaka kuolewa na mwarabu. What's your comment?

Huu uzi utakuwa darasa kubwa kwangu. Pia Kama umeiva katikamaswala ya utawala wa kanisa katoliki utakuwa msaada kwangu.

Natanguliza shukrani.
 
Kuhusu kanisa siwezi kusema chochote kwa kuwa ni mambo ya imani na pia kanisa lipo more complex..

Ukisikia house ni namna nyingine ya kusema familia..

Tunaposema royal house ni sawasawa na Royal family.. vilevile noble house ni sawasawa na noble family.

Ila unatumia house pale unaposema majina yao ili kutofautisha na familia za kawaida.. mfano.

Kama wewe ukoo wako ni Massawe tunasema Massawe family ila kama ingekuwa ni royal house tungesema House of Massawe.

Familia ya malkia ina jina lake nalo ni Windsor-Montbatten (sina uhakika kwenye spelling) so officially inaitwa House of Windsor-Montbatten.

Na vilevile noble family zina majina yake kutokana na Rank, mfano familia ya Orleans ilikuwa noble family yenye nguvu sana kipindi France ilipokuwa chini ya mfalme.. na iliitwa House of Orleans.

Wafalme wa Austria walikuwa wanatoka familia ya Habsburg ( House of Habsburg) Russia ilikuwa Romanov (House of Romanov), Mfalme wa Uholanzi (Netherlands) anatoka familia ya Orange (House of Orange) n.k hapo nafikiri umeelewa.

Kuhusu Princess Diana ni ngumu kwa kuwa ina nadharia nyingi ikiwamo hiyo ya kuuwawa, so wengine wanaweza kuchangia ila siwezi kuongelea chochote maana hamna uhakika sana.

Kuhusu nani atamrithi malkia; sheria za kurithi zinaweka warithi kwenye mstari (line of succession) Warithi ni watoto wa kwanza wa watoto wa kwanza. Mtoto wa kwanza wa malkia Prince Charles ndio Mrithi wa kwanza, anafuatiwa na mtoto wa kwanza wa Prince Charles ambaye ni Prince William Duke of Edinburgh, na wa tatu ni Prince George of Cambridge ambaye ni mtoto wa William.

So baada ya malkia anafuata mwanawe wa kwanza, then mjukuu wa kwanza then kitukuu cha kwanza.
 
Mkuu Makanjamna, nasikia kuna vimaneno Maneno kuwa kuna waingereza wanatamani waachane na huo mfumo wa Umalkia na Ufalme Queen and King. Je ni kweli ? Kutatokea impakt gani hilo liliwezekana ? Je, huu ni mfumo mzuri katika zama hizi ?
 
Ilikuwa ni kustaafu kwa Prince Philip kazi za kifalme.
 
Mkuu Makanjamna, nasikia kuna vimaneno Maneno kuwa kuna waingereza wanatamani waachane na huo mfumo wa Umalkia na Ufalme Queen and King. Je ni kweli ? Kutatokea impakt gani hilo liliwezekana ? Je, huu ni mfumo mzuri katika zama hizi ?
Hiyo ipo nchi nyingi ulaya, na ni kawaida kama jinsi na sisi tuna upinzani na chama tawala. Sio wote wataridhika na mfumo uliopo.

Ila tunajua kuwa wafalme na Malkia wengi duniani hasa nchi za Ulaya hawana nguvu kubwa kisiasa, wengi ni figureheads tu wa nchi na wapo pale kama alama ya umoja kwenye siasa za vyama, wapo kuwaunganisha wananchi wa itikadi zote.

Kwa uingereza, Malkia na familia ya kifalme bado wanakubalika (high approval rates) hivyo ni ngumu kwa siku za karibuni kuondolewa. Na vilevile sio rahisi sana kumwondoa Malkia maana utakuwa umeivunja U.K. na hilo ni gumu sana ukizingatia bado wana maumivu ya BREXIT.
 
  • Thanks
Reactions: dtj

Mkuu Sana!

Kuhusu UK mbona kwa sasa naskia eti wale wa Scottish wanataka kujitoa UK?

Pili, mbona chama cha labour kimekuwa hakina ushawishi Sana siku hizi za karibuni?

Nawasilisha.
 
kuoa kwa wenye nazo ni kujitoa mhanga
Bora hata angebaki jeshini tu.......

Halafu sipatii picha Dodi Al Fayed angeingia kwenye hio familia na kupata watoto wa kambo(half brothers wa Harry &Charles) ingekuwaje
 
Babu Prince Phillip jana Ijumaa, alitangaza kuachia kiti cha Duke of Edinburgh itapofika mwezi wa tisa mwaka huu.

Kwa sasa mzee huyo ana umri wa miaka 96 na ameamua kupumzika na kuacha shughuli mbalimbali za kijamii ambazo huzifanya akiwa kama Duke wa Edinburgh.

Prince Phillip ni kiongozi na mlezi wa taasisi zipatazo 780 nchini Uingereza na pia huwa ana miadi kiasi cha 110 za kukutana na watu au vikundi mbalimbali nchini humo.

Hivyo basi wazee hawa wawili Prince Phillip na Malkia Elizabeth wa Pili wameamua kupunguza mihangaiko ya hapa na pale nchini humo na kuwaachia Prince Charles na Prince William.

Prince Charles ni wa pili kuvalia taji la ufalme au "first heir to the throne" baada ya Malkia na anafuatiwa na Prince William au "second heir to the throne".
 
Mkuu Sana!

Kuhusu UK mbona kwa sasa naskia eti wale wa Scottish wanataka kujitoa UK?

Pili, mbona chama cha labour kimekuwa hakina ushawishi Sana siku hizi za karibuni?

Nawasilisha.

Kuhusu Scotland kujitoa, article za union zinaruhusu, lakini ni mpaka mambo mengi yawekwe sawa, hasa katika mambo ya uchumi. So kujitoa wanaweza ila sio rahisi hivyo.

Labor party na kupungua ushawishi wao labda ni sababu ya mambo ya BREXIT though UKIP ndio walikuwa champions wakubwa wa kujitoa, na conservative walitaka kubaki Labor wakaishia kuwa katikati. Ila siwezi kucomment sana labda aje mwingine mwenye ujuzi na siasa za U.K
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Uingereza kwa sasa haina Archduke, nchi kama Austria na Prussia enzi zile walikuwa na hii title.. na mara nyingi ilikuwa inashikiliwa na Heir apparent (Mrithi wa kiti). Na Archduke simply ni head of all dukes... Refer Archbishop.

Pia title ya Duke ni equivalent na Prince, ingawa Prince ni wale waliotoka kwenye Royal family tu.. ndio maana Uingereza Princes wote pia ni Dukes.

Duke ambaye siyo Prince anaitwa Peer, na anatoka katika Noble family (familia ya kiheshima).. sio Royal family.

noble families zinahold titles nyingi.. kwa uingereza zinakuwa chini ya familia ya kifalme na zinaitwa peerage families..

Ranks zao ni..

1. Dukes and Duchesses
2. Marquess and Marchioness
3. Earl/Count and Countess
4. Viscount and Viscountess
5. Baron and Baroness

Hao hapo juu ni wale ambao wanarithi hizo title (hereditary peerage), nikimaanisha ikiwa baba ana title ya Duke, akifariki mtoto anairithi na hii huendelea kwenye familia vizazi na vizazi.

Kuna wale wanaopewa heshima na Malkia au Mfalme lakini hairuhusiwi kurithisha title yao kwa watoto.. na wengi wanakuwa na title ya LORD au LADY na vilevile BARON au BARONESS.. refer Margareth Thatcher alipewa title ya Baroness.. so jina lake lilikuwa Baroness Thatcher.

Kuna pia hawa Knights, hawa hupewa heshima ya Maisha na Malkia au Mfalme lakini hawapo kwenye hili kundi la Peers.. Knights huwa na title ya SIR na baadhi ya watu maarufu kama Elton John na Richard Branson wanayo hii title.

Kama una swali lolote uliza..

Ladha ya JF imebaki kwny habari Kama hizi za Kimataifa ambazo 'Wachambuzi uchwara' wa JF hawatii kwato zao!

Shukran Jazeelah kwa Darsa duara!
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Back
Top Bottom