Kikao cha familia.......baba akirudi bar..lol...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,847
leo nimejikuta namkumbuka mjomba wangu mmoja.......
hivi...ambae niliwahi kwenda kuishi likizo moja nyumbani kwake....

nilikuwa sijui kuwa mjomba yule mlevi...mbwa...
alikuwa akija home anaonekana mstaarabu....
sasa usiku akirudi ameshalewa ndo anaitisha kikao cha familia....aisee
watoto wote wanaamshwa na mkewe anaitwa na watu wote tulio nyumbani kwake saa hizo

inawezekana ni saa nane au tisa usiku...watu wote wanaamshwa
halafu anaanza kutoa nasaha zake..lol...
ushauri na kuponda kwa wenye makosa na kadhalika...yaani....

yaani watu mna usingizi mnaamshwa kuelezwa umuhimu wa shule kwa mfano...lol..

sikurudi tena nyumbani kwake likizo ilipoisha...but nimekuja kugundua walevi weengi wana vituko mno majumbani mwao

na watoto waliolelewa na walevi wana visa viingi vya kusimulia...

hebu na nyinyi simulieni vyenu...basi.....
 
Dingi yangu alikuwa nouma,
Akirudi usiku yuko tingasi, unaamshwa na kuanza kufundishwa tuition, hapo atakuwa anawasifu walimu wake wazungu waliomfunduisha kiingereza, ole wako akute umekosea spelling za kiingereza, utachezea bakora, eti unadhalilisha lugha ya Malkia Elizabeth.................
 
my aunt akilewa bana...analia kila kitu anachoambiwa...
na anahisi hata watoto wadoogo wanamuonea yeye...sa cjui anawaona wakubwa kwa wakati ule..?

nje ya familia:huyu mshkaji wetu akilewa tilalilaa anavua suruali...abaki na boxa tu..so hapo inabidi msepe bar aise
 
leo nimejikuta namkumbuka mjomba wangu mmoja.......
hivi...ambae niliwahi kwenda kuishi likizo moja nyumbani kwake....

nilikuwa sijui kuwa mjomba yule mlevi...mbwa...
alikuwa akija home anaonekana mstaarabu....
sasa usiku akirudi ameshalewa ndo anaitisha kikao cha familia....aisee
watoto wote wanaamshwa na mkewe anaitwa na watu wote tulio nyumbani kwake saa hizo

inawezekana ni saa nane au tisa usiku...watu wote wanaamshwa
halafu anaanza kutoa nasaha zake..lol...
ushauri na kuponda kwa wenye makosa na kadhalika...yaani....

yaani watu mna usingizi mnaamshwa kuelezwa umuhimu wa shule kwa mfano...lol..

sikurudi tena nyumbani kwake likizo ilipoisha...but nimekuja kugundua walevi weengi wana vituko mno majumbani mwao

na watoto waliolelewa na walevi wana visa viingi vya kusimulia...

hebu na nyinyi simulieni vyenu...basi.....

na ww??
lolo
 
TB , Aisey ! Nina Majomba yangu kama akiwa hajanywa ni mpole mno !
Mtu anaweza kuitukana dini yake atakavyo na asijibu neno !
Cha kushangaza awe ameshalamba na asikie mtu anaizungumza vibaya dini yake hapatatosha ! Yaani akishelewa ndiyo anaiva kiimani !
Na ndiyo ataanza kuwagongea wapangaji anaowadai kodi saa 8-9 usiku .
 
Uncle wangu ana vituko vingi sana, nikianza kueleza hapa hapatoshi kwa kweli. lol
 
Mmmmh, ulevi noma, pombe isikieni tu
Kama hajawahi kunywa mmoja wa wanafamilia inachekesha
Ila akiwa wa nyumbani, it's a very sad story.

Sina experience nzuri na pombe at all.
 
Mmmmh, ulevi noma, pombe isikieni tu
Kama hajawahi kunywa mmoja wa wanafamilia inachekesha
Ila akiwa wa nyumbani, it's a very sad story.

Sina experience nzuri na pombe at all.

mshukuru mungu wako mi na ndugu yangu alikuwa hadi anaonekana mzee kumbe ana miaka 29 tu baada ya kuacha sasa hivi hadi anakitambi aiseee..
 
Jaman pombe sio chai kbs,
Kuna mdada mets wetu pale home yeye alituhadithia nyumba aliyohama huko vingunguti baba mwenye nyuma aliliwa akirudi zake kutoka kuutwika huko anawaamsha wapangaji wote bahati nzuri walikuwa wadada,anawaamrisha kupanga mstari pale nje na kuimba wimbo wa taifa then ndio wanaruhusiwa kwenda kulala,na yeye anabaki hapo nje anaimba nyimbo zote za chama enzi hizo tanu mpaka atakapopitiwa na usingizi!

Anasema alikaa miaezi 2 tu pakamshinda,ila akiwa hajalewa hana neno hata siku mkataba ukiisha hujapata hela anakuruhusu ukae tu hata miezi 3 ukupata aunamlipa yani anakuwa na upendo na yuko fresh tu ila akilewa tu ndio hivo tena!
 
Marehemu shemegi yangu alikwa anaishi Korogwe. Huwa mara moja au mbili kwa wiki anaenda Tanga ili akusanye mali ya maduka yake. Lakini akiwepo Tanga, punde akimaliza shopping yake anaingia Bar na kuagiza chupa ya Johny mtembea. Atakunywa hadi mabasi yote ya kurudi Korogwe yamesha enda. Ana anza kukashifu mfumo wa usafiri na baadae anakodi Taxi ya kumpeleka Korogwe. Alikuwa anaimba saaana manyimbo ya JJB, Atomiki na Moro Jazz ya zamani. Lakini alikuwa mtu mzuri sana. Mimi nilikuwa napenda saaana kwenda kwake wakati wa likizo.
 
Mimi nikilewa kwa maana ya kupata nishai kidogo kwa sababu si mnywaji wa kupita kiasi huwa akili zinachaji kweli na kumbukumbu za marafiki zangu wa zamani hunijia....kwa kweli kama nina namba zao lazima niwapigie.

Siku moja nilimpigia binti mmoja ambaye alikataa kuwa na uhusiano na mimi miaka 2 iliyopita...aisee siku nilipopata nishai nilimpiga kiswahili kwenye simu mpaka kikaeleweka....Maskini angejua ni pombe angekataa.by the way sikuwa namhitaji sasa....ila mpaka leo ananipigia akitumaini nitamkumbusha tulichoongea.
 
leo nimejikuta namkumbuka mjomba wangu mmoja.......
hivi...ambae niliwahi kwenda kuishi likizo moja nyumbani kwake....

nilikuwa sijui kuwa mjomba yule mlevi...mbwa...
alikuwa akija home anaonekana mstaarabu....
sasa usiku akirudi ameshalewa ndo anaitisha kikao cha familia....aisee
watoto wote wanaamshwa na mkewe anaitwa na watu wote tulio nyumbani kwake saa hizo

inawezekana ni saa nane au tisa usiku...watu wote wanaamshwa
halafu anaanza kutoa nasaha zake..lol...
ushauri na kuponda kwa wenye makosa na kadhalika...yaani....

yaani watu mna usingizi mnaamshwa kuelezwa umuhimu wa shule kwa mfano...lol..

sikurudi tena nyumbani kwake likizo ilipoisha...but nimekuja kugundua walevi weengi wana vituko mno majumbani mwao

na watoto waliolelewa na walevi wana visa viingi vya kusimulia...

hebu na nyinyi simulieni vyenu...basi.....

Wlevi wengi wana busara kuliko masober kaka... bet with me.
Halafu karibu walevi wote, ukiondoa wale wanaopigana wakiishalewa, wana tabia ya honesty... yaani ni wakweli hata kama ukweli huo ni wa kuumiza kiasi gani.
I love your uncle!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom