Kikaangoni na Tundu Lissu muda huu

Kikaangoni na Tundu Lissu muda huu

Ortega

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2011
Posts
844
Reaction score
209
Kikaangoni LIVE na Tundu Lissu kwenye page ya East Africa TV.

================

Chama cha Mapinduzi kimeozaa kabisa- Tundu Lissu

tundu2.png

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amefunguka na kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeoza. Tundu Lissu amefunguka hayo leo alipokuwa akichat live na mashabiki katika ukurasa wa facebook wa EATV katika

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akichat na mashabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV.

kipengele cha Kikaangoni ambacho huwa kinafanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi Alasiri, lakini kwa wiki hii kilishindwa kufanyika Jumatano kutokana na Mbunge huyo kupata dharura na kupelekea kufanyika leo.

Tundu Lissu amesema kuwa Mwalimu Nyerere alishawahi kuuliza swali kuna biashara gani Ikulu swali ambalo mpaka leo halijaweza kujibiwa na viongozi mbalimbali ndani ya CCM ambao wamekuwa wakiitafuta nafasi hiyo kwa gharama kubwa mno,lakini pia amesema wingi wa watia nia katika chama cha mapinduzi unathibitisha tuhuma za miaka mingi kuwa chama hicho hakiwezi kurekebishwa tena.

"Kwanza, kunaonyesha jinsi gani hicho chama kilivyooza. Mwalimu aliuliza swali ambalo halijawahi kujibiwa: 'Kuna biashara gani Ikulu hadi watu wanakimbilia kuingia humo'? Pili, kwa sababu ya wingi wa watia nia, CCM imethibitisha tuhuma zetu za miaka mingi kwamba hiki chama hakirekebishiki tena.

Lakini pia Tundu Lissu amezidi kufunguka kuwa moja ya mtia nia kupitia chama cha Mapinduzi ambaye ni Makongoro Nyerere amekiri wazi na kusema kuwa Chama cha Mapinduzi kimekamatwa na vibaka.

"Kumbuka alichosema mtia nia Makongoro Nyerere: 'Chama chetu kimekamatwa na vibaka!' Na kila mtia nia, ukimwacha Edward Lowassa, amedai kwamba atapiga vita rushwa iliyokithiri katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu."

WABUNGE UPINZANI KUTOKA BUNGENI
Siku za hivi karibuni wabunge wa upinzani waliamua kutoka bungeni baada ya kuona hawajatendewa haki na Spika wa Bunge ambae ni Anne Makinda hivyo mashabiki wa ukurasa wa facebook walitaka kujua kwanini wabunge hao waliamua kufanya maamuzi hayo badala ya kukomaa na kukabiliana na Chama tawala na hapo ndipo Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliposema kususia mkutano wa bunge ni moja ya njia ya mapambano ya kisiasa na ya kibunge.

"Kuna namna nyingi za mapambano ya kisiasa na ya kibunge. Kususia vikao ni mojawapo ya njia hizo za mapambano. Tumechaguliwa ili kuwawakilisha wananchi, sio kuhalalisha uharamia na uhalifu dhidi ya nchi yetu na wananchi. Sasa tunapoona kwamba uwepo wetu Bungeni unaweza kutumiwa kuhalalisha uharamia na usaliti wa taifa, choice tuliyo nayo ni kutoka nje na kupaaza sauti kwamba nchi inauzwa na maharamia.

Hii ni mbinu ya tangu zama za kale katika mwanzo wa Mabunge. Nitoe mfano mmoja maarufu. Kwenye Bunge la Uingereza kuna Wabunge wengi wa Chama cha Scottish National Party (SNP) na Sinn Feinn cha Ireland ya Kaskazini ambao wamechaguliwa kuwa Wabunge lakini hawajawahi kukanyaga kwenye Bunge la Uingereza kwa sababu wanadai uhuru wa nchi zao.

Wanaona kwamba kushiriki kwao katika Bunge la Westminster ni kuhalalisha utawala wa Uingereza katika nchi zao Scotland na Ireland." Aliongeza Tundu Lissu.

"Kwa vyovyote vile, Serikali mpya ya UKAWA haitakubali kuendelea na sheria ambazo hazina maslahi yoyote kwa nchi yetu na watu wake. Sheria zilizopitishwa kihuni namna hiyo na ambazo zinaweka rehani rasilimali zetu hatutazikubali. Gesi ambayo imegunduliwa katika eneo letu la Bahari ya Hindi inatakiwa itufaidishe sisi kwanza kabla haijanufaisha wageni. Ni serikali ya UKAWA pekee ndiyo inayoweza kuhakikisha kwamba hilo linafanyika." Aliongeza Tundu Lissu.

CCM WALIMTUMIA ZITTO KABWE KUTUGAWANYA NA KUTUVUNJA NGUVU
Mbunge Tundu Lissu amesema kuwa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alikuwa akitumiwa na Chama tawala kuwagawa na kuwavunja nguvu lakini kwa bahati mbaya huo mpango umeshindikana, ndiyo maana wapo watu waliamini kutimuliwa kwa Zitto Kabwe Chadema chama hicho kingeweza kufa au kupata maafa makubwa lakini imekuwa tofauti sana toka tumemfukuza Zitto Kabwe chama kimezidi kukuwa na chenye nguvu kuliko kipindi kingine chochote katika historia yetu.

"Zitto Kabwe ni hadithi ya jana, sio adui yetu nambari moja. Tulipomfukuza kwenye chama tulitabiriwa kiama na maafa makubwa. Hayakutokea. Chama chetu leo ni kikubwa na chenye nguvu kuliko katika kipindi kingine chochote katika historia yetu. Sisi hatuna, na hatujawahi kuwa, na chochote cha kuficha. Wamejaribu sana kutuchafua kwa mambo ya kutunga. Imeshindikana.

Walimtumia sana Zitto Kabwe kutugawanya na kutuvunja nguvu. Imeshindikana. Hatutaki kuondoa 'kasoro na mapungufu ya CCM', tunataka kuiondoa CCM yenyewe madarakani. Akina Yuda Iskariote hawatakosekana katika mapambano haya. Ndivyo ambavyo imekuwa zama zote zilizopita, ndivyo itakavyokuwa katika zama nyingi zinazokuja. Wajibu wetu ni kukabiliana na mayuda Iskariote hawa na kuwashinda."

TUNAWAGOMBEA WAZURI SANA UKAWA

Tundu Lissu ameweka wazi kuwa kupitia umoja wa vyama vya siasa ambao wanaunda UKAWA kwa mwaka huu wamekuwa tofauti sana na kusema kuwa wamekuwa na wagombea wazuri sana hivyo amezidi kuwaomba watanzania kujitokeza kuwapigia kura na kusubili matokeo na wasiishie kupiga kura na kuondoka vituoni.

"Msipige kura halafu mkaondoka vituoni. Hakikisheni mnabaki vituoni hadi hapo matokeo yatakapotangazwa.

pili, hakikisheni mnatusaidia kuweka mawakala katika kila kituo. Sisi tutajitahidi kuweka mawakala wazuri. Kama unajiona unaweza kuwa wakala, tafadhali jitokeze.

Tatu, mwaka huu ni tofauti sana na miaka yote ya nyuma. Tuna wagombea wazuri katika nafasi zote zinazogombaniwa: madiwani, wabunge na Rais. Uzoefu wetu umetuonyesha kwamba tunapokuwa na wagombea wazuri, tunapata mawakala wazuri na wananchi wanajitokeza kutupigia kura.

nne, mwaka tumehamasisha na tunaendelea kuhamasisha wananchi wenye sifa kujiandikisha kwenye BVR. Uzoefu wetu tena unatuonyesha kwamba tukihamasisha wapiga kura wanatu[igia kura. Kwa hiyo, msife moyo. Kura za zitalindwa kwa udi na kwa uvumba."

UNGEKUWA RAIS UNGEFANYA NINI
Mbunge Tundu Lissu alisema kuwa kama angepata nafasi ya kuwa rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania angeweza kufanya mabadiliko ya mifumo ya kiutawala na ya kufanya maamuzi, alizidi kusisitiza kuwa Rais wa nchi hii ana mamlaka makubwa sana kikatiba na kwa kiasi kikubwa yuko juu ya sheria.

"Kama ningekuwa rais wa Jamhuri wa Tanzania kwanza kabisa itakuwa ni kubadilisha mifumo ya kiutawala na ya kufanya maamuzi. Rais wa nchi hii ana mamlaka makubwa sana kikatiba na kwa kiasi kikubwa yuko juu ya sheria.

Kwa sababu ya mfumo huu, sio Rais tu, bali pia watu wake, mawaziri, wakuu wa taasisi za serikali, n.k. hawawajibiki kwa wananchi na kwa vyombo vya uwakilishi wa wananchi yaani Bunge. Tukitaka Rais aweze kuwajibika kwa ahadi anazotoa, lazima tupunguze madaraka makubwa aliyo nayo na kinga mbali mbali za kisheria na kikatiba zinazomfanya awe nusu Mungu.

Tukiweka utaratibu wa kumwajibisha Rais pale anapokosea, yeye na watu wake wataogopa kutuchezea na rasilmali za umma zitaheshimiwa."

 

Attachments

  • 11707739_1264461873568228_7385603538687158732_n.png
    11707739_1264461873568228_7385603538687158732_n.png
    60 KB · Views: 1,766
Huyu hana jipya tangu alipomtukana Nyerere hiyo dhambi itamtafuna kana ZITTO anavyotafunwa na dhambi ya usaliti.
 
Atwambie kwanini alimtukana nyerere mtu aliyetutoa utumwani mwenye heshima ya utakatifu katika taifa hili,
 
Tundu Lissu ni kweli ubunge umekuletea umasikini? Umejisikiaje baada ya serikali kupunguza kiinua mgongo cha wabunge ambacho ulikuwa umeishakipigia hesabu kukitumia wewe na familia yako?
 
Naomba kumuliza Lisu amejiandaaje kwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kuwasaidia wananchi wa majimbo mengine ya siginda nao waweze kupata uelewa wa haki zao na kuachana na mazoea ya kuchagua ccm.
 
Huyu mheshimiwa angekuwa anatoa hoja kwa utulivu na mtiririko km Zito angeweza kuliokoa sana Taifa hasa ktk kuepusha kupitisha madudu mengine yasiyoeleweka bungeni. Ila tatizo huwa anawaka sana kiasi cha kufanya spika atumie ubabe kumkalisha chini.

Sera yao ya kususia bunge inacost sana taifa, lakini pengine ni njia ya kuexpress kuwa hawajaridhishwa na jambo.

Ila kuna msemo: Ukisusa wenzio twala... sasa jamaa kweli wala tena watafuna haswaaa.

Mungu awajalie warejee tena mjengoni ila wabadili staili, siyo kukacha bungeni.
 
Sina swali zaidi ya kumpongeza kwa kazi kubwa anayofanya bungeni na jimboni mwake.
 
Tuna angalia hotuba ya mh Rais huyu hana jipya tangu ajuwe kuwa ni mpinzani basi anapinga hata mvua
 
Usituletee siasa maji taka hapa,tueleze nyie mnamwenzi vp nyerere?
 
Huyu mheshimiwa angekuwa anatoa hoja kwa utulivu na mtiririko km Zito angeweza kuliokoa sana Taifa hasa ktk kuepusha kupitisha madudu mengine yasiyoeleweka bungeni. Ila tatizo huwa anawaka sana kiasi cha kufanya spika atumie ubabe kumkalisha chini.

Sera yao ya kususia bunge inacost sana taifa, lakini pengine ni njia ya kuexpress kuwa hawajaridhishwa na jambo.

Ila kuna msemo: Ukisusa wenzio twala... sasa jamaa kweli wala tena watafuna haswaaa.

Mungu awajalie warejee tena mjengoni ila wabadili staili, siyo kukacha bungeni.
wamesusaje bunge wakati walifukuzwa na spika ili miswada ya ges ipitishwe na madudu yake kirahisi,? Kwenye hotuba ya mkulu hata wangekuwepo wangefanya nini?
 
Naomba kumuliza Lisu amejiandaaje kwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kuwasaidia wananchi wa majimbo mengine ya siginda nao waweze kupata uelewa wa haki zao na kuachana na mazoea ya kuchagua ccm.
Haya, muulize
 
Ni hatari kubwa kwa taifa kuwa na watu wanaojadiriana badala ya kujadiri masuala muhimu ya kitaifa. Lisu a personality ni tofauti na Lisu na hoja za bungeni na za kisiasa
 
Tundu lisu una mpango wa kugombea tena ubunge kwa awamu ya 5??
 
Nampongeza sana kwa jitihada zake katika kipindi chake chacha utumishi wake ila ushauri wangu wanatakiwa wafanye siasa za kujitoa uhai!
 
Tafadhari mtazame na kumsikiliza Tundu Lisu akifafanua mambo kibaao.

Yuko live hotmix muda huu, amekumbana na Thomas Ngawaiya, amepigwa maswali ya msingi na kuulizwa sababu za msingi za kususia bunge na kuonyesha dharau kwa kiti, hana jibu la maana zaidi ya kutoa mamifano yasiyokuwa na tija. Mara ooh hata wakati wa kugombea uhuru wa nchi za Afrika palikuwa na migomo mbalimbali kwa hiyo ndio wamegoma! Hasemi kasoro za muswada wala nini!
Source: Yuko live Hotmix eatv
 
Back
Top Bottom