Kijiweni na Mashabiki wa Ndala

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,350
3,451
Nikiwa nishaanza shamra za kusherekea ushindi mzito wa leo wa Simba S.C dhidi ya Ruvu.. Nipo kijiweni na mashabiki wa Ndala wakiwa wamenyong'onyea.. Kisa.. Mkata Umeme!!

Nasikia wakijadili kauli ya Kocha wao.. Kua Ndala wawe na uvumilivu na Mkata Umeme.. kwani jamaa alikua nje ya uwanja kwa mda wa miezi 6.

Hawa jamaa wamejiuliza maswali haya, wakakosa majibu;
1. Kabla ya kumsajili, Je walifahamu kua kwanini jamaa alifungiwa kucheza soka kwa mda wa miezi 6?
2. Kama walifahamu, kwanini walimsajili mtu ambaye hakua uwanjani mda mrefu?
3. Inakuaje Mkata Umeme analipwa zaidi ya milioni 5 akiwa benchi.. Huku wanaowapa ushindi mkiwalipa laki 8?
4. Twite alitimuliwa kisa umri.. Je mna taarifa Mkata Umeme ni kinda la miaka 36?

Wakuu zangu Sibonike Belo Nifah Guasa Amboni demigod Nyenyere juan de otaru libeva Blank page Konaball Mwana Mtoka Pabaya Bailly5 babake nasreen Frank Wanjiru Ulimakafu bila kumsahau ndugu yenu Makoye Matale... naomba mnipatie majibu.. niwape hawa Ndala kindakindaki wenzenu.

Muhudumu fanya mambo haya mawili mda huu, kipindi nasubiri majibu;
1. Niongezee kinywaji
2. Ongeza sauti ya huo wimbo... "... ama kweli wajinga ndo waliwao.. kekundu.. kekundu.. kekundu... ".
 
Mashabiki wa ndala wana mdomo sana...ngoja waendelee kuchezewa kekundu....

nilisikia saivi wanatembeza bakuli ili wapate hela ya kulipa mishahara....

Kanjibhai keshasepa.....ngoja waisome namba
Zile jeuri za kambi sijui Uturuki.. kwisha.. Na washukuru mvua zimekata msimu huu.. Lasivyo wangekua wanafanya mazoezi bwawani.
 
Mkata umeme hawezi kuwa 36!

Tambwe naye alizeeka ghafla baada ya mikia kukosea hesabu wakamtema akaenda International.

Leo mkijitahidi sana ni sare. Jamaa wameishajua hamna msamiati wa fair play Msimbazi. Baiskeli yenu ya miti itaanza mambo yake!

Nasikia mnamrudisha Serunkuma aje kuongeza nguvu?
 
Mbona Mavugo uliyesema rekodi zake za kufunga magoli ni sawa na Messi naye anakalia benchi siku hizi ?
Mkuu majibu yanahitajika.. Hayo ya Mavugoal tutayajadili siku nyingine.
 
Mkata umeme hawezi kuwa 36!

Tambwe naye alizeeka ghafla baada ya mikia kukosea hesabu wakamtema akaenda International.

Leo mkijitahidi sana ni sare. Jamaa wameishajua hamna msamiati wa fair play Msimbazi. Baiskeli yenu ya miti itaanza mambo yake!

Nasikia mnamrudisha Serunkuma aje kuongeza nguvu?
Mkuu naihifadhi hii kauli yako.. Nitarejea baada ya dk. 90.

ANGALIZO: Leo sipo eneo korofi.
 
Mkuu naihifadhi hii kauli yako.. Nitarejea baada ya dk. 90.

ANGALIZO: Leo sipo eneo korofi.
Afadhali ume declare haupo eneo korofi kimawasiliano.
Tuonane baada ya dakika 90 leo. Ukwell kuhusu baiskeli yenu utaanza kuonekana.
 
Wewe sembo sijui umekula maharage ya wapi. Jaribu hata ku-google kidogo utapata umri wa mkata umeme. Huyo na wengine ni wachezaji wa kulipwa, taarifa zao zipo.
 
Mkata umeme hawezi kuwa 36!

Tambwe naye alizeeka ghafla baada ya mikia kukosea hesabu wakamtema akaenda International.

Leo mkijitahidi sana ni sare. Jamaa wameishajua hamna msamiati wa fair play Msimbazi. Baiskeli yenu ya miti itaanza mambo yake!

Nasikia mnamrudisha Serunkuma aje kuongeza nguvu?
Acha akili za uccm ndala fc wewe
 
Wewe sembo sijui umekula maharage ya wapi. Jaribu hata ku-google kidogo utapata umri wa mkata umeme. Huyo na wengine ni wachezaji wa kulipwa, taarifa zao zipo.
Haha.. Mkuu sio mimi niliyosema hayo.. Ni mashabiki wenzako wa Ndala.. Na vipi kuhusu majibu ya hayo maswali mengine?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom